"UHALIFU NI NINI?
Uhalifu ni utendaji wa jambo lolote lililokatazwa kutendwa Kisheria au kwa sheria ndogondogo(By Laws) za Mtaa,Kijiji,Kitongoji,Kata/Shehia, Halmashauri au nchi."
Bulaya naye ni mmoja wa wahalifu, aane kwanza kujihukumu yeye
Walipokuwa wanakamatwa watu ambao sio wa mlengo wenu na sisi tukalalamika mlisema kuwa wakiachiwa wataharibu uchunguzi. Hivyo hivyo kwa kakoko akiachiwa ataharibu uchunguzi
Hukuwahi kumsingizia bali uliwahi kupost story za uongo, swali je ni nani alikuwa anakutuma? Maana katika shutuma zako zote hakuna hata moja ambayo uliweza kuweka ushahidi hadharani
Kama alikubali kuja kufungua hilo jengo mwanzoni mwa march, sasa nini kilimzuia maana mpaka tarehe 12 march (karibu na nusu ya mwezi) tuliambiwa kuwa alikuwa ofisini anapiga kazi?
rudia kusoma andiko taratibu labda unaweza kumuelewa mleta mada. Hoja kuu hapa ni kwanini kwenye mambo mengine huwa hafuati sheria? Mfano mzuri ni wabunge wa CUF waliofukuzwa na Lipumba ambaye hakuwa kiongozi wa chama waliondolewa bungeni na kuapishwa aliowateua wakati kesi ilikuwa mahakamani...