Nitakujibu kwa kifupi sana. Niliwahi kusoma makala moja ya historia ya kina Speke na Burton wakiwa wakizungumzia utafiti wao wa chanzo cha mto Nile na kufika ziwani (Tanganyika). Walidai kuwa chanzo cha jina hilo kwa lugha yetu ikiwa na maana ya "sail in the Wilderness". Wakati wakizunguka...
Jina la Tanzania halitakiwi kisheria kuwa ndani ya hati isipokuwa nchi zinazoungana. Kwa afeika nzima ni sisi tu tumeweza. Isitoshe jina ni jina tu mnaweza badilisha wakati wowote kwa nchi ile ile hata kama hati ya Uhuru imeandikwa jina jingine.
Wewe unaweza badilisha jina lako kesho...
Hapana sijatukana isispokuwa penye ukweli tuuseme, sisi Wadanganyika. Kikwete alitaka kuuza pwani yote Kwa mkataba wa bandari ya Bagamoyo hakuna Mtanganyika wala Mzanzibar alosema huyu Mtanganyika kauza nchi, tena kibaya zaidi wakamtukana Magufuli alotufumbua macho. Leo kinatokea kitu kama kile...
Mnadanganywa ndio maana mnaitwa WADANGANYIKA. Hakuna Mtanzania anayeishi nje aliukana Utanzania kwa sababu kuna process na balozi zetu hujulishwa pale mtu anapoukana Utaifa wake.
Hutakiwi kusikiliza parapanda za vucuzela ukaamini pasipo kutumia akili yako. Mtu akiukana Utanzania leo hii...
Ulosema yote nakuelewa na nakubali nawe lakini kilichokosekana hapo nini? jina tu la Tanganyika ulopewa na mkoloni ndio unalilia. Sasa ndugu yangu wewe utakula jina? Kuwa na jina Tanganyika utafaidika na kipi au fahari ya macho! maana unapoomba kitu ujue faida na hasara zake.
Jina tu la...
Niwaambieni hivi. Juhudi za Uhuru wa Tanganyika na Zanzibar ulikuwepo toka kabla ya Nyerere wakati AA ikiendesha shughuli zake kote bara na Visiwani. Cecil Matola na Mzee Kreist Sykes wakiongoza makao Makuu Dar kwa sababu Mtawala wa kote alikuwa Muingereza. Sultan alikuwa kama King Charles wa...
Huwezi chagua wazazi - Baba na Mama yako wameshakupa jina lako. Ukitaka jina la Babu huyo ni mzungu mshenzi unayemchukia sana alimtesa bibi yako. Unalitaka jina hilo ili uonekane na wewe mzungu au?
Yamepitwa na wakati mkuu tulikuwa tukienda Zanzibar na Passport, leo hii huendi nayo. Anaweza mtu kusema unatakiwa kubeba Passport na ukaamini. Hofu ya Zanzibar ni Population ambayo hata katika mipango miji tunazingatia. Sasa mbona Bara inawakataa Diaspora wanaoishi nje? Je hao sio Watanganyika...
Mkuu sijachanganya kitu isipokuwa nawamsha Wadangantika mjue kuwa nyie ni kitu kimoja mligawanywa pasipo hiari yenu. African Association ilianzishwa na Waafrika wa Bara na Visiwani na hata kablanya ASP haijaungana mwaka 1957 mwl. Nyerere alienda Zanzibar akitaka vyama vyote vya waafrika...
Kwa hiyo unacholilia ni jina? Ok tunakuita Bara umepungua nini?viiongozi? Maana ukisema Serikali maana yake unataka viongozi ilihali Serikali ya JMT inafanya kazi zile zile.
Wenzenu huko Ulaya mpaka Wahindi wanaongoza nyie mnakalia Utanganyika. Afrika kazi kugombania urithi matokeo mnakosa...
Umeenda Zanzibar au hadith tu za simulizi. Mbona wapo Wabara wengi wanaishi na wamewekeza Zanzibar. Wapo Wangazija, wahindi, Wachina, Wazungu wewe unabakia kulia tu. Hizi Siasa za kutafuta mchawi zinawapotosha sana, nenda kawekeze Zanzibar na utaishi kama Mzanzibar. Nina jamaa zangu wanaishi...
Hakuna kitu MTANGANYIKA wala MZANZIBAR isipokuwa kuna mzawa wa Bara na Zanzibar kama ilivyo mzawa wa NewYork na Chicago wote ni Wamerekani.
Hoja ya kuiua Tanganyika ni hekima kubwa sana kwa sababu Tanganyika ingekuwa na wabunge 600 Wa Bara na Bunge la JMT. Madiwani pia mara 2 na Mawaziri...
Sawa kabisa hata Zanzibar kulikuwa na mchanganyiko kama huo mpaka Wachina walikuwepo. Kuna watu kutoka Comoro (Ngazija) Tabora, Kigoma, Wazaramo na hata wa kanda ya ziwa ambao waliunda African Association.
Muungano haukua wa bahati mbaya isipokuwa tulilazimika kuwa nchi mbili kutokana na mfumo...
Hayo majibu yako sio ya Katiba. Kama unasema Mpemba anayepatikana Bara ni Mzanzibar, basi fahamu pia kuwa Asili ya Kabila la Mama Samia ni kutoka Bara kwa hiyo yeye ni Mtanganyika.
Leta jingine
.
Watanganyika ni Wananchi wanaopatikana upande wa pili wa Muungano! mbona haieleweki. Upande wa kwanza wa Muungano ni upi?
Je, Mmasai anayepatikana Zanzibar huyu sio Mtanganyika! Au Mpemba anayepatikana Dar huyo sio Mzanzibar?
Na kwa tafsiri hiyo, Huyu rais wa Zanzibar Hussein Mwinyi ni...
Kwa hiyo Tanganyika ya miaka mitatu ambayo tayari.kulikuwa na Wazanzibar ndani ya chama na Serikali.
Ujue watu wengi hawafahamu hata harakati za Uhuru kwamba Kuna Wazanzibar walishiriki na wengine Wanachama wa TANU.
Hata historia ya hii CCM nyuma ilianza mwaka 1927 na chama cha African...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.