unamtindio wa ubongo wewe ! ki vipi chadema inahusika, sana sana kama si chadema basi asingegundulika kuwa anatumia mavazi ya kijeshi kinyume cha sheria, hakutumwa na chadema kuvunja sheria, na kama alivunja sheria akahukumiwa na mahakama na mwenyewe kukiri kosa lake, basi hiyo ndiyo stahili...
Mwalimu alikuwa yeye, na hakujifanyisha, kujiigiza wala kujifananisha, alichokuwa anakisema ndicho alichokuwa ana kiishi, yeye alikuwa ndiye yeye yule na si mwingine kwa mema, mazuri na mapungufu, kama mungu alivyo mjalia ndiyo maana anaheshimika, na ataendelea kuheshimika kwa wote wanao penda...
Namshangaa Mh Chambo kumteua Bw Jaso Rugairuza kuwa Mwenyekiti wa kamati,anamfahamu vizuri huyo Mhe Rugairuza ??kweli,Hvi Tanzania inakwenda wapi?
Huyu jamaa aliyeteuliwa hafai kwani ni yeye ndiye aliyesababisha mrundikano wa wa mizigo pale Bandarini alpokuwa Port Manager kabla ya Cassian...
nimejitambua, leo kweli baada ya kuangalia picha hizi, nimejifunza mengi mno. hongera nyingi kwa walio post picha zao humu na nimesikitika sikupita mapema kuangalia huku. I will come back one day with a big suprise BIG UP and thanks to all that contributed to this thread !!!
William, Hongera sana kwa kuthubutu, nilitamani sana nikuone ukijieleza pale bungeni jana , na bahati nzuri nikabahatika kukushuhudia ukijieleza, sikufahamu, lakini nilifarijika kwa maelezo yako na nilitamani wakupitishe, bali nafasi zilikuwa chache. Unaweza, jiamini na uthubutu tena mwanzo mzuri !
Katika nafsi yangu nimeamua kubadilisha mwelekeo wa historia ya nchi yangu, nakili maandiko haya , watu watakuja yakumbuka, 2012 ni mwaka wa mwisho wa uhujumu na unyanyasaji ! ni mwaka wa mwanzo wa mwiasho wa propaganda za amani kuwa kisingizio cha kuwaibia wananchi, na mimi nitathibitisha hilo...
Tanganyika , Tanganyika yangu nakupenda sana , ila kwa hali hii inavyo endelea , harufu kali ya damu inanukia, mzaha mzaha huzaa usaha ! wengi wetu tulikuwa mabingwa wa kuimiliki kalashnikov , na kwenye Range tulifika mpaka kwenye Tano bora ya kikosi, sasa naona wakati unasogea watu kukumbushwa...
Alikuwa mtanzania aliyependwa na watanzania wengi, ona hata Ole Sendeka naye yupo !! na wengine wengi tu mpaka huko Ifakara, huu kweli ni upendo kwake bila kujali kitu chochote zaidi ya UTU. kwaheriri dada Regia
Regia ! ama kweli katoa fundisho kwa watanzania wote, kuwa chama si hoja, hoja ni usafi wa moyo wako na uzalendo kwa watanzania wenzako, mapenzi mema kwa nia njema yakitendwa matokeo yake ni upendo ulio onyeshwa kwake na watanzania wote, bila kujali itikadi zao ziwe zozote zile !! mungu ailaze...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.