Search results

  1. Mindi

    "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza

    Ni kweli mkuu, pengine nimeandika Kwa namna ambayo naweza kueleweka visivyo. Ila ukisikiliza hiyo clip utaelewa ninachozungumzia
  2. Mindi

    Serikali yayafungulia magazeti ya MwanaHALISI, Tanzania Daima na Mseto

    Clown! Title mujarab kabisa kwa Palamagamba. A professorial Clown! Quite an achievement!
  3. Mindi

    Serikali yayafungulia magazeti ya MwanaHALISI, Tanzania Daima na Mseto

    Yaani mkuu haya magazeti yatahoji uchafuzi mkuu 2020, na hizo chaguzi zijazo. Tunajua CCM wamezoea vya kunyonga, na baada ya Utawala wa Magufuli, ndio kabisaaa hawajui kuchinja. Haya Magazeti yatawaumbua, na sitoshangaa yakifungiwa tena
  4. Mindi

    Ummy Mwalimu: Kuanzia sasa matibabu ya Joseph Haule(Prof. Jay) yatagharamiwa na Serikali

    Inashangaza sana kwamba kuna mamia ya wananchi wanashindwa kuchukua maiti za wapendwa wao kisa wanadaiwa gharama za matibabu. Kuna wengi ambao wanafariki kwa kukosa fedha ya kugharimia operesheni na tiba kwa ujumla. Upo sahihi mkuu. Serikali ilitakiwa kuchangia tu. Hii inanikumbusha saluti...
  5. Mindi

    Serikali yayafungulia magazeti ya MwanaHALISI, Tanzania Daima na Mseto

    Habari njema sana, nitaanza tena kununua magazeti. Itakuwa burudani kubwa kuwasoma tena akina KONDO TUTINDAGA, NARONYO KICHEERE, SAED KUBENEA, na wengineo. Hawa jamaa huwa hawaogopi kabisaaa kufukua kinyesi, mizoga na yooote yaliyoooza na kuvunda ila yamefichwa!!
  6. Mindi

    Kwanini CCM wanatuita SACCOS?

    Sikubaliani na mwelekeo wako wa kukiri kwamba ccm wana hoja pale wanapodai CHADEMA ni saccos ya Mbowe. Kinachotokea ndani ya CHADEMA sasa ni kama ilivyokuwa kwa ccm na Nyerere enzi hizo. Unapokuwa na mmoja anayejitolea sana kwa chama, kukitumikia kwa nguvu zote, kutojitafutia mafanikio au faida...
  7. Mindi

    Zitto Kabwe Jitafakari

    Nilimsikiliza Zitto Kabwe, mmoja wa vigogo katika viongozi wa vyama vya siasa vya upinzani hapa Tanzania, akitoa hotuba yake katika mkutano wa Baraza la Vyama vya siasa. Nilimsikia akimuomba Rais Samia, kwa unyenyekevu mkubwa, "asaidie" ili Mbowe awe huru. Nilisikiliza pia majibu ya rais...
  8. Mindi

    PhD ya Musukuma yazua gumzo, Chuo kilichomtunuku hakitambuliki

    Umewahi kumsikia Profesa J katunukiwa PhD? Au uprofesa? Yeye kaamua tu kujiita kutokana na usanii wake. Hakuwahi kuvaa magwanda ya graduu ya chuo kikuu kama huyo msukuma. PhD ya Msukuma ni kituko cha pekee, acha kulazimisha wa "kufanana na" Msukuma
  9. Mindi

    PhD ya Musukuma yazua gumzo, Chuo kilichomtunuku hakitambuliki

    Haya, kuna ile PhD ya Magufuli nayo ilizua mjadala, ambao ulizimwa baada ya mpingaji mkuu wa PhD hiyo kupotezwa jadi leo. Ben Saanane. Ya Jaffo sijaifuatilia binafsi, lakini tunaweza kuorodhesha hapa PhD zenye utata: 1) Dr. Magufuli 2) Dr. Msukuma Kasheku 3) Dr. Jaffo Hivi ile ya Lyatonga Mrema...
  10. Mindi

    Chongolo anachanja mbuga kuimarisha chama lakini Mnyika yuko ofisini anatunza mafaili, hakika CHADEMA mnafeli sana

    Zipo sababu za msingi sana kuendelea na mapambano, hata katika mazingira magumu kiasi gani. Mosi ni kwamba hao wakandamizaji wanabadilika, ipo tofauti kubwa kati ya Mkapa na Magufuli, na Kikwete. Pia kuna haja ya kuwaanika madhaifu yao. Halafu binadamu tuna tofautiana. Mimi mfano, toka utotoni...
  11. Mindi

    CAG Assad alisema ni mtu mjinga pekee ndo anaweza kufanya manunuzi cash: Anajifunza nini Entebbe Airport?

