Nyani Ngabu,
hongera kwa huu uzi. Uzi huu ukitumika vizuri utarudisha kule tulikokuwa JF, kama uwanja wa kuelimishana, kupashana, kuwaidhiana nk, na si uwanja wa matusi, kebehi nk.
Kila la heri wana JF wote.
Mpe haki yake bana, mahakama ndio itajua kuwa alikuwa na makosa ama la, sio suala la kuangalia yaliyopita huko shuleni. Jamaa yuko rumande, anafuata nyayo za Baba yake aliyetuhumiwa kutaka kumpindua Mwalimu.
Tatizo "mfumo kristo" umeanza kutingishika. Maaskofu hawaishi vituko, wanashindwa kujibu hoja za Waislam kwa kutaka Serikali iwajibie. Hilo halishangazi, manake ndio mfumo huo. Tamko kama hili likitolewa na Waislam huo ni uchochezi, lakini upande wa pili ni haki yao. Haya yananikumbusha yale ya...
Katika vitu ambavyo tunatakiwa kushikamana ni wakati wa chokochoko ya vita. Sidhani kama una uzalendo kwa haya unayoandika, leo hii TZ ikipigana na Malawi waumiao ni ndugu zetu walioko kule mpakan na wapiganaji wetu, wengine nao tutaumia manake itabidi mambo mengi yasimame kwa ajili ya vita...
DM, kuzindua ramani mpya ni jambo la kawaida mno, manake TZ sasa ina Mikoa na Wilaya mpya. Sasa katika kuliweka hilo ulitaka mpaka usiweke, na kama ingekuwa hivyo mbona ramani zao wao wanaweka mpaka mwisho wa maji?. Pia tokea nakuwa ramani zinazotengenezwa na TZ zina mpaka katikati ya maji...
Hawa wanakuwa 9, ndani ya hao CCM walikuwa nao 8 na mmoja upinzani. Wa CCM 8, watano wanatoka Bara na watatu Visiwani. Ila huyo mmoja wa upinzani, huwa anachaguliwa kwa mizengwe, sababu kura nyingi zinatoka CCM basi huchaguliwa yule wanayemuona anatoka ktk chama kidogo kinachoendana na CCM, ama...
Yani inachefua kupitiliza, alishasema kuwa posho zimeongezwa kwa kuwa maisha Dodoma gharama zimepanda. Sasa kuna justification gani walipwe siku tano tu, ina maana Jumamosi na Jumapili (siku za mapumziko) maisha hayako juu. Pia Serikali ipandishe posho za kila mtumishi akiwa Dodoma, ina maana...
Nami nichangie kidogo. Mwaka huo pia alikuwepo mwana mama aliyechukua fomu, naye alikuwa ni Bi. Rose Lugendo. Ila alipata wakati mgumu alipoingia kwa usaili mbele ya Nyerere.
Kama alivyosema Mkandala, Nyerere alimuomba Dk. Salim aje agombee, wakati huo Salim alikuwa Katibu Mkuu wa OAU. Salim...
Alichapwa maswali 9 kati ya mangapi akashindwa?, hata kama yote 9 alijibu hajui inategemea aliulizwa maswali gani. Sio kila uki-present watu huuliza katika areas zako. Mtu anaweza uliza swali kutokana na anachokijua kwa kufananisha na ulicho-present, na kuwa muwazi hutakiwi danganya.
Kuna maswali ya kujiuliza
1. Wakati gani mtu hufanyiwa vetting?
2. Vetting hudumu kwa muda gani?
Huyu Jaji Othman alishafanyiwa vetting, ndio akateuliwa na Rais kuwa Jaji katika Mhakama ya Rufaa. Kelele kuwa ndugu yake (sina uhakika) Rashid Othman kampendelea katika vetting zingeanza...
Kweli ni huzuni kubwa, alikuwa mtu mcheshi, mwenye hekima, busara na msaada mkubwa. Nakumbuka nilikutana naye ofisini kwake tarehe 27/10/2010. Tuliongea kwa muda wa kama dk 20. Ninapoumia zaidi ni pale ninapokumbuka yale tuliyozungumza na kupanga kuanza kuyafanyia kazi katikati ya mwezi wa 12...
Wakati Mahabusu wanafariki Mbeya, Mwema alikuwa likizo. Wale waliotuhumiwa kuwaweka Mahabusu katika chumba kidogo ambao walikuwa Maaskari, walikamatwa na kuwekwa ndani kusubiri kosa la kusababisha vifo. Lakini nao wakatoroka, Mwema akaahirisha likizo kwenda kushiriki zoezi la kuwatafuta...
Katibu Mkuu Kiongozi (KMK) hustaafu kama viongozi wengine, mfano makatibu na manaibu katibu wakuu wa Wizara. KMK hayuko katika kundi la viongozi wa kisiasa ambao hawana suala la kustaafu kama Mawaziri, Wakuu wa Mikoa nk.
Kweli muda wake wa kustaafu ulifika, lakini akaongezewa muda. Hilo la...
Kigoma kusini nani mshindi?, manake kwa mujibu wa hiyo tovuti ya Bunge wameandika majina mawili kwa jimbo moja la Kigoma Kusini. Wameorodheshwa GULAMHUSSEIN SHABANI KIFU wa CCM na DAVID ZACHARIA KAFULILA wa NCCR-MAGEUZI.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.