Search results

 1. M

  Wanaowania urais Z’bar waonywa kuacha kuchafuana

  Wanachama wa CCM Zanzibar ambao wameanza mbio za kuwania urais mwaka 2020 kwa kuunda makundi wameonywa kuacha malumbano na kuchafuana ili kulinda mshikamano uliopo ndani ya chama hicho. Onyo hilo limetolewa mjini hapa na mmoja wa wazee wa CCM, Kombo Mzee, ambaye amesema hali ya mshikamano...
 2. M

  Wengart katika kashfa ya bangi

  Thread hii iliwekwa humu masaa machache yaliyopita lakini ikaondolewa bila maelezo yoyote. Kwa nini tunataka kutetea uhalifu? Picha hizi hapa chini zinaonyesha gari la Wengart Windrose Safaris likiwa limekamatwa huko Arusha baada ya kukutwa na shehena ya bangi. Hii ndio biashara ambayo...
 3. M

  Kampuni ya Wengert katika kashfa ya bangi

  Wengert katika kashfa ya bangi: Kampuni hii ya Kimarekani ambayo imekuwa ikikiuka order za serikali na kung'ang'ania vitalu vya uwindaji sasa inazua maswali mengi. Mwaka uliopita gari moja ya kampuni ya Wengert Windrose Safaris ilikamatwa huko Arusha ikiwa na shehena ya bangi. Mtuhumiwa hadi...
 4. M

  Ahsante NEMC

  Mapema wiki hii nilimsikia Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Eng. Bonaventure Baya, akisema kusababisha kelele kwenye maeneo ya makazi ya watu ni kosa kisheria. Hakika nilikuwa siujui ukweli huu. Binafsi nakerwa sana na kelele kama muziki wa sauti ya juu (siku hizi bodaboda ni kero kubwa zaidi), kwenye...
 5. M

  Bilionea Mohamed Dewji 'MO' kuikwaa tuzo nyingine

  Bilionea Mtanzania Mohamed Dewji huenda akaikwaa tuzo ya 2015 person of the Year ya FORBES iwapo kura zitatosha. yeye ni miongoni mwa nominees watano waliofikia fainali. Ukitaka kumpigia kura ingia: Forbes Africa Person of the Year 2015Forbes Africa Person of the Year 2015
 6. M

  Huyu straika wa Simba kutoka Senegal ni hatari!

  Baada ya kupata taarifa kwamba Simba wanamleta straika kutoka Senegal aitwaye PAPA NIANG (mdogo wake Mamadou Niang), nilimwangalia kwenye Youtube na kugundua kwamba ni mkali. Jamaa anapiga mashuti makali kwa kutumia miguu yote miwili, na pia ni msumbufu kwa mabeki kama alivyokuwa Emmanuel Okwi...
 7. M

  Sitasoma tena gazeti la Mawio

  Leo nilinunua gazeti la Mawio ili kupata uchambuzi kuhusiana na CHADEMA kumpokea mkuu wa mafisadi na kumfanya mgombea wa urais kwa tiketi ya UKAWA. Lakini badala yake nimekutana na habari nyingi zinazoonesha kusifia na kutetea uamuzi wa fisadi huyo kuingia CHADEMA. Nilikuwa naliamini gazeti...
 8. M

  Kwa Jaji Ramadhani CCM inaweza kupoteza uchaguzi

  Iwapo CCM itamsimamisha Mzanzibari Augustino Ramadhani kuwa mgombea wake urais katika uchaguzi ujao itang'oka madarakani. Jaji Ramadhani ana mapungufu mengi kuliko inavyoelezwa. Aliwahi kusimamia muhimili wa Mahakama kwa muda mrefu na katika kipindi hicho ndipo mahakama ilikuwa kinara wa rushwa...
 9. M

  Idadi ya wadhamini wa Lowassa Arusha yazidi ya wapiga kura

  Inashangaza kuona idadi inayoripotiwa ya wanachama wa CCM wanaojitokeza kumdhamini Lowassa katika mikoa mbali mbali inazidi hata idadi ya wanachama wa CCM na wa vyama vingine katika mikoa hiyo. Kwa mfano leo tumeambiwa kwamba amedhaminiwa na wanachama 129,322 huko Arusha. Idadi hii inazidi ile...
 10. M

  Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni

  Hivi toka lini Watanzania tumepoteza haki ya msingi, inayosema mtu hana hatia mpaka pale yule anayemshutumu aweze kudhibitisha kwamba ana hatia mbele ya mahakama? Lakini kwenye suala hili la IPTL, baadhi ya wabunge wetu walisimama bungeni na kuwahukumu watu mbalimbali waliopata misaada kutoka...
 11. M

