Biashara ya Kuchakata na Kufungasha Unga wa Mahindi (Sembe na Dona)

FIDO DIDO

Member
Mar 6, 2012
24
7
Maize-Flou.jpg


Hellow wanaJF,

Nina wazo la kuanzisha biashara ya kusaga unga wa sembe na ku-pack kwa ajili ya kuuza. Jamani naombeni mawazo yenu.


WADAU WENGINE WANAOHITAJI KUJIFUNZA KUHUSU BIASHARA HII
Kutokana na ripoti ya umoja wa mataifa kupitia shirika la WFP, nchi zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara zinakabiriwa na ukame, hilo huenda likasababisha ukosefu wa chakula miongoni mwa jamii maskini.

Kutokana na ripoti hizo, ndipo nikaja na wazo la ujasiliamali baada ya kuona mambo ya ajira hayasomeki, ikichukuliwa sasa hivi ndo niko mwaka wa mwisho chuoni.

Kama habari inavyojieleza kuna mikoa yenye njaa hapa nchini kama vile Simiyu, Dodoma, Singida na kwingineko.

Kwa sasa niko Kigoma likizo-nyumbani, so wakati wa mavuno mahindi huwa bei chee huku, mfano gunia la debe 6 huwa ni Tsh 35,000/= tu. Sasa ndipo nimefikilia kwa mtaji wangu wa Tsh 1,000,000/= ambayo ni kujipinda na kuweka hela ya bumu ninaimani nitaipata.

So, kwa wakazi wa mikoa hiyo na mingine, pia wazoefu wa hii biashara ya kuchukua mahindi huku na kuyasaga unga wa dona na kuyauza mikoa hiyo siwezi kupata faida?

Nawasilisha.
Habari zenu wadau,

Ninaomba kama kuna mzoefu wa biashara hii aweze kunisaidia mawazo jinsi ya kuanzisha biashara ya kusaga, kukoboa na kuuza unga pamoja na kujua ni mashine aina gani zinafaa kwa kazi hii pamoja na bei zake.

Natanguliza shukrani.


MICHANGO YA WADAU KUHUSU BIASHARA HII
ABC'S ZA KUANZA NA KUENDESHA HII BIASHARA
Mambo unayotakiwa kuangalia ni kama ifuatavyo:

Mtaji wa biashara
Hakikisha una mtaji wa kutosha utakao wezesha kufanya yafuatayo:
  • Kulipia pango la sehemu ya biashara
  • Kununua mahindi, kukoboa, kusaga,kufunga kwenye mifuko
  • Kulipia gharama za kusafirisha unga kutoka masjine hadi sehemu yako ya biashara
  • Pesa ya kutosha kulipa mishahara ya wafanyakazi angalau miezi mitatu ya mwanzo
  • Akiba kwa ajiri ya dharura
Upatikanaji wa mahindi
Lazima ufahamu kuwa upatikanaji wa mahindi hutegemea msimu. Kuna wakati mahindi yanakuwa mengi sokoni na bei yake inakuwa nafuu. Wakati ambao sio wa msimu mahindi yanakuwa machache na bei yake ni ghali. Kwa wale wanaoishi Dar es Salaam hutegemea mahindi kutoka Songea, Iringa, Mbeya, Rukwa na Dodoma

Msimu mzuri wa mahindi kwa wafanya biashara wa Dar ni June – December na msimu mbaya ni January – Mei. Kwa Dar es Salaam mahindi yanapatikana Manzese Darajani au Tandale asubuhi na mapema kila siku ispokuwa Jumapili na sikukuu

Aina ya Mahindi ya Kununua
Itabidi upate uzoefu wa kufahamu aina nzuri ya mahindi kununua ambayo ni yale yenye kutoa unga mwingi na pumba chache. Mahindi mabaya ni yale yenye kutoa pumba nyingi na unga mchache. Kwa taarifa yako, mara nyingi mahindi yenye mbegu kubwa uhusishwa na pumba nyingi, unga mchache

Jinsi ya Kununua mahindi
Inategemea na ukubwa wa mataji alionao mfanya biashara ambapo kama ana uwezo ni heli anunue mahindi mengi kwa wakati mmoja na kuyaweka ili wakati bei ya mahindi ikipanda basi yeye atakuwa hana matatizo

Kama nafasi ya mfanyabiashara kipesa siyo kubwa sana anaweza akanunua mahindi ya gari zima; yaani tani 10, 20 au 30 kutegemea uwezo wake kipesa.

