Huyu mtafiti anayo hoja, labda ni figures tu amekosa, ila ukweli ni huo ndoa nyingi ni mfu, mfano mtaani ninapoishi kuna kaya kama 380, kuanzia 2012 hadi sasa kuna ndoa zaidi ya 100 ninazozifahamu zimesambaratika na nyingi ni za viapo vya kifo kitutenganishe
Ila waTanzania tunajijua kila mtu na siri yake namna anavyoishi
Unakuta mtu analipwa 500K
Anavaa
Anakula
Analipa nauli
Anasomesha
Analipa kodi ya nyumba
Anajenga
Anahonga
Anafungua kibiashara
Anashiriki vikao vya kuzungusha kama tulivyo
Simu haipungui kifurushi
Na hapo hujalipia choo ukiwa mjini mihangaikoni
Hujahudumia Khadija (mtarajiwa)
Hujasafiri kwenda kwenye msiba kijijini
Hujamnunulia mzazi sukari na mafuta ya taa
Hujachangia mambo ya kijamii mtaani kwako
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.