Kwanza kabisa ili kuweza kuelewa dhana hii kwa ufasaha, ni LAZIMA upate fursa japo kwa uchache kusoma nyaraka zifuatazo
1. Katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977(The Constitution of the United Republic of Tanzania,1977)
2. Katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, toleo 2010(...
KWA NINI MHESHIMIWA NDUGAI AMEJIUZURU
Katika siku za karibuni nchi yetu imepatwa na moja ya tukio kubwa kabisa katika medani za uongozi wa kisiasa, tukio hilo ni ile hatua ya aliyekuwa Spika wa Bunge la 12 la jamhuri ya muungano wa Tanzania mheshimiwa Job Yustino Ndugai kujiuzuru nafasi...
Hicho kikundi cha watu wa ovyo anachokisema mheshimiwa Rais wetu, kinaonekana ni kama kina watu wenye nguvu kubwa sana
Sasa sijui ni kina nani hao wenye nguvu kubwa kiasi hicho?
Ni matumaini yangu, kwa nguvu kubwa za kikatiba alizonazo mheshimiwa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania...
Ukisoma katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kwenye ibara ya 54(3) inataja baraza la mawaziri ndio chombo kikuuu cha kikatiba cha kumshauri mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwenye mambo yanayohusu utekelezaji wa majukumu yake ya Urais
Sasa kama kuna...
Nchi yetu kwa sasa imepata changamoto ya upungufu wa mvua, hii ni kwa mujibu wa mamlaka ya hali ya hewa nchini (TMA), jambo lililopelekea upungufu wa uzalishaji wa umeme hapa nchini, hiyo ni kwa mujibu wa taarifa kwa umma iliyotolewa na shirika letu la umeme hapa nchini (Tanesco) jana tarehe...
Mwaka 2006, nchi yetu ilikubwa na ukame, nakumbuka waziri mkuu wa wakati huo Edward Lowassa, alikwenda nchini Thailand, kujaribu kufanya mazungumzo na serikali ya Thailand, ili walete wataalamu wao waje kuleta utaalamu wa KUTENGENEZA MVUA ikiwa ni njia mojawapo ya kukabiliana na ukame kwa...
Leo nchi yetu tumepata mkopo wa 1.3 trilioni kutoka IMF (International Monetary Fund) tumefurahia sana watanzania na kupongeza sana kwa hatua hii
Lakini ukifuatilia sana mikopo hii, ambayo mabeberu wanasema eti ni mikopo ya masharti nafuu (concession loan) kutoka kwenye hizo taasisi za...
Moja ya changamoto kubwa sana tuliyonayo hapa barani Afrika, ni nchi nyingi za Afrika kuwa na mifumo ya utawala inayotoa MAMLAKA MAKUBWA SANA KWA MTU/ TAASISI MOJA.
MAMLAKA MAKUBWA SANA ambayo yanaweza kuamua hatma ya maisha yako na
familia yako kwa ujumla.
Watu wengi kwa kutambua hilo...
Mwaka 2004, kulizuka mjadala mkubwa sana miongoni mwa wananchi, baada ya Serikali ya awamu ya tatu, chini ya hayati Rais Benjamin William Mkapa, kufanya maamuzi ya kununua ndege maalumu kwa ajili ya matumizi ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, kwa safari za ndani na nje ya nchi...
Nakumbuka awamu ya tatu wakati serikali ikitaka kununua ndege ya Rais aina ya Gulfstream G550 kwa thamani ya bilioni 46
Watanzania walio wengi, walionyesha kupinga hatua hiyo, kwa kuzingatia hali ya uchumi ya nchi yetu kwa wakati huo
Lakini, aliyekuwa waziri wa fedha wa wakati huo, mzee...
Binafsi nimepata fursa ya kutazama clip moja ikimuonyesha mheshimiwa mkuu wa mkoa wa Dodoma akiongea nawananchi kuhusu suala la kambi za masomo ya ziada kwa wanafunzi wakati wa likizo.
Kama mwananchi nimesiitishwa na baadhi ya maneno yaliyotumika pale.
Hoja yangu hapa sio SAHIHI au KUTOKUWA...
Ukisoma katiba yetu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka1977, kwenye ibara ya 33( 2)
Inamtaja Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kama
1. Mkuu wa nchi( Head of state)
2. Mkuu wa serikali ( Head of the government)
3. Amiri jeshi mkuu ( Commander in chief)
Hivyo basi, Rais...
Ni mabadiliko sahihi yanayoenda kuboresha utendaji wa kazi ndani ya mikoa yao na serikalini kwa ujumla
Mheshimiwa mkuu wa Mkoa Albert Chalamila, mara kadhaa amekuwa ni mtu wa kutoa kauli tata sana kwa lugha nyepesi ni mropokaji, kwa nafasi yake kama mkuu wa mkoa sio busara sana kuwa mropokaji...
Kumbukumbu zangu zinaonyesha, mara kadhaa manaibu waziri wa wizara ya kilimo wanapata bahati ya kuteuliwa kuwa wakuu wa mikoa
Nakumbuka mzee Stephen Masato Wassira, alikuwa naibu waziri wizara ya kilimo, baadaye hayati Mwalimu Nyerere akamteua kuwa mkuu wa mkoa wa Mara
Mzee Njelu...
Nimejaribu kuangalia sheria na kanuni kadhaa kuhusu hili swala la KUSTAAFU kwa wakuu wa mikoa.
Nimesoma sheria ya utumishi wa umma ya mwaka 2002 (The Public Service Act,2002) pamoja na mabadiliko yake.
Pia nimesoma kanuni za utumishi wa umma za mwaka 2003 (The Public Service Regulations...
Acha uongo wewe
Mheshimiwa balozi Joseph Sokoine, aliteuliwa na hayati Rais Dr John Pombe Joseph Magufuli kuwa naibu katibu mkuu wa ofisi ya makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, kutoka kuwa balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji
Kwa taarifa yako, katibu mkuu( Permanent...
Acha kupotosha wewe, mheshimiwa Balozi Joseph Sokoine, aliteuliwa na Rais hayati Dr John Pombe Joseph Magufuli kuwa naibu katibu mkuu ofisi ya makamu wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania kutoka kuwa balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji, hapo alifanya kazi na mheshimiwa Rais Samia...
Hii hoja kuwa wametambulishwa kwa kufuata nani alitangulia kuwasili nchini Uganda nayo SIO KWELI
Kwa sababu mkuu wa nchi wa kwanza kuanza kuwasili nchini Uganda alikuwa ni Rais Mohammed Abdulahi Mohammed wa Somalia na kufuatiwa na Rais Evariste Ndayishimiye wa Burundi ambao wao...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.