Wengine hawana uwezo wa kununua mahindi ya kujaza gari zima lakini wamo kwenye hiyo biashara. Wanachofanya ni kuungana wafanyabishara wadogo watatu au wane na kuchanga pesa za kuweza kununua gari zima

Upatikanaji Mashine ya kukoboa na kusaga mahindi
Kama una mtaji wa kutosha basi ningekushauri ununue mashine ya kukoboa mahindi na ya kusaga unga. Lakini kwa kuwa unaanza hii biashara kwa mara ya kwanza sio vizuri kutumia pesa nying kununua mashine wakati bado huna uhakika na biashara yenyewe.

Unachoweza kufanya ni kukoboa mahindi na kusaga unga ukitumia mashine ambazo tayari zipo na gharama yake huwa ni nafuu. Kwa wale wakazi wa Dar es Salaam juna mashine nyingi tu maeneo ya Manzese Darajani na Tandale

Ufungashaji wa unga (packaging)
Kwa wakazi wa Dar es Salaam pale Tandale wako wataalamu wa kuchora nembo itakayotumika kutambua biashara yako na vile vile watapiga chapa mifuko yako. Gharama huwa inakuwa juu kwa mara ya kwanza lakini gharama hiyo upungua baadaye kwa kuwa utengezaji wa nembo hufanyika mara ya kwanza tu.

Unaweza ukatengeneza mifuko ya ujazo wa 5kg, 10kg, 25kg na 50kg kutemea na aina ya wateja utakaohudumia

Uuzaji unga wa sembe
Hii hatua inahitaji upate msaada kutoka kwa washauri wa masoko (marketing consultants) ambao watakuelekeza jinsi ya kufanya utafiti wa soko, kujitangaza, kutangaza bidhaa, mikakati ya mauzo na kadhalika

Mahali pa kufanyia biashara
Hakikisha kuwa unapata sehemu nzuri ya kufanya biashara ambapo kuna nafasi ya kutosha kufanya biashara na pana vutia kwa wateja. Pia pawe na usalama wa kutosha kwa wateja na vifaa vya kufanyia kazi.

Aina ya wateja utakaohudumia
  • Ni vizuri ufanye uamuzi ni wateja gani unataka kuwahudumia- wafanyabiashara ya unga wadogo, kati au wakubwa
  • Tafiti ni aina gani ya huduma wateja wanapenda
  • Baada ya kufahamu aina ya wateja unaotaka kuwahudumia ni vizuri kufahamu ni huduma gani inavutia hao wateja wako.
Weka vivutio sehemu ya kufanyia biashara
Hakiksha sehemu ya biashara inavutia kwa kuweka vifaa kama television, music system, air conditioner na kadhalika

Mvuto wa Wafanyakazi
Hakikisha wafanyakazi watakatoa huduma kwa wateja ni nadhifu na wanapendeza kutokana na mavazi yao. Pia wafanyakazi wawe wachangamfu kwa wateja

Bei ya unga wako wa sembe iwe yenye mvuto
Hakikisha bei za mifuko yako ya unga sio za chini sana kiasi cha kufanya biashara iendeshwe kwa hasara au za juu mno kufanya wateja washindwe kuzimudu

Uwekaji wa hesabu za biashara
Unatakiwa uwe na utaratibu wa kuweka kumbukumbu za manunuzi ya vitu, malipo mbali mbali, pesa za mauzo na kadhalika. Kumbukumbu hizo ndizo zitakazosaidia kutengeneaza hesabu zitakazoonyesha kama biashara inaendeshwa kwa faida au hasara

Weka pesa zako benki
Hakikisha pesa zote zinazotokana na biashara zinawekwa benki. Usichanganye pesa za biashara na matumizi yako binafsi.