  Nyumba na kiwanja vinauzwa Dar

  Nyumba yenye vyumba saba na fremu za biashara iliyopo eneo la Buza nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam inauzwa kwa bei nafuu. Pia kuna kiwanja kikubwa ambacho unaweza kujenga nyumba nyingine. Piga simu namba 0654692628 upate maelekezo zaidi.
 12. M

  Eneo linauzwa Gongo la Mboto Dar es salaam

  Eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 8,919 lililopo Gongolamboto Moshi Bar kwa Diwani linauzwa. Ni eneo lenye majengo ya shule na mazao mbalimbali. Wasiliana na Musa namba 0653410175 au 0657741517 au 0713613319. Pia kuna nyumba ya vyumba saba pamoja na strong room na fremu ya duka...
 13. M

  Katibu Mkuu EAC ampiga vita Spika EALA

  Kuna taarifa kwamba Katibu Mkuu wa EAC Dk Richard Sezibira ndiye anayeongoza na kuchochea vita ya wabunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kutaka kumng'oa Spika Margaret Zziwa. Imeelezwa kuwa Dk Sesibera ndiye aliye nyuma ya pazia kuratibu zoezi la kumn'goa Spika Zziwa (kutoka Uganda) na...
 14. M

  Eti First Lady amejifungua hivi karibuni?

  Kuna mtu aliye karibu na first family kaniambia kuwa Bi Mkubwa - First Lady amejifungua hivi karibuni, lakini suala zima linafanywa siri sana. Mimi nimeshangaa kwani sijawahi kumuona akiwa mja mzito. Au yale mavitenge aliyokuwa anajitanda atokeapo hadharani yalikuwa yanaficha tumbo? Mbona katika...
 15. M

  Taifa stars ya miaka 50 ya uhuru

  Hebu tuchangie mawazo kupata timu ya wachezaji bora wa mpira wa miguu waliowahi kuchezea Taifa Stars katika kipindi cha miaka 50 iliyopita. Wale waliowashuhudia wachezaji wa miaka ya mwanzoni mwa 60 watatusaidia iwapo wanawakumbuka ma-star wa enzi hizo waliokuwa na kipaji adimu cha kutandaza...
 16. M

  Tufanye nini kuiokoa nchi yetu?

  Wakuu, nimekuwa nikijiuliza mara nyingi nini kifanyike kubadili mwelekeo wa nchi yetu. Tunashuhudia nchi ikiangamia kwa kukosa huduma muhimu kama umeme na maji, huku maisha yakizidi kuwa magumu zaidi. Watawala tuliowapa dhamana ya kutuongoza hawaonyeshi kuwa serious ku-address matatizo yetu...
 17. M

  JERRY SANTO kuhusu soka ya Bongo

  Jerry Santo: In Tanzania players are kingsBy Patrick Korir Former Tusker skipper Jerry Santo is amazed at football in Tanzania. Across the border, players are held in much higher regard compared to players in Kenya, says Jerry. Playing in Dar for Simba SC for a second season since crossing...
 18. M

  Hii ndio shughuli ya TANESCO!

  Jana nikiwa napita maeneo ya Ubungo na family yangu, mwanangu mwenye umri wa miaka 6 aliliona jengo la TANESCO na maandishi makubwa "TANESCO" akaniuliza: "Baba, kumbe pale ndio TANESCO?" Nikamwambia: Ndio, pale ni makao makuu ya TANESCO" Akaendelea: "Kwa hiyo pale ndio wanapokata umeme?"...
 19. M

  Msiba mkubwa: Adam Lusekelo Mwakang'ata

  Taarifa za kusikitisha zilizonifikia muda mfupi uliopita zinasema mwandishi wa habari maarufu ADAM LUSEKELO amefariki dunia leo alfajiri kwenye Hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam. Taratibu za mazishi zinafanywa nyumbani kwake jirani na lililokuwa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Ubungo...
 20. M

  Hizi ndio nchi zenye machafuko...

  Nilikuwa naangalia nchi zenye machafuko (unrest) na maandamano huko Mashariki ya Kati na Afrika nikakutana na article hii ya CNN ambayo imezitaja nchi na vyanzo vya machafuko hayo. Nimepata faraja baada ya kuona kuwa Tanzania haimo katika orodha hii kwani maandamano yake ni ya amani, na hayana...
Top Bottom