Search results

 1. MotoYaMbongo

  MSAADA TAFADHALI.

  Jamaa yangu wa karibu namba yake ya simu mke wake kaidukua, kila akifanya mawasiliano na watu mkewe anajua, hadi meseji, afanyeje kukabiliana na hali hii? Mwenye ujuzi tafadhali msaada.
 2. MotoYaMbongo

  Naomba ushauri ninunue simu ipi kati ya hizi?

  Naomba wajuzi mnipe ushauri ninunue sim ipi kati ya Samsung galaxy a10 na Samsung galaxy a20?
 3. MotoYaMbongo

  MSAADA.

  Nina Samsung Galaxy J1. Nikiiweka mfukoni ikakandamizika kidogo tu nakuta imezima. hadi nitoe betri na kurudisha ndio nikiiwasha inawaka. Mwenye ujuzi inaweza kuwa nini anipe elimu. Sent using Jamii Forums mobile app
 4. MotoYaMbongo

  Waziri TAMISEMI tusaidie Tabora, Walimu hawafundishi

  Mh, Waziri, Tabora Walimu hawafundishi, wanavunja vipindi kwa kulazimishwa kwenda kupanda miti, wiki mbili za mwanzo mwezi Januari zimekwenda na maji kazi kupanda miti. Wiki hii tena Mkuu wa Mkoa kaanzisha tena Watumishi wote wapande miti na Walimu hakuna kufundisha ni kupanda miti, tena...
 5. MotoYaMbongo

  Rais anaweza kumfukuza jaji mkuu ?

  Wajuzi nisaidieni elimu, naomba kuuliza, Rais wa nchi ya Tanzania ana mamlaka ya kumfuta kazi Jaji Mkuu aliyemteua?
 6. MotoYaMbongo

  Tecno W3 kujaa cached data.

  Nina sim tecno w3, ninapotumia internet halafu nikiangalia kwenye internal storage nakuta storage inapungua hadi nifanye ku clear cached data. Hakuna namna ya kuzuia hizi cached data? Nimechoka ku clear kila baada ya siku kadhaa. Imekuwa adhabu sasa. Naomba mwenye utaalam toa msaasa tafadhali.
 7. MotoYaMbongo

  Western Wall Israel ina Historia gani?

  Nimeona ziara ya Trump Israel, moja ya sehem alipotembelea ni WESTERN WALL. Kwa mwenye kujua naomba anielimishe, hiyo Western wall ina hadhi gani. Maana nimeona ni ukuta wa zamani ila unapewa heshima kubwa.
 8. MotoYaMbongo

  IDARA YA UTUMISHI URAMBO NI JIPU UCHUNGU, WAZIRI HUSIKA TUMBUA

  Walimu wanateseka, wananyanyasika, Wamepanda madaraja tokea 2014 hadi leo hii naandika uzi huu bado hawajabadilishiwa mshahara, wamefatilia hadi wamechoka, kila siku wanaambiwa wapeleke nyaraka, wanapeleka halafu wanasubiri ikifika mwisho wa mwezi hola! Imefika mahali sasa wengine wanafatilia...
 9. MotoYaMbongo

  Utumishi na TSD Urambo ni Jipu

  Walimu wamepanda madaraja tokea 2014 hadi leo hawajarekebishiwa mshahara, wamefuatilia hadi wamekata tamaa, Pia kuna Walimu wa mda mrefu madaraja yao wanazidiwa na wa Juzijuzi tu na Elimu wako sawa, kuna harufu ya Rushwa idara ya Tsd, tunawasihi Tamisemi wafanye uchunguzi Urambo Serikali...
 10. MotoYaMbongo

  BAVICHA yatikisa kwa Sitta

  Jana umefanyika mkutano mkubwa wa Bavicha Taifa Urambo viwanja vya Tarafani, Mwenyekiti Bavicha Taifa alihutubia sambamba na makamanda kutoka Mbeya, Iringa, Kilimanjaro, Mara. Muitikio wa vijana, Wazee, Kinadada ulikuwa mkubwa sana, pia tukio lililoshtua wengi ni kupewa kadi ya uanachama...
 11. MotoYaMbongo

  Magreth Sitta arejea Urambo haraka

  Baada ya kupata taarifa vijana wa M4C wamepiga kambi Urambo, na kubomoa ngome za Mme wake fisadi Sitta, amerejea ghafla kujaribu kupambana, lakini vijana wa M4C wanapiga kazi usiku na mchana ili kuzoa ushindi Serikali za mitaa.
 12. MotoYaMbongo

  TV mr Uk Vipi ubora wake ?

  Wajuzi nisaidieni, vipi hizi flat tv zimeandikwa mrUK, Zina ubora gani?
 13. MotoYaMbongo

  Naomba ushauri simuelewi mke wangu

  Nimekaa na mke wangu miaka miwili sasa, tuna mtoto 1, kinachoniumiza kichwa, mke wangu yeye nikitaka tendo la ndoa anadai nimuwahi kabla hajapata usingizi, akishasinzia nikamwamsha ili tupeane tunda anachukia sana, na asubuhi hivyo hivyo, leo nimemuuliza kama anamchepuko bora aniambie akasema...
 14. MotoYaMbongo

  Kwa nini israel haitaki wapalestina wajitawale?

  Naomba mwenye ufaham wa hili anielimishe, mi najiuliza sana, kwa nini Wayahudi hawataki Wapalestina wajiundie Taifa lao na wajitawale?
 15. MotoYaMbongo

  Hakuna kupanda madaraja mwaka huu.

  Nimezipata hizi taarifa kwa watu wawili kuwa Serikali imetoa waraka kuzuia Watumishi kupanda madaraja mwaka huu eti hela hakuna, mwenye taarifa za uhakika nisaidie kama ni kweli au ikoje?
 16. MotoYaMbongo

  Naomba kuuliza.

  Naombeni msaada jamani, dada yangu amechaguliwa kidato cha tano Loreza Sec-Mbeya, hatujapata joining instruction naomba kujua mahitaji ya muhimu na aina ya sare ili nimuandalie. Naombeni msaada huo.
 17. MotoYaMbongo

  Ndoa yangu iko hatarini, Ushauri unahitajika.

  Nimeoa mwaka huu. Ndugu wa mke wananjaa sana halafu uelewa wao katika maisha mdogo sana, kila tatizo wakipata kimbilio kwangu, na mimi maisha yamenibana sana siwezi kuwalea. Mke wangu hadi amechoka na anaogopa kuwaambia ukweli, jamani naombeni ushauri nifanyeje. Hali sio nzuri.
 18. MotoYaMbongo

  Naomba kuelimishwa.

  Heshima wana JF, Naomba kujua adhabu ya mtu anayekamatwa na pembe za ndovu kisheria ikithibitishwa bila shaka mahakamani. Kuna jamaa yangu amekamatwa nazo.
 19. MotoYaMbongo

  Ingekuwa Tanzania tungeweza?

  Kwanza nawapa pole wakenya kwa yaliyowakuta, Hatimae operesheni imemalizika na magaidi wote wameuawa, hivi ingekuwa ndio magaidi wameteka jengo Tanzania, vyombo vyetu vinauwezo kwa kukabiliana na tukio gumu la kigaidi? Wataalam tujuzeni.
 20. MotoYaMbongo

  Re: Spika Anne S. Makinda agoma kuzungumzia kama atagombea uraisi 2015

  Yani Bi Kidude akiwa rais, tutakuwa Taifa Mfu.
Top Bottom