Credit: siriyamafanikio.blogspot
MASHINE NA USIMAMIZI
- Unatakiwa uwe na machine nzuri sana ya kukoboa na kusaga (unaweza kusaga unga kwa mara ya pili ili kupata unga laini zaidi)
- Uwe na mahindi mazuri ambayo hayajaliwa na wadudu (lengo unga usiwe na harufu ya uozo)

- Sehemu nzuri ya kuhifadhi unga ili usiharibike (kusiwe na joto sana wala unyevunyevu), njia nzuri na rahisi ya kumaintain quality ya unga ni kuuanika juani baada ya kusaga kabla ya packaging (ukipigwa jua siku 3 au 4 utadumu muda mrefu sana)
- machine za mafuta zipo (kerosine) huwa zinatumika sana vijijini.

- Solar machine sijawahi kusikia & am sure haiwezekani c'se energy consumption ya machine ni kubwa sana, kupunguza consumption unatakiwa kusaga mahindi mengi bila kuzima zima machine

Challenge: Unahitaji watu waaminifu sana kusimamia machine yako na watu wa kuyasafisha mahindi vinginevyo utaibiwa vibaya sana
NI BIASHARA NZURI, INAHITAJI ENEO LENYE NISHATI ISIYO YA KUSUASUA
Hii biashara nilishawahi ifanya na mzee wangu ni kazi nzuri ukiwa na capital ya kutosha. changamoto zake kubwa ni upatikanaji wa mahindI hasa kuanzia miezi ya kumi na mbili mpaka wa nne.

Faida yake sio ya kutisha ila inalipa sana, nyingine ni umeme hasa kwa maeneo ya Dar ni taab sana hii inakulazimu mara nyingi kazi ifanyike hata usiku, pia site yake ingependeza iwe eneo karibia na transformer ili uwe unapata umeme wa kutosha. Kwenye soko pia mwanzo ni mgogoro sana ila ukishakuwa na jina na hasa ukapata wateja kama wacomoro umepeta.

Kitu kingine ni wanafanyakazi, hapa ndio tatizo inabidi upate wafanyakazi waminifu sana na mara ya mwisho ilikuwa kukoboa na kusaga kwa tonne moja ilikuwa ni 2500, hapo bila kushusha mzigo toka garini. Ukija kwenye upande wa kusagia wateja hapo ni wewe tu ila jua mashine nying unazoziona Dar ni za kusagia wateja na hapa kwang mimi ndo naona inalipa sana.

Mwaka juzi tone moja kusaga na kukoboa ilikuwa ni 30000 na ukiwa na kinu kizuri unaweza futa mzigo wa tonne 30 per 24hrs. ila kuna watu temeke wanatengeneza mashine complete set the last time ilikuwa 70mil na per day inauwezo wa tonne60. Mara ya mwisho nilipopita stereo ilikuwa haijaanza fanya kazi. Kwa ujumla ni kazi nzur sana; nikijikusanya lazima na mimi niiifanye, ila in the hot cake ni unga wa ngano sijui wanafanyaje kina Azam.
UNATAKA MASHINE YA KUCHONGA AU YA DUKANI, CHAGUO NI LAKO

Kuna mashine za kuchongesha SIDO na nyingine unaweza kununua mojamoja dukani japo vinu huwa vinakuwa vidogo kwa hizi za dukan. Nadhan za kuchongesha ni nzuri zaid coz ni ngumu, bei nafuu na pia unaweza kumwambia mchongeshaji akutafutie zile mota za zamani ambazo zinauwezo mkubwa. Mashine (kusaga & kukoboa) mpya kwa Arusha dukani ni Tshs 4.7mil na SIDO unapata mpaka kwa 4.6 mil.

Kwa wachongeshaji wa mitaani zinapatikana kwa mil3. Mtafute huyu jamaa anachongesha mashine nzuri na anakufanyia installation mwenyewe bure kama utanunua kwake. Anaitwa Tall anapatika Ngarenaro kwa wale wa Arusha. 0754315171.

