Hapa nikitamka kwamba kwa hali ilipofikia haitakuwa sahihi mzigo huu kwa kuanzia akabebeshwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali? La sivyo tuonyeshwe aliishauri nini serikali. Kama ushauri alitoa kupinga swala hilo na serikali haikuzingatia ushauri huo, kwanini basi hakujiuzulu?
Hapa ndipo tatizo la siasa zetu lilipo. Hakuna atakayekubali jina lake kutajwa kuwa alihusika na kuandaa mkataba uliozaa janga hili. Hasa alieweka sahihi kuidhinisha jambo hilo angetolewa hadharani tukamfahamu au tukawafahamu.
Hii mada imekaa kama kitu mtu kajitungia tu kaleta hapa na watu wanapoteza muda wao buree. mleta hii mada hebu tuwekee video yake akiyazungumza hayo uliyoandika.
Hilo wengi tulidhania hivyo tangu ile siku ya kwanza. Lakini kukosekana tamko lolote la uhakika kupinga tamko ambalo limesemwa wazi kwenye mahojiano kama yale unaweza kutafsiri vipi?.
sasa mbona hatuelewi tatizo ni hatukufuata taratibu au wao ndiyo hawakufuata makubaliano? Mamlaka itoe maelezo kwa Taifa ili tufahamu ni nani alikurupuka.
Kama barua kama ile inaweza kuandikwa na kuwekwa wazi namna ile halafu inakuja kugundulika kuwa Tanzania tulikurupuka, aliyesaini ile barua...
Mfumo wa dili ndiyo tatizo wala siyo maji ya bwawa. Kwanza ukitaka kujua kwamba hilo bwawa halitakuja kulissaidia Taifa angalia mkandarasi aliyepewa hilo jukumu. Hana experience nzuri au stahiki ya kufanya kazi hiyo. Visingizio anavyotoa vya kuchelewesha ni vya kukosa "proper planning". Pili...
Tatizo kama unavyosema siyo kukopa, bali kukopa kwa kuzingatia vipaumbele vya kitaifa, mipango iwe thabiti na usimamizi mahiri wa matumizi ya hiyo mikopo na utekelezaji wa miradi. Usimamizi huo unaweza tu kuwa na mafanikio na kuwa endelevu kama kutakuwa na sheria katili za kuhakikisha wanaokiuka...
Jiulize ni kwanini tuko mahiri sana kutafuta mikopo lakini yanapokuja maswala ya kujitetea kwenye kesi za mahakama za biashara za kimataifa hata kuongea hatuwezi??
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.