Sasa najiuliza hao Wakristo wa Ethiopia waliofuata Ukristo wao tangu miaka 1700 walimsaliti nani? au nini?
Yaani unaleta nukuu ya Kenyatta ambaye ni Gikuyu na tunajua Wagikuyu walikuwa na dini yao kabla ya wamisionari wakisali kwa Kirinyaga (Mlima Kenya). Ila wakati Waethiopia walikuwa Wakristo...
Haiwezekani, Waroma walipofika mashariki waliwakuta Waarabu tayari. Hawakukuta pale Waafrika ili waanze kuzaa.
Pia hujui kitu chochote kuhusu physical features za Abraham au Ishmael.
Siyo inaonekana? Wote wanaona tufe. Wote wanazunguka tufe, sivyo?
Kama Dunia ni bapa, unaizunguka namna gani?
Vipi unaona umbo lake jinsi unavyopita juu yake, kuona mapya kila ukiendelea pale yaliyoonekana kama chini ya upeo (horizon)?
Hasa vipi unasurvive ukirushwa juu vile kama hakuna tufe...
Ukiona maelezo yoyote mtandaoni (kama ni wikipedia au tovuti nyingine), angalia kama inataja marejeo AU kama ni tovuti ya Chuo fulani. Makala hiyo ya wikipedia inaonyesha marejeo, unaweza kuangalia marejeo na kuamua kama zinatosha. (Ziko pia makala za wikipedia bila marejeo au marejeo mabovu)...
Hiyo lugha itafika wapi ilhali watumiaji wake wanaitendea kwa namna hiyo??
Kila duara ni mviringo.
Kimsingi ni bapa lakini inaweza kupindwa pia. Ikipindwa kabisa si duara tena bali tufe.
Hayo maneno yote yana ufafanuzi katika elimu ya hisabati.
Ila wewe endelea tu...
Watu walijua tangu zaidi ya miaka elfu mbili dunia ina umbo la tufe.
Soma yafuatayo:
Eratosthenes wa Kirene alikuwa mtaalamu wa hisabati, jiografia, historia na lugha tena mkurugenzi wa maktaba ya Aleksandria katika Misri. Anakumbukwa hasa kama mtu wa kwanza aliyekadiria mzingo wa dunia...
Na wewe tafakari jinsi unavyotumia lugha. Nusu-duara - je upande wa kushoto au kulia?
Tunajadili Tufe au Duara.
Kwenye tufe hakuna juu au chini. AU: Juu ni kila upande unaoelekea mbali na kitovu cha tufe.
Kaka soma nilichoandika.
Wewe unauliza kuhusu dai tunaenda kwa kasi ya 10,000 km/h, Dai hilo halina msingi.
Ukiongea kasi unahita kusema kasi kulingana na nini?
Maana wakati unapopanda basi ya mwendokasi
unatembea na kasi ya takriban 50 km/h kulingana na barabara chini yako
unazunguka kwa kasi...
unauliza kuhusu:
Aleyn said: "Tena wazungu wanakwambia inazunguka 10,000km/h"
Usiulize "wazungu", ulizia sayansi ya fizikia, pamoja na hisabati
A) Kwenye uso wa Dunia tunazunguka kwa kasi ya takriban kilomita 1666 kwa saa ukikaa kwenye ikweta (=Nanyuki, Kenya). hapa TZ kidogi chini yake...
je una maanisha hali hiyo?
ni kawaida. kama Mwezi uko juuya upeo wa macho, tunaweza kuuona. Kiasi cha nuru yake hutegemea na pembe lake kwa Dunia. Kwa hiyo huwezi kuona mwezi mpevu kabisa wakati wa mchana.
Umependelea kukaa kimya kuhusu mfano wa satelaiti maelfu zinazozunguka Dunia kila siku. Satelaiti zinazorushwa angani kwa roketi, sawa na nateknolojia zinazopeleka vyombo hadi Mwezi au mirihi na sayari nyingine. Satelaiti zinazorushwa tangu miaka 40. Mengine hukaa karibu juu ya uso wa Dunia...
Tuendeleaa polepole.
Kuna tofauti ya kimsingi baina hadithi za Abunuwasi na maelezo ya fizikia na astronomia kuhusu ulimwengu.
Hadithi za Abunuwasi husimuliwa kuhusu mambo yanayotokea kati ya binadamu zikionyesha ujanja na matokeo yake - au matatizo yake.
Katika sayansi ya kisasa...