Wanachokifanya hawa jamaa ni unatafuta mashine mwenyew unayoippenda then unawaonyesha wanalipa hela na wanakufanyia installation kazi inabaki kwako kuwarejeshea hela. Wenye hii kampuni ni wazungu kwa maelezo zaid unaweza kumpgia huyu jamaa wa kizungu.
MASHINE BORA NI IPI?
Hongera kwa jitihada zako za kukamilisha ujenzi wa kiwanda cha unga, kwangu mimi nilitaka tu kukupa ushahuri kuwa katika dunia ya leo hatutumii tena roller machine kwa kukoboa kwani inakuwa na wastage kubwa ya mahindi, wastani wa gunia la kilo 108 kgs kwa roller machine utajikuta unapata kg 75 au 78 za mahindi, lakini kuna mashine za kisasa output baada ya kukoboa inakuwa kg 92 hadi 95 ktk gunia la kg 108 hii inakupa faida kubwa na tija zaidi.

Ukiamua kutegeneza unga wa dona, machine hii ndo yenyewe, capacity yake ipo ya ton 20 kwa siku, 30tons kwa siku hadi 50tons inategemea utaaamua kutumia hammer mill au vip, hata hivyo ktka kusaga kama utaamua kutumia hammer mill ni wakati mzuli kupata vinu vizuli vya kisasa kabisa vinavyotumia motor ya HP50 vinu 3 stainless steel unga unakuwa bora sana na sio carbon steel mill.

Haya bwana, kazi ni kwako. Thanks
CHUKUA UZOEFU HUU
By experience! Nenda mikoa ya Iringa au Mbeya, nunua mahindi moja kwa moja kwa wakulima, sogeza mahindi kwenye mashine ya kusaga iliyo karibu ili kupunguza carriage cost!

NB: Hapa uwe umeshaongea na watu wa mashine, ikiwezekana uwe unawaachia pumba ili gharama ya usagishaji iwe chini zaidi (chini ya 5000/= kwa gunia)

Mahindi yakifika kiasi unachotaka, anza kusaga na kupaki(kwa kuanza unaweza kuwa unatumia mashine ya kushonea ya kukodi na mifuko yenye nembo ya mtu mwingine (mtafute)!

Gharama ya mfuko tupu usio na nembo ni around 200-350 bei ya jumla na 400-600 wenye nembo)

Kipimo kiwe kilo 5, 10, 25 na 50 (gharama ya upakiaji kwa makuli ni around 700 kwa kila kilo 50!

Tafuta magari yanayosafirisha mizigo mikubwa, ongea nao wakuunganishie mzigo wako kwa wasafirishaji wengine (madalali are so good in this)!

Mzigo ukifika mkoa wako wa soko waombe wakushushie sehemu ambayo ni rahisi kwako!

Sambaza mzigo kwa wateja wako!
 
Wazo lako ni zuri, kwani kuwekeza ktk chakula na ukahakikisha unakidhi viwango na mahitaji ya walaji wako utanufaika na kunufaisha wengi, binafsi nakushauri endelea na mpango wako.
 
Ni biashara nzuri, tafuta location nzuri ambayo distribution itakuwa within that radius, then capture the market with quality product and competitive price.
 
Asante mkuu nipo na Dar na nimetafuta location maeneo ya kimara kwa ajili ya kufunga mashine but sijapata kampun ya uhakika ya kunitengenezea mifuko kwa ajili ya ku-pack.
 
Ahsante mkuu nipo na dar na nimetafuta location maeneo ya kimara kwa ajil ya kufunga mashine but sijapata kampun ya uhakika ya kunitengenezea mifuko kwa ajil ya ku pack.

Watafute Hill Packaging. Huyu jamaa mmiliki anaitwa Hillary ni mjasiriamali mzuri sana, ana kiwanda cha kutengeneza viroba kipo mapinga Bagamoyo mwanzo kabisa karibu na Bunju.
 
Mkuu hiyo ni plani nzuri sana na hata mimi nina huo mpango na naendelea kuuvutia kasi.

MKUU HII BIASHARA UKIWA SIRIAS UNAWEZA KUWAFIKIA WAKINA AZAM MAKE NA WAO HAWAKUANZIA JUU

- Ila unatakiwa kuwa mbunifu sana na kufanya watu wanunue bidhaa zako na si za wengine make wanaofanya hii business wako wengi so ni kwa nini wanunue kwako na si kwa wengine?
 
