Tatizo la ukosefu ama tuite nishati dhoofu hapa nchini si la kisera bali la kisela..yes, haiweekani jambo serious lichukuliwe ki comedian. Sitashangaa kesho tukisikia uteuzi wa kaimu- makamu wa naibu waziri ambaye atakuwa superintendent wa mito na mabwawa.
Wengine hutumia magazijuto kuelekea mechi ambayo fundi hakuweka vizuri pima maji mengi yalikua yakipita juu ya vidonda vya tumbo mbuzi yule hakula majani jeshini baada ya bei ya nondo kupanda mwalimu akashauri tutumie daftari la mistari midogo ili kukabiliana na utelezi wakati wa kuotesha nyaya...
Kwa kua wanasiasa ndo wamekua waamuzi wa kila kitu dhidi ya wananchi basi nawashauri wote waliohitimu kidato cha sita wachukue mchepuo wa Sayansi ya Siasa na uongozi wa uma kwa miaka mitatu tu kisha waingie bungeni walau kwa miaka miwili kisha miaka mitano ijayo waje hapa kutoa shukrani!
Kama niwazavyo ni sahihi basi tuwe na roho ya kiungwana kabisa kukubali hata kuichangia serikali nusu ya kila tulicho nacho kwa kuwa tulikubali bila shuruti kubatizwa kuwa wanyonge. Tuauige mfano wa enzi za utawala wa ki chief ambapo wananchi walikuwa wanaporwa kila kitu in the name of royal family.
Bado sasa tutakatwa tozo kwenye ndoa,kisha tozo kwenye imani na mwisho kabisa tozo ya ongezeko wa thamani kwenye uhai, kila mwananchi alipe 10% ya ongezeko wa umri na akishindwa kulipa sheria kali za wanasiasa zichukue mkondo wake.
Tanzania kabla ya kuchagua wanasiasa wananchi wana nguvu na thamani sana ila baada ya kuchagua wanasiasa wana nguvu maradufu ya kupanga hata hatma za wananchi. Huu ni upuuzi ambao wenye akili wasipoukemea kwa busara itafika wakati wasio na akili watatumia ujamaa wao kuangamiza taifa. It is a...
Hakuna lisilowezekana chini ya jua kama wanasiasa wangeacha ubinafsi pembeni na kutanguliza maslahi mapana ya nchi mbele. Ifahamike kwamba watawala watakuja na kupita ila taifa litabaki! Katiba mama wa sheria zote duniani na mlezi mzuri ni lazima awe na familia bora!
Swali lako ni mtambuka kwa kuwa kuishi maisha affordable kuna factor nnyingi za msingi kuangalia. Mathalani unaweza kupata nyumba ya bei rahisi kupanga ila gharama za maisha kwa maana ya nauli na mahitaji mengine ya muhimu ikawa juu.
Kwa mantiki hiyo ni lazima tufahamu aina ya shughuli zako ili...
Ndoa ni kukaa pamoja na kutatua matatizo ambayo msingekuwa nayo kama msingeoana...Uamuzi ni mmoja tu hapa,ama kumpenda mwenzi wako kama alivyo ama usubiri akuue kisha tukupe ushauri.
Vitabu vya dini vinatuasa tusijihusishe kwenye vitendo vya kuzini kabla ya ndoa wakati huo huo tunawekewa viuongo vya ndoa kabla...so hapa nashauri akili za kuambiwa uchanganye na za kwako.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.