Namshangaa sana Rais Kikwete. Kule Mwakata, Kahama watu kama 40 wamekufa na wengine wengi wameathirika vibaya sana kwa mvua na upepo mkali, yeye anajitia kwenye pipa huyo anaelekea Ruanda. Hawa ndiyo viongozi wetu na viongozi wa chama tawala. Hawajali maisha ya watu hata kidogo si kwa wakati wa...
Wangwanga hii topic ni tamu. Siku zote nikijiuliza jukumu la wasomi, hasa wanaotoka UDSM, katika kuleta mabadiliko katika nchi. Nasema wasomi hasa UDSM kwa sababu ndiyo chuo kikuu chetu cha mwanzo hapa TZ. Matarajio yetu ilikuwa chuo hichi kiongoze katika kuleta maendeleo na mabadiliko ya...
Kigogo na wenzekao mnaounga mkono unyama wa polisi Tanzania, naona mnafikiri baina ya miguu miwili tu. Bahati mbaya hamfikirii mbali hata kidogo Lakini Waswahili walisema, "Tumbili (kima) wakimaliza miti huja mwilini". Kwa hivyo hiyo miti itamaliza siku moja na mtawaona ndani miili yenu...
Tanzania ndiyo siku zote tusipige hatua mbele kwa sababu Watanzania kusema kweli wanaogopa kuchekwa. Kusema polisi kanipiga tunaogopa kuchekwa, kusema kiongozi au mkuu wangu kazini kanitongoza au kaniomba ngono tunagopa kuchekwa. Hii"taboo" ya kuogopa kuchekwa lazima iondoshwe katika akili za...
Haya wale wanaojinata kwa Tanzania kuwa ni nchi ya sheria na haki. Tanzania chini ya CCM hakuna sheria ni haki. Mamboa yanavyokwenda ni kuwa ama ukubaliane na CCM au wakudhalilishe. Tokea litokee tendo hili na watuhumiwa kusema mbele ya mahkama na kuripotiwa na vyombo kadhaa vya habari...
Hili ni la Tanganyika kwa hivyo ni uhalifu. Lingalikuwa ni la Zanzibar lingalikuwa la ugaidi. Sasa leteni FBI na hili wasidie uchunguzi. Au uchunguzi wa hili si muhimu?
Kwanza poleni sana ndugu zetu wa Songea na Tanganyika kwa jumla. Habari ya kusikitisha sana.
Sipendi kusema haya kwa furaha lakini inabidi niseme kama ukumbusho kwa yaliopita, yaliopo na yajayo kwa nchi yetu au Tanganyika na Zanzibar. Huko nyuma wenzetu wa Tanganyika walizowea kusikia...
Jamani marais hao hawapendi kudanganywa. Hakuna nchi inayoitwa Tanzania ambayo imetimiza miaka 50 ya uhuru. Tuweni wakweli. Hivi tunavyofanya tunaandika historia ya vizazi vyetu. Vizazi vyetu vitakuja kutusuta, jamani hawa mababu zetu walikuwa wamesoma au angalau walikuwa wanajihangaisha kutumia...
Masahihisho ndugu Amoeba: Hapana Muungano kati ya Tanzania na Zanzibar, bali ni baina ya Tanganyika na Zanzibar. Tanzania ilizaliwa baada ya huo unaoitwa Muungano.
Muungano ni lazima ujadiliwe tena kwa undani, siyo juu. Hautaki kupigwa brush huo. Nahisi Wananchi wengi wa Tanganyika hawajuwi hasa huu Muungano una lengo gani. Wanabebeshwa mzigo wasioujuwa.Ni tofauti sana na wananchi wengi wa Zanzibar. Wao wanaelewa Muungano una malengo gani.
Wasiotaka...
Ndugu zangu wa Tanganyika naona emotions zinakuchukuweni sana. Wengine hata hamjuwi mnazungumza nini, mamo tu kwenye mdundiko. Fanyeni utafiti wa haya mambo. Quran ilichomwa moto huko Zanzibar na Mtanganyika na hatukuona hamasa au emotions kama hizi na wala hatukuvisikia vyombo vya habari...
Tusiwe wenye hamasa kiasi hicho. Kesi iko mahkamani, kwa nini hatuiachii sheria kuchukuwa mkondo wake. Kwa nini moja kwa moja tunafanya tathmini (conclusion) kuwa ni dalili tosha Wazanzibari hawautaki Muungano. Huu Muungano uliopo ni wa viongozi wa Serikali na uhusiano wa watu utakuwepo pale...
Ndugu wanaforum,
Binafsi nampongeza Bi Sofia Simba kwa ushujaa wake. Hii aliyoitowa mwanamama huyu ni kweli isiyo na doa kuhusu CCM na ufisadi. Uliojaa ndani ya CCM ni ufisadi ufisadi ufisadi na kama hutaki kushirikiana na ufisadi ndani ya CCM ni vigumu sana kuendelea. Mambo yatadhihirika...
Ukweli kushambuliwa kwa mzee Mwinyi si suluhisho la tatizo na wala si ustaarabu aliopaswa huyu kijana kuonesha. Pegnine anahitaji mchakato wa jinsi ya kujibu mambo asiyokubaliana nayo wakati wa mazungumzo au mijadala.
Kijana kafanya kosa lakini vile vile kwa nilivyoona katika video na kusoma...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.