Search results

  1. MATHIAS KABYEMERA

    Yupo wapi Edie Ganzel

    Kama ni utunzi wa hadithi, namkumbuka sana Edie Ganzel. Sina uhakika kama ana uhusiano na Stanley Ganzel wa TBC ila hadithi yake ya “SIKUWA FUKARA” naikumbuka sana. Nikiona wanavyotahabika wanufaika wa serikali za awamu ya pili hadi nne, waliofutwa vyeti feki, waliotumbuliwa n.k, natamani...
  2. MATHIAS KABYEMERA

    Rais, saidia kupunguza gharama za vifaa vya Ujenzi watanzania tujenge makazi yetu!

    Nadhani bado watanzania mnakumbuka kuwa Kagera tulikumbwa na tetemeko la ardhi. Nyumba zetu nyingi zilibomoka kabisa na nyingine nyingi zilipata nyufa ambazo zililazimu kubomolewa kabisa au zilihitaji matengenezo makubwa. Kwa bahati mbaya sisi raia hatukupata msaada wa vifaa vya ujenzi au ruzuku...
  3. MATHIAS KABYEMERA

    CECAFA yakwepa yaliyoikuta sportpesa super cup

    Mara nyingi mechi za watani huwa zinapata attention kubwa. Kwa jinsi Sportpesa super cup ilivyopanga ratiba yake katika michuano inayoendelea Kenya ilionekana wazi walipanga nusu fainali iwe Simba na Yanga na Ghor Mahia na AFC Leopards. Lakini mambo hayakuwa hivyo ikaishia Simba kukutana na...
  4. MATHIAS KABYEMERA

    Tanzania kuwalipa wasichana 25,000 kupunguza maambukizi ya VVU/UKIMWI

    Serikali imepanga kumlipa msichana mwenye umri kati ya miaka 10 - 22 Tsh. 25,000 kila mwezi ili kumpunguzia vishawishi vya ngono. Mradi huu utafanyika kwa majaribio katika wilaya zote za mkoa wa Singida, Dodoma na Morogoro. Hii imetokana na utafiti ulioonesha kuwa kwa vijana wenye umri wa...
  5. MATHIAS KABYEMERA

    Afrika kusini yazindua mpango wa kujenga vyoo vya kisasa shule za msingi

    Kutokana na matukio ya wanafunzi kufa kwa kutumbukia katika vyoo vya mashimo katika shule za msingi, rais wa Afrika Kusini kapiga marufuku matumizi ya vyoo hivyo na kuanza mchakato wa kujenga vyoo vya kisasa nchi nzima. Unadhani kwa Tanzania, kipi kiwe kipaumbele katika shule za msingi kati ya...
  6. MATHIAS KABYEMERA

    Ndege ya Shirika la Condor iliyokuwa ikielekea Zanzibar yatua kwa dharura Mombasa

    Ndege ya Shirika la Ujerumani Condor imetua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Moi Mombasa. Ndege hiyo ilikuwa ikipeleka watalii Zanzibar. Abiria wamehairisha safari na kupelekwa hotelini wakisubiri ndege nyingine ili kuendelea na safari. ----- A plane belonging to German leisure airline...
  7. MATHIAS KABYEMERA

    Kwa hili wamiliki wa mitandao ya simu mnatuonea

    Mtu umepoteza simu, unaambiwa uende na kitambulisho halali. Unakibeba wanakuomba photocopy yake unaitoa. Mwisho wa siku wanakuambia utaje namba tano ulizokuwa unawasiliana nao. Nizitaje kutoka wapi wakati simu imeibiwa. kama hili ndilo hitaji, kwanini nilete vitambulisho? Nadhani hapa...
  8. MATHIAS KABYEMERA

    TANZIA: Urbadius Kidavuli aliyekuwa Katibu Mtendaji Idara ya Utume wa Walei afariki

    Fr. Urbadius Kidavuli aliyekuwa Katibu mtendaji Idara ya Utume wa Walei baraza la Maaskofu Tanzania (TEC) amefariki. Katika hali ya kushangaza, yeye anatoka jimbo la same na hivyo kuwa ni padre wa tatu wa jimbo la Same kufariki ndani ya siku tatu tu. Mungu ampe pumuziko la milele mbinguni. AMINA
  9. MATHIAS KABYEMERA

    HIVI NANI ANAPIGA AVATAR ZA JF?

