Search results

 1. beth

  Marekani: Mshauri wa zamani wa Rais Trump ahukumiwa miaka mitatu jela

  Roger Stone, aliyekuwa mshauri wa Rais wa Marekani, Donald Trump wakati wa kampeni za uchaguzi ambaye jina lake lilitajwa wakati wa kesi ya Urusi amehukumiwa kifungo cha miaka 3 na miezi 4. Uamuzi kuhisiana na kesi zilizokuwa zikimbali Stone umetolewa katika mahakama jijini Washington...
 2. beth

  Marekani na Taliban kusaini makubaliano ya amani

  Waziri wa nchi za kigeni wa Marekani Mike Pompeo anasema makubaliano ya siku saba ya kusitisha uhasama baina ya Marekani na Taliban yataanza kutekelezwa usiku wa leo ingawa hajasema yataanza muda gani hasa. Hatua hiyo itakuwa mwanzo wa kutiwa saini makubaliano ya amani kati ya taliban na...
 3. beth

  Ruvuma: Wawili wafariki baada ya kusombwa na maji

  Watu wawili wamefariki dunia katika kata ya Matumbi halmashauri ya wilaya ya Madaba mkoani Ruvuma kwa kusombwa na maji ya mto huku baadhi ya barabara na madaraja yakiathirika kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha. Diwani wa kata ya Matumbi Bw.Valentine Mtemauti amesema mito kwenye kata yake...
 4. beth

  Ukraine: Wakazi wa Mji ambao Serikali imepeleka walioondolewa China sababu ya Corona washambulia mabasi kupinga uamuzi huo

  Baada ya Serikali ya Ukraine kutangaza kuwaondoa raia wake waliokuwepo China kufuatia mlipuko wa Corona Virus, Wakazi wa Mji ambao watu wao wanatarajia kukaa kwa muda wa siku 14 wakati wapo kwenye uangalizi maalum wameshambulia mabasi yaliyokuwa yakisafirisha watu hao na kufanya vurugu. Wakazi...
 5. beth

  Lesotho: Polisi yasema Waziri Mkuu wa nchi hiyo atashtakiwa kwa mauaji ya Mkewe wa kwanza

  Waziri Mkuu wa Lesotho Thomas Thabane, 80, atashtakiwa kwa mauaji ya mkewe wa kwanza Lipolelo Thabane, Polisi wameeleza. Bwana Thabane alitangaza kuwa atajiuzulu mwezi Julai kutokana na umri wake, bila kuzungumzia shutuma dhidi yake. Mkewe wa sasa Maesaiah Thabane tayari ameshtakiwa kwa...
 6. beth

  Sudani Kusini: Rais Kiir na Mpinzani wake, Riek Machar wakubali kuunda Serikali ya Muungano

  Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir na Mpinzani wake Riek Machar wamekubaliana kuunda serikali ya muungano kufikia siku ya Jumamosi kama walivyokubaliana. Hatua hiyo inafuatia mkutano uliofanyika katika Ikulu katika mji mkuu wa Juba siku ya Alhamisi. Rais Kiir ameahidi kuwalinda viongozi wa...
 7. beth

  Lesotho: Waziri Mkuu Thomas Thabane atakiwa kujiuzulu, Chama tawala chasema. Thabane atashitakiwa kwa mauaji ya mkewe

  Chama tawala nchini Lesotho kimemtaka waziri mkuu kujiuzulu leo Februari 20, 2020, ikiwa ni siku 2 tu tangu mkewe wa sasa aliposhtakiwa kwa mauaji ya mkewe wa awali. Mke wa sasa wa Waziri Mkuu Thomas Thabane, Maesaiah Thabane (42) alifikishwa mahakamani Februari 18 mwaka huu na kushtakiwa...
 8. beth

  Mwanasayansi aliyegundua mfumo wa 'Cut-Copy-Paste' afariki dunia

  Mtaalamu wa Sayansi aliyegundua mfumo maarufu wa 'Cut-Copy-Paste' ambao unatumiwa na maelfu ya watu duniani kote amefariki dunia. Lawrence "Larry" Tesler alikuwa na miaka 74. Chanzo cha kifo chake bado hakijawekwa wazi. Tesler amewahi kufanya kazi katika makampuni mbalimbali yakiwemo Apple...
 9. beth

  Mke wa Rais Museveni atakiwa kufika mbele ya Bunge

  Spika wa Bunge la Uganda ametoa wito kwa Mke wa Rais wa Uganda ambaye pia ni Waziri wa Elimu, Janet Museveni kufika mbele ya chombo hicho cha kutunga sheria kufuatia mkanganyiko kuhusu kuanza kutumika kwa mtaala mpya wa elimu. Waziri huyo alishindwa kufika mbele ya Bunge Jumanne Februari 18...
 10. beth

