Waungwana hatutusi:
Waungwana hatutisi, sikia Jitu Bandia
Twaongea kwa wepesi, na pia twaitikia
Na maneno ni vipisi, kichwani humalizia
Sikia Jitu Bandia, waungwana hatutussi!
Haja yake ni kisima, kwa kina kaelezea
Matusi hajayasema, wakati aelezea
Usongo wake kisima, malenga kaongelea...
Ugonjwa wake Vipini!!
Ninaazia salamu, kujibu bin fulani
Kaelezea ugumu, avionapo vipini
anaipata na hamu, na kuihisi mwilini
Ugonjwa wake vipini, kwa wanakwake puani!
Kwa ari kaelezea, kwake huo mtihani
Ashindwa kujizuwia, avionapo puani
Ashiki yampandia, avurugikwa kichawni!
Ugonjwa wake...
Kitu ambacho Wa Tz hatujakielewa ni kuwa tangu upinzani uanzishwe Tanzania na chama tawala (CCM), Tanzania hatujawahi kuwa na upinzani!
Vyama vingi vimeanzishwa lakini viongozi wao wana njaa na wakichekewa tu na utawala wanalainika!! Katika huu mfumo wa vyama vingi wanaoumia ni raia wa...
Hatari Kubwa!
Nimekumbuka utunzi, akiimba Marijani
Nilikuwa si mjuzi, kuuelewa kichwani
Akimkanya mzinzi, mke wa wake jirani!
Aliimba Marijani, sawa kucheza na moto!
Sawa kucheza na moto, na miye nafikiria
Kukumbuka ya utoto, wakati unavizia?
Utapata mkong'oto, huruma nakuonea
Aliimba...
Pole nasema pokea, kujihisi masikini
Mungu ndiye ajalia, zaidi ya milioni
kichwani nafikiria, hujitazami mwilini
Wajihisi masikini, wekati wewe tajiri?
Utajiri si mapesa, wala magari ya ghali
Utajiri si kutesa, kwa hali pia na mali
Utajiri ni hamasa, afyayo ya kimwili
Wajihisi masikini, wakati...
"Penye nia"
Penye nia kuna njia, welishasema zamani
Msemo nakumbukia, na yake pia thamani
Usjeikata tamaa, utajafika nyumbani
Penye nia pana njia, walishasema wahenga.
Fikisha wako ujumbe, ajuwe yalo moyoni
Pitia hata kwa jumbe, wake hapo mtaani
wajuwe nawe ni jembe, hunao pia utani
Penye...
Impact itakuwepo, kwani baada ya hapo ina maanish Profesa atadai fidia, na pesa zote alizokosa alipotenguliwa kwenye nafasi hiyo. mfano mishara yake na marupurupu yake yote! Hapo mlipaji ni Serikali - kwa kifupi walipaji ni Wa tanzania walipa kodi wote!
Mpendwa,
Ilikuwa Aprili, tarehe naikumbuka
Kukujuza sina hali, kwako weye nimefika
Nikaomba ufadhili, kwa dhati nikatamka
Ilikuwa Aprili, ningali ninakumbuka!
Kwa kina nilikujuza, kwako weye nimefika
Na tena sikujikuza, kwa dhati niliandika
Na lugha nikaiuza, kutaka kueleweka
Ilikuwa...
Safi.
Ni aibu askari mzima kitambi utadhania wana mimba!
Ndiyo maand hata youle Hamza aliweza kuwanyang'anya bunduki na kuwaua kirahisi.
Askari wanatakiwa wawe wakakamavu.
Mpendwa mwana Fulani,
Kumbuka kuna korona;
Nanianzia salamu, binti mwana Fulani
Ingawa nina ugumu, ungali mwangu moyoni
Kwangu weye ni muhimu, hujatoka akilini
Kumbuka kuna korona, utulizane nyumbani
Kipindi hichi kigumu, tulia mwana fulani
Utoke kama muhimu, vinginevyo kaa ndani...
Kongole wetu Malenga;
Kongole wetu malenga, utunzi wako mahiri
Ukweli umeulonga, na fumbo hilo la siri
Wengine wamejigonga, watazama editori
Ngoma sasa inadunda, twahitaji wetu manju
Kongole hii ni yako, ipokee mikononi
Heko nyingi ni za kwako, kwa kubakia fanini
Ninalitoa tamko, fumbo...
Kisa cha kofia bungeni
1
Kisa cha sasa kofia, kimetokea bungeni
Na hoja aliitoa, akilalama bungeni
Kwa kina kaelezea, kadharauliwa juweni
Kisa cha kweli kofia, kimetokea bungeni!
2
Kakasirika jamaa, kajieleza bungeni
Heshima kamvunjia, hajaelewa kwanini?
Ni vipi amemvua, baraghashia...
Hapa tusilaumu mtu, wa kulaumiwa watu wajua kiswahili na pia wataalam wa Kiswahili kwani makosa kama haya hawayakosoi. Wanakaa kimyaa tu.
Pia kuna tatizo kubwa kwa Watanzania kutotaka kujituma na kuomba kazi sehemu kama BBC na kazi nyingi za kimataifa.
Mnajua majirani zetu wanajituma sana na...
Nadhani anafikiria kuwa hatutakumbuka yaliyotokea, au aloyafanya!
Nakumbuka kipindi hicho kils kitu kiliuzwa bei karibu na bure. Je twaweza kuvirudisha? Baada ya hopo ndiyo nilijitoa katika kuchangia siasa humu jamii kwani nilikuwa sielewi watu bado walikuwa wanamtetea ati analeta maendeleo...
Mpende hivyo alivyo
Kupenda kweli upofu, mpende hivyo alivyo
Na tena ni usumbufu, nasema ujuwe hivyo
Mpende bila ya hofu, mpende ndivyo alivyo
Kupenda kama upofu, mpende hivyo alivyo
Ni mke na siyo jike, naomba unielewe
Ala vyako pia vyake, mnapendana wenyewe
Chakula chako ni chake...
Ikulu siyo nyumbani;
Namtafuta tabibu, mwenye kupiga ramli
Awezaye kunitibu, na kunijibu maswali
Anipe pia sababu, zenye uzito kamili
Namtafuta tabibu, anayejua ramli
Mganga au tabibu, na pia mnyenye tunguli
Nijuwe yalo nisibu, nikashindwa mara mbili
Nikaupata ububu, kuvurugikwa akili...
Nawajulisha bungeni, na ninyi wa humu ndani
Kinyag'nyiro nchini, na mimi nimo kwa ndani
Ninazunguka nchini, mijini na vijijini
Na mimi nimo kwa ndani, kinyang'anyiro nchini
Na mimi nimo njiani, Ikulu kuwe nyumbani
Nishaanza kampeni, nawajulisha juweni
Tena sifanyi utani, dhamira ipo moyoni...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.