Wanajukwaa! Salaam;
Kuna ndugu yangu yuko Dar anatafuta dakari wa familia. Akiwa wa hospitali za rufaa itakua bora zaidi ili aweze kusaidia habari za vipimo nk. Hana tatizo la kiafya kwa sasa ila anataka daktari wa karibu kwa ajili ya kupima afya mara kwa mara na kumshauri kwa ajili ya afya...
Web haina maelezo ya kujitosheleza kabisaa!! Naomba kujua hiyo 5,000USD is for what? Ina include vipimo na mambo mengine au? Please hebu dadavua!! Kama vipi ni PM
Wee Bandabichi! Sio kila kitu kinaulizzwaga hapa!! Tafuta mtu mwenye Blackberry atakusaidida kirahisi sana. Hata hivyo kuchat itabidi uwe umelipia kutegemea na mtandao unaotumia...
Ni kweli kwa baadhi ya watu! Binafsi nawashangaa wanaotumia muda mwingi ku design picha na maneno mengi yasiyo na tija. Ni vizuri tuutumie mtandao kufanya ya maana kama kupata na kutoa information zenye msaada wa watu... Big up Mheshimiwa!
Nimekatishwa tamaa sana! Kama hali ni hiyo kwa MM sijui kwangu itakuwa je... Hata hivyo ngoja tusubiri revolution ulosema pengine itaturudisha kwenye mstari..
Pamoja na kumlaumu Ndugai, kuna haja y akuyajadili aliyoyasema pia. Jamani hii nchi imefikia mahali ambapo kila mtu anakufa na chake. Ndugai anayoyasema ni kweli wala hayana ubishi. Juzi tu kuna Assistance mmoja alihudhuria kikao kwa niaba ya bosi wake wizarani, alirudi baada ya masaa mawili na...
Ahsante Ndebile! Nashukuru kwa ushauri ila kwenda chuo kwa sasa sio rahisi kiasi hicho. Mbali na gharama nahesabu zaidi muda. Hebu nione waliosoma hapo Tengeru kama wapo humu wanisaidie basi hiyo elimu.
Naendelea kutanguliza shukrani...
Wadau! Nimeamua kwenda kulima... nimekata shauri kuwa mkulima lakini wa kisasa. Tafadhali naomba msaada wa yeyote mwenye vitabu vya ELIMU YA KILIMO anisaidie. Ikiwa kwenye soft copy itakuwa vizuri, vinginevyo bado nitashukuru. Vikiwa kwenye lugha ya kiswahili (kama vipo) itakuwa vizuri...
Du! Kweli mwaka huu tutasikia na kuona mengi! Hawa ndio watunga sheria wetu kwetu jamani? Sio ajabu nchi kulaaniwa, kumbe wawakilishi wetu wanafanya mzaha katika wakati ambao tunawategemea sana.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.