Fahamu utajiri kwenye biashara ya fedha za kigeni (FOREX TRADING)

Davion Delmonte Jr.

JF-Expert Member
Oct 27, 2013
2,149
1,710
Huu ni mwendelezo wa mada nilizokuwa nikiandika
i) Treasury bills
ii) Treasury bonds (Utajiri uliopo kwenye dhamana za serikali: Sehemu ya II (bonds))
iii) na leo ni FOREX TRADING (Fahamu utajiri kwenye biashara ya fedha za kigeni (FOREX TRADING))

Kwa ambao walikua hawafahamu kwamba, biashara ya fedha za kigeni (forex trading) ndiyo ndiyo biashara yenye ujazo mkubwa wa mapato (turnover) kwa siku kuliko biashara yoyote duniani. Inakadiriwa kwamba kwa wastani wa siku moja forex trading inafikia turnover ya zaidi ya trilioni 4 za dola (ambazo kibongo bongo ni kama trillion 8000).

Hii ni maradufu hata ya biashara inayofanyika pale new York stock exchange kwa siku ambayo yenyewe inafika kwenye dola zaidi ya bilioni 70. Hivo ni dhahiri kabisa soko la fedha za kigeni (forex market) ndilo soko kubwa zaidi ulimwenguni katika masoko yanayohusisha uwekezaji wa kifedha.

Hivo katika ujazo huo mkubwa wa biashara kwenye fedha za kigeni ni wazi kwamba kila siku kuna utajiri mkubwa unaotengenezwa na biashara hii. Na ni watu wengi sana wananufaika nayo.

Biashara ya fedha za kigeni ni nini?
Kwa maana rahisi kabisa biashara ya fedha za kigeni ni kununua pesa ya nchi fulani na hapo hapo kuuza pesa ya nchi nyingine ili kufanya ubashiri wa bei kwa lengo la kujipatia faida.

Mfano tu mimi nnavoenda kariakoo bureau de change pale nnapotoa shilingi 2100 na kununua dola moja kwa dhumuni la kwamba huenda baada ya mwezi mmoja dola ile moja itapanda na kuuzwa 2350 na hivo ntakua nimepata faida. Hapo tunasema umejihusisha kwenye biashara ya fedha za kigeni.

Sababu kubwa inayovutia watu kuingia kwenye biashara hii nnayoiita ya? ubashiri?; ni kuwa thamani ya fedha ya nchi fulani inakuwa na tabia ya kupanda au kushuka dhidi ya fedha ya nchi nyingine kutegemeana na sababu nyinginyingi kama hali ya uchumi na jiografia ya kiasiasa ambazo ntaziongelea baadae. Hivo lengo hasa la wanaofanya biashara hii ni kutumia kupanda na kushuka huku kwa fedha fulani ili kunufaika.

Biashara hii inafanyika vipi ?
Katika biashara ya fedha za kigeni kuna kitu kinaitwa hapa ni unakua unaongelea zile fedha ambazo unataka kuzitumia katika kufanya ubashiri wako. Pair maarufu katika forex market ni kama EUR/USD, GBP/USD, USD/CHF na USD/JPY hizi pair zenye USD zinaitwa major pair.

Kabla ya kwenda moja kwa moja kuelezea fursa za biashara hii ya forex trading kwa Tanzania, nitagusia kidogo wenzetu walioendelea nchi za ulaya, marekani na mataifa ya Asia namna wanavoifanya biashara hii.

Kwa watu wa nchi hizo biashara ya FOREX inafanyika online. Yaani katika hayo mataifa huwa kuna ;FOREX brokers?; ambao mtu akishajiunga na broker wake basi anafanya deposit ambayo hiyo inakuwa ndiyo mtaji wa muhusika. Baada ya hapo akisha ingia online kuna platform kwenye program ambayo inasimamiwa na broker wake inakuwa inaonesha list ya pair za fedha za kigeni ndipo atakuwa ananunua ama kuuza fedha zake.