  Vifusi vya uchafu vyapatikana kwenye tenki za mafuta za ndege ya Boeing 737 Max

  Shirika la Boeing linakumbwa na hatari ya kukabiliwa tena na suala la usalama wa ndege zake baada ya vifusi kupatikana kwenye tenki za mafuta katika ndege kadhaa ambazo zilikuwa zinasubiri kuwasilishwa kwa wanunuzi. Msimamizi wa ndege aina ya Boeing 737, amewaambia wafanyakazi wake kwamba...
 11. beth

  Umoja wa Mataifa: Ulimwengu umeshindwa kulinda Watoto

  Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa siku ya Jumatano, inasema ulimwengu umeshindwa kumlinda mtoto na hatari za kiafya zinazotokana na athari za mabadiliko ya tabia nchi na lishe hafifu. Ripoti hiyo iliyopewa kichwa cha habari 'Hatma ya watoto ulimwenguni'imetolewa na timu ya wataalamu zaidi...
 12. beth

  Rwanda: Human Rights Watch yataka kifo cha Kizito Mihigo kuchunguzwa

  Shirika la kutetea Haki za Binadamu, Human Rights Watch linataka uchunguzi ufanywe kubaini chanzo cha kifo cha mwanamuziki maarufu wa nyimbo za injili nchini Rwanda, Kizito Mihigo. Mkurugenzi wa shirika hilo katika kanda ya Afrika ya kati Lewis Mudge, ameiambia BBC kuwa shirika hilo linatilia...
 13. beth

  Rais Magufuli afanya uteuzi wa viongozi watatu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika (TCDC)

  Rais John Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi watatu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika, uteuzi ambao ulianza rasmi Januari 30 mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo walioteuliwa ni Dkt. Benson Otieno Ndiege ambaye amekuwa Mrajis wa Vyama vya Ushirika...
 14. beth

  Niger: Watu 20 wafariki dunia baada ya kukanyagana wakati wakipokea msaada

  Watu 20 wanmepoteza maisha baada ya kukanyagana wakati wakipokea msaada wa Chakula na Fedha katika Mji wa Diffa huko Niger. Waliofariki ni Wanawake 15 na Watoto 5. Inadaiwa kuwa maelfu ya watu walijitokeza kupokea msaada huo uliokuwa unatolewa na Gavana Babagana Umara Zulum katika Kituo kimoja...
 15. beth

  Cameroon: Watu 22 wapoteza maisha katika shambulio la kijiji

  Watu takribani 22 wameuawa katika shambulio la kijiji kimoja kaskazini-magharibi mwa Cameroon, Umoja wa Mataifa (UN) umesema. Zaidi ya nusu ya waliouawa katika kijiji cha Ntumbo walikuwa ni watoto. Vyombo vya habari vya nchini humo vinadai kuwa baadhi walichomwa moto mpaka kufikwa na umauti...
 16. beth

  Rwanda: Msanii maarufu wa nyimbo za injili Kizito Mihigo akutwa amejinyonga ndani ya Kituo cha Polisi

  Polisi ya Rwanda imetangaza kwamba msanii maarufu wa nyimbo za injili, Kizito Mihigo amekutwa amejinyonga kwenye Kituo cha Polisi. Kwa mujibu wa tangazo la Polisi, maiti ya msanii huyo imepatikana katika chumba alichokuwa anazuiliwa kwenye Kituo cha Polisi mtaa wa Remera, mjini Kigali. Polisi...
 17. beth

  Uingereza: Tahadhari za mafuriko zatolewa kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha

  Mvua kubwa na upepo mkali vimeikumba Uingereza na baadhi ya maeneo ya Ufaransa na kusababisha baadhi ya mashirika ya ndege kukatisha safari zake. Huko Wales wakaazi walilazimika kuondoka kwenye makazi yao baada ya mvua kubwa kunyesha ndani ya kipindi cha masaa 48. Uingereza imesambaza...
 18. beth

  Mbeya: Mtoto wa miaka 17 auawa baada ya kujaribu kupora fedha

  Mtoto Victor Mwasoro (17), ameuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kuvamia kibanda cha kutuma na kupokea fedha akiwa na bastola ya baba yake kwa lengo la kupora fedha. Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki katika eneo la Sae jijini Mbeya na kwamba mtoto huyo alifariki kutokana na kipigo...
 19. beth

  Libya: Waziri Mkuu aonya kutokea kwa mgogoro baada ya miundombinu ya mafuta kufungwa

  Waziri mkuu wa Libya Fayez al-Serraj anayeongoza serikali inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa amesema kufungwa kwa miundombinu ya mafuta nchini humo kutasababisha mgogoro mkubwa wa kifedha. Akizungumza na waandishi habari mjini Tripoli, Al-Serraj amesema hasara iliyokwishapatikana kutokana...
 20. beth

  Mali: Wanamgambo wavamia kijiji na kuua watu 31

  Watu wapatao 31 wameuawa hapo jana katika shambulio dhidi ya kijiji cha Ogossagou nchini Mali. Maafisa wa serikali ya Mali wametangaza habari hiyo baada ya watu wenye silaha kuvamia kijiji hicho katikati ya nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika. Maafisa wa eneo hilo wamesema kuwa, watu wenye...
Top