    Yaani wewe unaandika kuhusu mada ambayo huna hata ule uelewa wa mwanzo tu. Miradi mikubwa kama ya marekebisho makubwa ya uwanja wa ndege huendana na mikopo. Magufuli kakopa sana tu kwenye miradi mingi. Kosa lakevni kukopa sana mabenki ya biashara, kama ilivyo kwenye hii ishu ya ya Entebe, badala...
  12. Mindi

    Chongolo anachanja mbuga kuimarisha chama lakini Mnyika yuko ofisini anatunza mafaili, hakika CHADEMA mnafeli sana

    Naam, nia ya dhati wanayo, anayeharibu siasa za Tanzania ni maiti ya ccm. Ndio maana ccm huwa hawajibu ngumi za kisiasa za CHADEMA, sababu ccm ni maiti. Polisi na dola ndio wasemaji wao
  13. Mindi

    Chongolo anachanja mbuga kuimarisha chama lakini Mnyika yuko ofisini anatunza mafaili, hakika CHADEMA mnafeli sana

    Kilikuwa kikao cha ndani, lakini wanachama 15 wa CHADEMA waliswekwa ndani. Wakati ccm wanafanya mikutano ya hadhara nchi nzima bila tatizo. Lakini hapo sasa ndio ushangae, chama mmekizuia kufanya mikutano lakini mnakiogopa kama nini sijui. Inaeleweka kwamba Kikwete ete CHADEMA wamekatazwa...
  14. Mindi

    Kama maji yameongezeka mto Ruvu ndani ya saa 48, basi hata Kidatu, Kihansi na Pangani yataongezeka kama wanaohujumu wakidhibitiwa

    Hiyo nayo propaganda tu. Miaka 3 mfululizo mvua zilikuwa nyingi mafuriko kila siku. Sasa kuna ukame maji ya kidatu lazima yapungue. Enzi za Magufuli alilazimisha wenye viwanda wazime mitambo ili kuepusha mgao wa umeme.
  15. Mindi

    Kuna sababu gani Tundu Lissu kukaa kimya kabisa kwenye kesi ya Ugaidi ya Mbowe?

    Hii ndiyo ile hadithi ya fisi anamfuatilia binadamu, akiamini ile mikono inayokwenda mbele na nyuma, itadondoka apate mlo! Yaani kumbe mnamgwaya sana Lissu eeh? Sasa hamuambulii kitu. Hamjatosheka tu na akina Lijualikali, Mtatiro na kina Silinde? Lisu ni habari ingine kabisaaaa. Sahauni!
  16. Mindi

    Kuna sababu gani Tundu Lissu kukaa kimya kabisa kwenye kesi ya Ugaidi ya Mbowe?

    Ni kweli mwanzo alikuwa anachambua kesi mfululizo kwenye Maria Space, akaja kusimama kuongea. Lakini baadae kukawa na cyber lounge maalum kwa kuchambua kesi hiyo, akapambana kisheria na kaka yake Alute aliyekuwa anapinga kuzungumzia kesi iliyo mahakamani. Lissu alikwisha kuongelea maana ya kesi...
  17. Mindi

    Mfahamu Jenerali Ulimwengu, a True Pan-African Legend

    Kama hayo ndio ujuayo, basi sina zaidi.
  18. Mindi

    Mfahamu Jenerali Ulimwengu, a True Pan-African Legend

    Eti technical issue! Kwa hiyo kama asingemkosoa Mkapa hiyo technical issue isingekuwepo? Semeni ukweli, tabia hii mbaya ya kuvua mtu uraia kisa anakosoa serikali, ni mambo ya AIBU. Hivi unajua kwa vipi Nyerere hakuwahi kufanya ujinga huu? Anaamini katika Pan-Africanism kiukweli. Hii habari ya...
  19. Mindi

    Mfahamu Jenerali Ulimwengu, a True Pan-African Legend

    Jenerali ni Jabali, moja ya watanzania wazalendo wa kweli wa nchi hii, wachache sana. Anastahili kupewa tuzo ya kitaifa. Anasimamia ukweli, haki, Uhuru wa maoni na Demokrasia. Hongera Sana Jenerali Twaha Ulimwengu
  20. Mindi

    Mfahamu Jenerali Ulimwengu, a True Pan-African Legend

    Tatizo wala siyo shule ndogo. Tatizo tumbo limepewa kipaumbele, unafiki na mediocrity. Yaani watu hata hatujui PANAFRICANISM ni kitu gani. Eti fulani siyo raia! Sisi wote ni waafrika
Back
Top Bottom