Ila msingi mkubwa unakua ni ule ule mfano: kama mtu ana mtaji wa $ 10,000 halafu anataka kufanya ubashiri wa kununua EURO. Akiingia kwenye online platform yake ataona bei ya kununulia EURO ie EURO/USD = 1.23 ikiwa na maana EURO moja inauzwa kwa dola 1.23. Hivo hiyo dola $ 10,000 kwa bei ya 1.23 itaweza kununua EURO (10000/1.23)=8130.08

Kwa hiyo imetumika $ 10,000 ambayo imenunua EURO 8,130. Na mwekezaji amefanya hivo penginepo kwa kubashiri kuwa bei ya EURO dhidi ya dola itapanda. Kama inatokea utabiri wake unakuwa kweli na bei ya EURO kwa dola inapanda na kufika EURO/USD = 1.37 ina maana sasa akiziuza tena zle EURO 8,130.08 atapata USD(8,130.08?-1.37)= 11,138.21 wakati pesa aliyokuwa nayo kama mtaji ni $ 10,000 lakini kutokana na ubshiri wake ameshatengeneza faida ya $ 1,138.21 ambayo itakuwa inaonekana kwenye system za computer.

Hivo ndo namna biashara hiyo kwa wenzetu inavofanyika. Lakini sababu dunia sasa ni kijiji, bishara hii unaweza kufanya hata kwenye simu yako hiyo ya smartphone. Nimegusia tu kwa hapo maana lengo langu ni kuzungumzia biashara hii kwa mazingira ya Tanzania na namna unaweza ukatengeneza utajiri.

Watoto wa mjini wanasema pesa ndefu. Ila kwa wale ambao wanataka pia kupata uzoefu na kuifanya kama wenzetu walioendelea basi kuna hawa ma FOREX broker unaweza ukawagoogle: FXCM, eTORO, DUKASCOPY na XM. Hawa ni mabroker wa kuaminika na wote wana mpaka apps za simu kwa hiyo ukipenda unaweza ukawaangalia na kujifunza.

Jua yafuatayo kwanza
Kabla ya kufanya biashara hii nnayoiita ya ubashiri; ni vema ukawa na uelewa wa kujua ni kitu gani kinapelekea thamani ya pesa ya nchi inaporomoka ama kupanda dhidi ya fedha ya nchi nyingine.

Ni kama biashara ya bidhaa nyingine tu, mfano katika kilimo mkulima anaweza kubashiri bei kubwa ya mazao yake kwa sababu mvua zilikuwa chache na mavuno ni kidogo hivo ujasi wa bidhaa sokoni ukiwa ni mdogo na mahitaji hayajabadilika ni dhahiri bei itakuwa ni kubwa kwa mazao yake, hivo atakuwa sahihi kwa ubashiri wake aliofanya kabla.

Vivo hivyo katika biashara ya fedha za kigeni unaweza kubashiri kushuka au kupanda kwa thamani ya fedha yako dhidi ya fedha nyingine ili kujua kwa usahihi kama ni wakati muafaka wa kununua ama kuuza fedha za kigeni.
Kama mwekezaji unatakiwa kujua sababu jumla za kuporomoka ama kupanda kwa thamani ya fedha ya nchi dhidi ya fedha ya nchi nyingine. Sababu hizo ni kama zifuatazo na uhusiano wake katika thamani ya fedha.

i) Mfumuko wa bei (inflation), inflation ikiwa ndogo inaonesha thamani ya pesa ipo juu kwa sababu pesa inakua na uwezo mkubwa wa kununua kwa sababu bei zipo chini. kinyume chake ni sahihi kwamba kama mfumuko wa bei unakua ni mkubwa dhidi ya nchi tunazofanya nazo biashara iki maanisha wao inflation inabaki kuwa ndogo ina maana lazima pesa yetu ipoteze thamani dhidi ya pesa yao.

Kwa nchi yetu hapa kwa sababu tunatumia sana dollar inamaana kwamba ki nadharia trading partner wetu ni USA ambao wao inflation yao ipo chini ya 2%. Kwa hiyo ni kwamba kwa vyovyote vile kama mfumuko wa bei unapanda ina maana tutegemee kuporomoka kwa thamani ya pesa yetu dhidi ya USD.

Kwa kutumia baadhi ya takwimu utaona ni namna gani mfumuko wa bei kwa kiasi fulani japo yaweza kuwa kidogo namna inahusika na kuporomoka kwa thamani ya fedha yetu.


Mfumuko wa bei.
Monthly weighted Average $ price

Ukiangalia chati hiyo kwa makini ni kwamba mfumuko wa bei una uhusiano wa moja kwa moja (+) na kupanda kwa bei ya dola. Japo inawezekana kwamba sio inflation imepelekea hivo lakini uhusiano upo hata kama ni kidogo.

