Huku Tanganyika kwa wasiojitambua, huyo Kitila Mkumbo si ajabu angepokelewa kwa vifijo na nderemo.
Huko visiwani naona kashushwa kutoka mawinguni anakovinjari na kurudishwa maskani kwake ardhini.
Hongera zake huyo mama...kwa sisi wakongwe wa JF katukumbusha zama za kumkoma nyani giledi..
Kwa...
Hii nchi ni ya wanafiki hivyo inaongozwa kinafiki na hilo ndilo tatizo letu sugu. Watawala na watawaliwa wote kwa pamoja tunajua kuwa tatizo kuu ni CCM.
Sasa cha ajabu...wanaokiri ukweli huo hawajai hata kwenye kiganja cha mkono. Kwa unafiki wao wengi wako tayari kuwabebesha lawama...
Duh! Kweli ndege wafananao daima huruka pamoja.
Hivyo hivyo chawa, mende na nzi wanajua pahala pao.
Ni kweli pia huwezi ukapanda mchicha ukavuna nyanya.
Pole sana Crocodiletooth, cha kuvunda halina ubani.
Achana na hilo lichawa lisilo na akili.
Chakula kitamu kimewekwa mezani, wewe unakaribisha ma inzi, wa nini?
Umetandika kitanda upate usingizi mnono, wewe unawaita chawa, wa nini?
Hivi sifa za uchawa ni zipi?
Very true, wewe si chawa, wewe ni binadamu! JF hakika imeshuka hadhi, si tena kile kisiwa cha hekima...ni kambi ya unafiki.
Achana nao, wengi wao ni watoto wasiojua tulikotoka na viongozi kama Ali Hasan Mwinyi aliyeigeuza Ikulu yetu Takatifu kuwa pango ya walanguzi.
Hawajui walikopotelea tausi waliotapakaa katika viwanja vya Karimjee na kuwa kivutio tosha kwa wageni waliobahatika kutembelea viwanja hivyo.
Hawajui...
Watu wa aina yako wewe na Pascal Mayalla, hakika hamuitendei haki taifa la Tanzania. Raisi akishatangazwa anaapa kwamba ataiheshimu, atailinda na kuitetea Katiba.
Baba wa Taifa aliwahi kumkemea aliyekuwa Rais wa Namibia, Sam Nujoma, kwa kumuonya kuwa Katiba si kama nguo, si shati la wewe...
Kwa Tanganyika umeme umekuwa anasa.
Kwa vipofu wasioona mwanga ni anasa.
Kwa sasa giza kwetu ni fahari.
Eti wapo wanaolilia umeme...wa nini?
Mbona mababu zetu waliishi bila shida?
Hawakuwa na umeme.
Watanganyika ni watu wa ajabu kweli kweli.
Tunadai kuishi kivyetu hatutaki kusihi kivyao!
Mbona...
Ninachoweza kusema kwa hakika na kwa kujiamini ni kwamba wewe ndiye mpumbavu. Tatizo la mpumbavu ni kwamba anaamini anajua kumbe hajui. Pumbavu hafichi ujinga wake, hapana, anauanika akiamini anachosema ni sahihi. Poor Tanzania, watu wa aina yako ndio hao hao wametamalaki nchini. Usiku mwema...
Hapana mkuu...kula, kushiba na kunenepa si lazima ukae meza kuu, unaweza kukaa meza ya pembeni ukala, ukashiba na kunenepa kwa kupitishiwa makombo.
Au unaweza kukaa chini ya meza ukala, ukashiba na ukanenepa kwa makombo yanayodondoka ama kwa makusudi au kwa bahati mbaya mradi unauma na...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.