Mambo ya kuvamiwa yanahusiana vipi na mikataba? Au ndio yale yale ya kuandika chochote ili uonekane umechangia. Nani anavamia nchi ya Tanzania?
Hata hivyo sikushangai sana maana muda mfupi uliopita ulianza kumlaumu Raisi mstaafu kuwa aliruhusu watu kula vyura na kitimoto kwenye hii thread...
Angalau sasa hivi hauongelei mambo ya Mwinyi kuruhusu watanzania kula vyura na kitimoto, baba una mambo wewe yaani sikuwezi kabisa.
Na hao wanaotaka kuvamia nchi na kuzima umeme ili kuleta giza ni kina nani?
Ungeweka ushahidi usingekuwa na sababu ya kuandika kitabu kizima. Watu hapa wakiona ushahidi huwa wanakubali. Sasa wewe unaeleza mengi lakini ushahidi hakuna na ndio maana bado watu wanakuuliza ushahidi wa madai yako hapa.
mimi bado naamini ukileta uthibitisho watu watakuelewa zaidi kuliko story zote hizi mwenzangu. Leta kadi namba au vinginevyo ili kuthibitisha usemi wako.
hawa hawawezi kuchukua nchi.... sisi ccm hatuna cha kutimuana wala nini.
Kwanza hata Lowasa kuna habari kuwa alionewa na inabidi arudishwe kwenye U-PM tu.
kidumu chama cha mapinduzi.
Mbona wanajeshi wanamlinda Kikwete na serikali yake kila siku bila tatizo kabisa. Na sasa vijana walipokusikia unataka kwenda msituni wameongeza siku za mazoezi ili wakuchafue huko msituni hadi ukimbie.
kwi kwi kwi
Naona sasa wewe unataka Dr Slaa na Zitto wakamatwe kama alivyosema Marmo. Kweli kabisa, Dr Slaa na Zitto watueleze waliipata vipi hiyo mikataba na hizo siri za serikali.
Mama, miye sina mpango wa kwenda bungeni. Ningekuwa na huo mpango ningesema. Kukiwa na kitu cha kufanyika, mimi namwambia Mwenyekiti wangu Kikwete na yeye anashughulikia mara moja.
Kwa mfano, ile issue ya uwanja wa fisi inashughulikiwa hata hivi sasa tunavyojadili hapa. Asante
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.