Kwa mwekezaji wa FOREX taharifa kama hizi ni za muhimu na lazima uzielewe kwa haraka mfano bureau of statistics ikitoa makadirio kuhusu inflation basi itakuwezesha at least kupata picha nini kinaweza kujiri kwa wajati ujao hivo uweze kufanya ubashiri wako vema.

ii) Nakisi katika biashara, hili wengi tunalifahamu kwamba nchi yetu tunaagiza nje (import) zaidi kuliko tunavyouza nje (export). Hivo kinachotokea shilingi yetu inapata pressure kubwa kwa sababu utalii tunaoutegemea utuletee dola ulikua umedorora. Na wakati huo huo tuna import zaidi matokeo yake ni kwamba too many shillings chasing too little dollars? na kupelekea pressure ambayo ikapandisha bei ya dola sokoni.

Sasa kama mwekezaji pindi unapopata taarifa za mwanzo kwamba kwa mfano import zinaongezeka au utalii umedorora. Moja kwa moja ubashiri wako utakuambia kwamba baada ya kipindi fulani bei ya dola itapanda. Na kama ulizinunua kabla basi utakuwa umefaidika. Nchi za ulaya na America kama import zinaongezeka masoko huwa yanapata shocks. Kwa sababu wawekezaji wanatenda kutokana na taarifa wanazosikia.

Kwa hiyo ukiwa mbashiri taarifa ni muhimu sana.

iii) Deni la taifa, hili linasikika kila siku kuhusu mzozo wa madeni wa ugiriki na misukosuko inayoipata sarafu ya EURO kila kukicha.

Ni kwamba nchi ikiwa na madeni makubwa yatapelekea presha ya mfumuko wa bei kwa sababu serikali itavutiwa kuprint more money ili kulipa madeni. Kitu ambacho kitaongeza ujazo wa fedha kwenye mzunguko na utapelekea mfumuko mkubwa wa bei na kushuka kwa thamani ya fedha.

Kwa waliosoma Historia kama mimi, baada ya WWI Germany aliamriwa kulipa War reparations kwenye Versailles treaty. Kilichotokea wakati huo Germany iliyokuwa inaongozwa na Weimer iliamua kuprint money ili iweze kulipa madeni ya war reparations lakini matokeo yake ilipelekea inflation kuwahi kutokea duniani na mwaka 1923 1USD=4,210,500,000,000 Gr.Marks

Hivyo kama mbashiri waweza kuangalia kwamba kwa Tanzania deni letu la nchi bado ni kubwa sana kwa hiyo unaweza ukabashiri kuwa shilingi yetu yawezekana ikaendelea kuporomoka huko mbeleni. Hivo kwa mfano unaweza kutumia ubashiri wako kununua dola nyingi kwa sasa ili baadae uje kuziuza ghali na kutengeneza faida.

iv) Performance ya uchumi wa nchi, ukuaji mzuri wa uchumi unaenda sambamba na thamani ya pesa ya nchi. Nchi kama Botswana au Rwanda pesa zao zipo imara sana kwa sababu chumi zao zipo stable na zinavutia uwekezaji kutoka nje ambao pia ni chachu ya kuwa pesa iliyo imara.

Kama mwekezaji kwenye FOREX lazima uwe unajua mwenendo wa uchumi wa nchi unakwendaje. Ili ufanye ubashiri mzuri huko mbeleni mambo yatakuwaje. Kwa Tanzania hapa itabidi usicheze mbali na machapisho ya banki kuu ya Tanzania.

v) Amani ya nchi, hili lipo wazi wewe kama kutakuwa na machafuko ni dhahiri lazima shilingi idorore. Hivo pia sio mbaya ukabashiri na hali ya nchi kwenye amani itakuwaje. Kama unahisi amani itatoweka unaweza ukaanza kununua fedha za kigeni nyingi kwa sababu baadae lazima ufaidike.

Sababu hizo hapo juu pamoja na nyingine nyingi ni mambo ambayo kama unataka kujiingiza kwenye biashra hii ya FOREX TRADING lazima uyaelewe ili ujue mbeleni mambo yatakuwaje.

Kumbuka biashara hii ni ya kubashiri na kitu cha kubashiri siku zote hatari yake ni kubwa. Hivo kama ulikosea kuzisoma alama hizo hapo juu vizuri basi tambua utaangukia katika hasara kubwa.
Kwa ufupi hii pia ni biashara yenye hatari (risk) kubwa mno.

Unatengeneza vipi pesa kupitia FOREX TRADING kwa Tanzania?
Kwa Tanzania na nchi nyingi masikini bado hawajaweza kuwa na mfumo ulio advance kwenye FOREX TRADING kama wenzetu wa nchi za magharibi.