    Kuna kipindi nikiwa bored huwa napita JF kusoma habari. Mimi sio mtu wa kutoa comments kwenye mada nisizokuwa na cha kuchangia. Ila wakati mwingine huwa naangalia profile photos maarufu kama avator. Ni kati ya vitu vinavyonivutia sana JF kwasababu nashindwa kuelewa aliyepiga picha hizo alikuwa...
  10. MATHIAS KABYEMERA

    Kwanini jana kwenye Europa league yametawala mabao matatu

    FC Astana 1 - 3 Sporting CP FT Borussia Dortmund 3 - 2 Atalanta FT Ludogorets Razgrad 0 - 3AC Milan FT Marseille 3 - 0 Braga FT Nice 2 - 3Lokomotiv Moscow FT Oestersunds FK 0 - 3Arsenal FT Real Sociedad 2 - 2Salzburg FT Spartak Moscow 1 - 3 Athletic Bilbao FT AEK Athens 1 - 1Dynamo Kyiv...
  11. MATHIAS KABYEMERA

    Pole rafiki yangu! Nawajulisha na wengine wajipange wasije wakaumbuka

    Kila mwaka inajulikana kwa ndugu zetu wa Kilimanjaro kusafiri mwishoni mwa mwaka kusherehekea sikukuu na jamaa zao. Ni jambo zuri na la kuigwa. Ila wengine huwa hawana nauli hivyo hudandia maroli ya mizigo. Sasa mwenzangu nae kadandia roli wakati anarudi. Wamefika katikati ya safari, ni usiku...
  12. MATHIAS KABYEMERA

    KATIKA MABADIRIKO YA SHERIA ZA MPIRA KIPI UMAKIKOSA?

    FIFA imefanya mabadiriko na marekebisho kadha wa kadha katika sheria, taratibu na kanuni za mpira wa miguu. Binafsi natamani wangerudisha "GOLDEN GOAL" ambalo lingefungwa tu kwenye dakika 30 za nyongeza mechi inaishia hapo. Je, wewe unamiss nini?
  13. MATHIAS KABYEMERA

    Kulipia mahari kwa watu wasiokuwepo ni haki?

    Kutoa mahari ni jambo la utamaduni. sio malipo kama wengine wanavyodai ila ni heshima kwa waliomlea mkeo. Sasa nashangaa mtu anadaiwa mahari ya watu ambao hawakuwahi kuwepo au walishafariki. Mfano 1. Babu na Bibi kumbe walishafariki 2. Mjomba kumbe mama anazaliwa peke yake 3. Shangazi kumbe baba...
  14. MATHIAS KABYEMERA

    Kwaheri wana Dar es salaam, Tunashukuru kwa matusi yenu

    Wiku hii wakazi wa Dar es salaam mliokuwa mmekuja kula sikukuu mikoani mnaanza kurejea makwenu. Tunashukuru kwa matusi yenu kuwa sisi ni washamba, hatujui kuendesha magari wakati mmekodi magari yetu n.k Inashangaza sana. Hawa jamaa ni wazaliwa wa huku, unakuta sisi tuna maisha bora kuliko wao...
  15. MATHIAS KABYEMERA

    Mwanaume kumchungulia mwanaume mwezie anakuwa anataka nini?

    Ninapokaa ni karibu na mto. Vijana wanaofanya vibarua huja kuoga jioni baada ya kazi. Kuna vijana wameweka kijiwe hapo kwa lengo la kuwaangalia wenzao wakioga na baada ya hapo huanza kupiga stori, fulani ana mzigo, au wa fulani ni wa kawaida sio kama wa fulani. Hawa wana maana gani?
  16. MATHIAS KABYEMERA

    Mchungaji afariki dunia baada ya kufunga siku 30; alitaka kuvunja rekodi ya Yesu Kristu

    Mchungaji wa Afrika Kusini Alfred Ndlovu (44) amefariki baada ya kufunga usiku na mchana kwa siku thelathini akitaka kuvunja rekodi ya Yesu Kristu aliyefunga siku 40 usiku na mchana bila kula wala kunywa kitu chochote. Mchungaji Alfred aliondoka nyumbani kwake tarehe 17/6/2016 na kuelekea...
  17. MATHIAS KABYEMERA

    Kifaa cha kudhibiti matumizi ya fedha chazinduliwa(chanzo BBC SWAHILI)

    Kampuni mmoja ya uingereza inatarajia kuweka kifaa kinachodhibiti matumizi ya pesa kwa kuwapatia wateja wake mshtuko wa umeme iwapo watapitisha kiwango cha matumizi yao. Kampuni ya Intelligent Environments,imezindua mfumo ambao utaiunganisha na mpiro wa kuvaliwa mkononi wa Pavlok ambao unatoa...
Back
Top Bottom