Je, ni kweli kuwa vichaa wana jicho la tatu?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,782
Naamini wote tuna ufahamu wa kutosha kuhusu jicho la tatu, kuona yasiyoonekana katika macho ya kawaida na kusikia pia ikiwemo na ufahamu wa yajayo.

Vichaa ni watu waliodharaulika katika jamii wana majina yote mabaya hawaogi ni wachafu wananuka hawana faida yoyote kuwa na ndugu kichaa ni msiba .

Ukichaa ni familia moja kubwa sana humo wapo machizi, wendawazimu, punguani wote hawa wanaingia kwenye kundi moja kubwa la vichaa.

Kwa tafsiri ya kawaida Ukichaa nk ni kutenda kinyume na kawaida kufanya mambo yasiyoeleweka na kutojitambua kuwa wewe ni nani uko wapi na unafanya nini. Zipo hospital maalum zinatoa tiba lakini kwa kiasi kikubwa mafanikio ni hafifu.

Kwahiyo tuzungumzie Ukichaa katika ulimwengu wa roho na ni kipi ambacho hutokea hata mtu akafikia hatua ya kuwa mwendawazimu chizi au kichaa kabisa.

Lakini vile vile tujiulize ni kwanini vichaa wengi hutibiwa kwa waganga wa jadi hasa wanaitumia maruhani mizimu na majini ? Kisha wakapona kabisa? Hapa sizungumzii wale wanaowehuka baada ya kutumia vitu kama bhangi nk .

Ukichaa ni roho chafu za mapepo majini na maruhani za kutangatanga zinazomuingia mtu na kufanya kikao ndani ya mwili wake...lakini pia kuna ule Ukichaa wa kukiuka masharti fulani ya mizimu ya ukoo au kabila .

Kinachofanyika ni hiki, aidha kwa kutupiwa kukanyaga au kuingiwa na hizi roho , mtu huondoka kwenye kikomo chake cha kawaida cha binadamu cha kuona na kusikia na kufunguliwa ulimwengu mwingine wenye mambo ya kutisha kuwehuka huanzia hapa.

Mwenzenu anaona kabisa mliokaa nao sio watu anakimbia anawashangaa mkimkimbiza na kumfunga kamba kumbe kiuhalisia alichoona ndio hicho ila kwakuwa mmefungwa na kiwango cha kuona nyie mnaona mmekaa na watu.

Huwa tunawashangaa wakiongea pekeyao Kimsimgi hawaongei pekeyao kuna watu wapo karibu yao na wanaongea nao wanapanga nao na kujadiliana mengi tu.

Kwakuwa kilichowaingia ni roho wabaya wachafu wanaotangatanga ndio maana hata siku moja hutamkuta kichaa wa namna hii anaoga au anakaa na kutulia sehemu moja ukimkuta wa hivyo ujue ni wale waliovunja masharti ya kimila kiukoo kuhusiana na mizimu ya kwao.

Nimekuwa na rafiki zangu hapa jukwaani wenye hamu ya kutaka kuwaona wachawi nikaambia wakishakuwa na huo uwezo hawakuwa wao tena! Sababu ni hii!!! Utafika kariakoo na kuona fisi wengi sana utakimbia na kupiga kelele watu watakukamata wakufunge kamba wao wanaona umewehuka wewe unawashangaa.

Utafika kwako utakuta kuna watu wanawanga sebuleni kwako utaanza kupigana nao.. loh mkeo atajua huyu tayari mirembe inamhusu kumbe maskini haoni kile unachokiona wewe.

Mifano ni mingi ngoja nikomee hapa kwanza.
 
Kimsingi na kisekondari hilo ni sahihi.Tuna mtu mwendawazimu mtaani kwetu anaitwa ADAMU.Huyu huwa anasimulia jinsi anavyokwenda kuzimu na manhari ya kuvutia kuliko huku duniani.Huwa anawataja hadi wachawi na wezi wa mtaani kwetu.Mada hii aione pia mshana jr kwa maelezo zaidi.

Hahhahaaaa mshana jr kuja pande hii Crispin Nyoni anakuita
 
Last edited by a moderator:
Hehehe Mshana katika ubora wake kudanganya watanzania.
People always like to hear what they want to hear, ukisema otherwise wanakuona hufai..
Na umewakaba kwelikweli kuwaambia kile wanachotaka kusikia, binadamu na kuamini supernatural.. Hehehehe, what a pitiful specie.
 
mshana jr, yaani avatar yako haijakaa kimaji marefu kabisa , naomba nikuulize nawe ya mapete huwa unayavaa au uko kidigitali zaidi?
 
Last edited by a moderator:
Maruhani ni roho ambazo kwa sehemu kubwa zinaishi nchi kavu, majini kwa sehemu kubwa wanaishi baharini na mizimu ni roho za wafu

Mizimu roho za wafu je ni wafu gani hao unamaanisha watu walokufa zamani yaan ni mababu zetu ktk koo zetu mfan sisi walugulu kule mzimu wetu KOLELO ana siyo
Ina maana roho zao ndo hizo mizimu siyo

Na je hizo roho za maruhani znazoishi nchi kavu ni zipi ? 7bu kwa Hapa tanzania mizimu yte ninayoijua ipo nchi kavu so maruhani ndo mizimu ya hio roho za wafu ?

Majini sehenu kubwa wanaishi baharini je waliobaki wanaishi wapi ?

Maruhani sehemu kubwa wanaishi nchi kavu je waliobaki wanaishi wap ?
 
Back
Top Bottom