Hivo kwa nchi kama Tanzania FOREX TRADING itakuwa inafanyika physically kwa kutumia Bureau de change ambazo zipo kwa wingi. Yaani mfano pale unaposoma viashiria vyako ukaona kwa mfano USD, GBP au EURO zitaenda kupanda, utachofanya ni kwenda kuzinunua na kuzihifadhi. Ukisubiri mda fulani ufike na zenyewe ziwe zimepanda bei.

Mfano
Katika mfano huu ufuatao nitaonyesha fursa zilizopo kwenye biashara hii kwa kuangalia ni pesa kiasi gani mtu angetengeneza kama kwa kutumia viashiria nilivovielezea hapo juu na kufanya ubashiri angewekeza kununua fedha za kigeni na gold kwa mwaka 2003 na kuziuza kwa mwaka 2013 yaani baada ya miaka kumi.

Baada ya kuangalia takwimu za kiwango cha kubadilishia fedha kwa miaka kumi iliyopita ambazo zinatolewa na banki kuu ya Tanzania.

Nilifanya uchambuzi na kugundua tangu mwaka 2002 hadi 2013 kuna bei za feza za kigeni zilipanda kwa zaidi ya asilimia 100 kwa Tanzania bila kusahau gold ambayo toka mwaka 2003 mpaka 2013 ilipanda bei kwa asilimia 884%.

Kwenye chart ifuatayo nitaorodhesha bei ya kununua kwa mwaka 2002 na bei ya kuuza kwa mwaka 2013 au kwa mwaka2012 kwa fadha za kigeni ambazo ni imara. Nimechagua Japanese YEN, USD, EURO, GBP, CANADIAN dollar, SWISS FR, south African Rand, New Zealand Kiwi na bila kusahau GOLD ambayo nayo kwenye FOREX TRADING inahesabika kama fedha.

Fedha ya kigani
Bei ya kununua unit moja kwa 2002 (TZS)
Bei ya kuuza unit moja kwa mwaka 2013 (TZS)
Ongezeko la bei katika asilimia. %


USD 991.561564.33
57.76
1424.08
2553.62
79.32


EURO
871.28
2073.68
138

YEN JAPAN
7.41
17.16
131.57

SWISS FRANC[/TD]
595.7[/TD]
1716.41[/TD]
188.13[/TD]


CANADIAN $
622.17
1584.13
154.61


NEW Z. KIWI
434.8
1307.47
200.7

SA RAND
8.67
18.6
114.53

GOLD/OZ
303,317
2,624,440.64
765.24

Ikiangalia hapo kwenye jedwali katika upande wa asilimia hapo ndipo kwenye utajiri. Mfano tu kama ulitumia TZS 100,000,000 kwa mwaka 2002 kununua GOLD kwa mwaka 2013 ungekuwa na kiasi cha (7.65*100,000,000)= TZS 765,000,000 ambayo ni sawa na faida ya TZS 665,000,000 ndani ya miaka kumi.

Au kama ungetumia pesa hiyo kununua New Zealand KIWI kwa mwaka 2013 ungekuwa na kiasi cha (2.007*100,000,000)= TZS 200,700,000 ambayo ni sawa na faida ya TZS 100,700,000.

Waweza tumia mfano wa kiasi chochote cha pesa kwa kuangalia ongezeko la asilimia na kujua kiasi ambacho kingepatikana baada ya kipindi cha miaka kumi kupitia jedwali letu.

Nimeamua kutumia mfano wa zamani kabisa nikiwa na sababu ya kuonyesha ni jinsi gani uwezo wa kubashiri ongezeko la bei litavokunufaisha kwa kiasi kikubwa na kwa faida kubwa ambayo huwezi kuipata kokote kwenye masoko ya fedha.

Hivo kama mwekezaji katika fedha za kigeni lazima kwanza uwe na jedwali lako kama hilo na kwa kutumia vile viashiria nilivovielezea unaweza kumulika hali ya bei hizo kwa miaka ijayo.

Ukiwa katika biashara hii ni suala la lazima kufatilia habari. Kwa mfano kama ulifanya ubashiri wa kununua EURO lakini ukiangalia kwamba nchi ya Ugiriki ina hatari ya kuondoka kwenye sarafu hiyo inamaana kuna wasiwasi wa bei ya EURO kushuka hivo cha kufanya hapo kama ulikua umenunua EURO unatakiwa uziuze ili kuepuka hatari ya hasara huko mbeleni.

