SAKATA LA ESCROW: Vigogo watatu Benki Kuu, Tanesco na TRA kortini Kisutu Dar leo. Watuhumiwa kwa ufisadi wa akaunti ya Tegeta Escrow, taarifa zaidi kukujia.
VUMBI LAFUNIKA ANGA: Vumbi zito latishia uhai wa wakazi wa Gairo, Kibaigwa, Kongwa na Dodoma mjini jioni hii; lazagaa na kutanda angani; watu wajifungia ndani.
TAARIFA YA KUKOSEKANA HUDUMA YA MAJI KWA SIKU MBILI JIJINI DAR
Dawasco inawatangazia wakazi wote wa jiji la Dar es salaam na Mji wa Bagamoyo kuwa mtambo wa kuzalisha Maji wa Ruvu Chini utazimwa kwa wastani wa saa 48 kwa siku za Alhamisi na Iijumaa ya tarehe 30 na 31 Octoba 2014, kuanzia saa...
UKAWA: Prof Lipumba amesema leo Dar es Salaam kuwa Ukawa watakutana Oktoba 26, kusaini makubaliano yao ya kumweka mgombea mmoja katika ngazi zote za uchaguzi.
VURUGU MARA: Wanajeshi 6 JWTZ jioni hii wavamia kituo cha polisi cha Tarime na kuwapiga polisi baada ya mwenzao kukamatwa, RPC Lazaro Mambosasa athibitisha.
CHANZO: Mwananchi
MAAFA RUVUMA: Watu 200 katika Kijiji cha Litapwasi wamenusurika kufa baada ya kunywa pombe (Togwa) inayodhaniwa kuwa na sumu. Tukio hilo limetokea katika sherehe iliyokua ikifanyika katika kijiji cha Litapwasi, kata ya Mpitimbi. Baadhi ya wahanga wa tukio hilo wamelazwa hospitali ya misheni...
CHADEMA WAANDAMANA: Polisi Kinondoni wawadhibiti kwa mabomu ya machozi wafuasi wa Chadema Kata ya Manzese jijini Dar es Salaam leo wanaopinga mchato wa katiba.
JELA MIAKA 60 GEITA: Mahakama wilayani Bukombe jana imemhukumu Luzelela Shibu (51) kifungo cha miaka 60 jela kwa kumbaka na kumlawiti kikongwe wa miaka 63.
VURUGU, MAUAJI LINDI: Mlinzi wa Durbhai Amin amuua kijana (miaka 22) kwa risasi wakati akipita kwenye shamba la mmiliki huyo leo. Wanakijiji Makwaya waandamana
KESI DHIDI YA BUNGE: Mahakama Kuu Dar yatupa ombi la serikali leo kutaka kesi ya TLS dhidi ya Bunge la Katiba isisikilizwe. Kesi ya msingi kuendelea.
============================
Chanzo:Mwananchi
TAMKO LA SERIKALI BUNGENI: Waziri DK A. Migiro atangaza bungeni mjini Dodoma jioni hii kuwa mjadala wa kusitishwa Bunge hilo umefungwa rasmi, na liko kihalali.
MAUAJI GEITA: IGP E. Mangu leo ametangaza bingo ya Sh10m kwa mtoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwa watu waliovamia kituo cha polisi jana usiku mkoani Geita.
Mwanafunzi wa Kijerumani aliyewasili Rwanda kutoka Liberia amewekwa kwenye karantini mjini Kigali akiwa na dalili zinazofanana na za ugonjwa wa Ebola.
==============
CHANZO: Mtanzania
=====================
Waliohofiwa kuwa na Ebola wagundulika kutokuwa na ugonjwa huo. Kwa taarifa zaidi...
HABARI! JAKAYA THEATRE ARTS WAKISHIRIKIANA NA TANZANIA ARTIST'S TOURNAMENT (TAT) Tunapenda kuwaalika katika bonanza la wasanii wa makundi yote ya sanaa Dar es salaam litakalofanyika kuanzia tar 16/08/2014,
Lengo kubwa likiwa ni kujenga urafiki na ushirikiano pia kujitangaza kwa kazi zetu...
Israel imewaita wanajeshi 16,000 zaidi wa akiba kuimarisha vikosi vinavyopigana Gaza, huku Marekani ikiiruhusu kutumia maroketi yake yaliyohifadhiwa huko.
===========================================
Gaza City (Palestinian Territories) (AFP) - Israel vowed Thursday it would not pull troops out...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.