Hivo ndivo biashara hii inavofanyika suala la habari na taarifa ni muhimu mno na lazima uwe makini katika maamuzi ya kuuza au kununua kutegemeana na habari unazopata.

Itoshe tu kusema biashara hii mbali na kuwa na faida kubwa pia ina hatari kubwa sana na inahitaji umakini.

Kwisha kusema hayo nadhani kuna uelewa fulani fulani umepatikana kunusu biashara hii ya fedha za kigeni (FOREX TRADING) namna inavofanyika kwa nchi za wenzetu na pia fursa zilizopo kwa nchi kama Tanzania.

Kama kuna member atakuwa na maswali zaidi basi kama kawaida JF ni kuacha comment tu na pia kama kuna nyongeza yoyote ile ambayo sikuiweka. Maana nimejaribu ku summarize kidogo sababu biashara hii ni pana sana.

nakala kwa Econometrician Bavaria bukoba boy kezacute
 
Mkuu asante kwa darasa,ningeomba ushauri kwa kuanza na 150,000 Tsh je naweza kununua fedha gani ili kukuza mtaji?
 
braza thread zako zote nimezipenda na kiukwel zinasaidia sana... lakini inaonekana umebase kwa watu wa kipato cha juu sana, kwa thread zote tatu tofauti sidhani kama utaweza kufanya hizo kitu kwa chini ya m10 za kitanzania!!!! na kama itawezekana faida yake inakuaje labda baada ya mwaka hivi
Hata ukiwa na pesa chini ya milioni. 10 inawezekana. Ni wewe tu kuangalia vile viashiria halafu ukanunua FOREX. Kama ulibashiri vizur hata kwa mwaka mmoja utapata pesa nzuri tu.
 
mkuu asante kwa darasa,ningeomba ushauri kwa kuanza na 150,000 Tsh je naweza kununua fedha gani ili kukuza mtaji?
Mkuu ni wewe tu hapo, currency za kununua zipo nyingi sana. Watu wamezoea usd lakini Kuna currency nyingi haziongelewi ambazo zina faida kubwa sana.

Sema Kabla ya kununua unatakiwa kujiuliza Kama Kuna uwezekano wa bei yake kupanda kwa kutumia vile viashiria vya kubashiri ambavyo ni mfumuko wa bei, deni la taifa, nakisi ya biashara, na Taarifa nyingine nyingine. Maana ukumbuke kwenye biashara hii lazima uwe mtu wa kusikiliza taarifa mbali mbali.

Ukisha jiridhisha sasa ndipo unaweza kununua Forex. Biashara hii Ina risk kubwa sana. Kwa hiyo lazima uwe makini.
 
Hii kitu ukikosea currency ikaenda against you unaeza kulia. I lost more than $5,000 japo nilipata highlights zote all the time and suggestions, sina hamu nayo ai em sole..even though its much better if u are trading out of the United States the rates of buying and selling aren't super high kama ukiwa ndani ya hiyo nchi

But hey guys... Donald Trump got rich through this. Kujaribu sawa ila rahisi sana kukata tamaa hasara nje nje hadi ifikie win win its mostly like u getting back what u lost.
 
Ubarikiwe mkuu.

Lakini inahitaji umakini wa hali ya juu hii Biashara.Sio nyepesi kama watu wanavyonukuu

Uzuri wake mtu yoyote anafanya kwa mtaji wowote.
Mie ninajamaa yangu yupo Hotel,ni Housekeeper,basi yeye tipu zake zoote huwa anaziweka na kuzibadilisha kwenda Tsh baada ya miezi sita,angalau huwa anaambulia chochote cha tofauti pale katika kupanda kidogo.Na akiona haijapanda huwa anakomaaa,hahaha aiseee inabidi uwe kichwa ngum lakini.

Ila mie nahisi ili ufanye hii kwa ufanisi uwe na link kama Nchi nne hivi.Uganda,Burundi,Kenya,Comoro,ili kama hapa bei ipo chini basi unaweza kuwa na jamaa huko ukapata exchange rate kwa bei nzuri.Ila kwa soko la humu nchini tu,bado halijawa zuri saana na sio rafiki kwa mfumo huu.Maana mie nilikuwa nafanyakazi mtaa wenye Bureau de Change nyingi,kuna siku unakuta rates inabadilishwa mara tatu kwa ndani ya siku moja.
 
Back
Top Bottom