Watafute Hill Packaging, huyu jamaa mmiliki anaitwa Hillary ni mjasiriamali mzuri sana, ana kiwanda cha kutengeneza viroba kipo mapinga Bagamoyo mwanzo kabisa karibu na Bunju

Mkuu LAT hawa Jamaa wanafanya kazi ya Ku pack kwenye chupa pia? Nina mpango wa kuanzisha kiwanda cha juice na ninahitaji watu wa kunifanyia Packaging mkuu.
 
Mkuu LAT hawa Jamaa wanafanya kazi ya Ku pack kwenye chupa pia? Nina mpango wa kuanzisha kiwanda cha juice na ninahitaji watu wa kunifanyia Packaging mkuu.

Hapana, wao ni viroba tu.

Mkuu, kwanini usifanye sourcing ya mashine ya ku pack juice china, ukanunua pep bottles na kupack mwenyewe, very very convinient.
 
Asante mkuu nipo na dar na nimetafuta location maeneo ya kimara kwa ajil ya kufunga mashine but sijapata kampun ya uhakika ya kunitengenezea mifuko kwa ajil ya ku pack.
Ebwana, hongera sana, nami nilikuwa na wazo kama lako, vitu vingine utanishauri na vingine tutapata kwa wadau humu JF.

Mimi pia nataka niwe nakoboa na kusaga unga wa sembe, na nitafuga nguruwe, kuku wa kienyeji na ng'ombe kadhaa wa maziwa ambao nitakuwa nawapatia hizo pumba nitakazokuwa nazipata.

Naomba unisaidie kujua ni vitu gani ambavyo natakiwa niwe navyo na (estimated cost) ili nifanikishe ku-implement huo mradi.

Na je, naweza kuweka mashine ya kutumia mafuta badala ya umeme. Je, mashine zinazotumia solar zinapatikana? (Msinicheke jamani ktk swali hili)

Mtaji na soko siyo tatizo kwa sababu tayari nina reliable market ya ku-supply kg 150 kwa siku
 
Ebwana, hongera sana, nami nilikuwa na wazo kama lako, vitu vingine utanishauri na vingine tutapata kwa wadau humu JF.

Mimi pia nataka niwe nakoboa na kusaga unga wa sembe, na nitafuga nguruwe, kuku wa kienyeji na ng'ombe kadhaa wa maziwa ambao nitakuwa nawapatia hizo pumba nitakazokuwa nazipata.

Naomba unisaidie kujua ni vitu gani ambavyo natakiwa niwe navyo na (estimated cost) ili nifanikishe ku-implement huo mradi.

Na je, naweza kuweka mashine ya kutumia mafuta badala ya umeme. Je, mashine zinazotumia solar zinapatikana? (Msinicheke jamani ktk swali hili)

Mtaji na soko siyo tatizo kwa sababu tayari nina reliable market ya ku-supply kg 150 kwa siku

Mkuu, 150 kg ni viroba vitatu vya 50kg!
 
Mkuu, 150 kg ni viroba vitatu vya 50kg!!!!!!!!!!!!

Eeh mkuu, ni sawa na viroba 90 kwa mwezi (hapo sijachanganya zile za jumla kwa wale wenye viduka vidogo vidogo).

After all, hii ni shughuli ambayo nataka nimpatie ndugu yangu ambaye anazubaa zubaa mtaani, mimi nitakuwa natumia pumba kwa kulisha nguruwe nitakaowaweka.
 
Eeh mkuu, ni sawa na viroba 90 kwa mwezi (hapo sijachanganya zile za jumla kwa wale wenye viduka vidogo vidogo).
After all, hii ni shughuli ambayo nataka nimpatie ndugu yangu ambaye anazubaa zubaa mtaani, mimi nitakuwa natumia pumba kwa kulisha nguruwe nitakaowaweka.

Mkuu, unahitaji kuwa na supply ability kubwa kwani biashara hii ina demand kubwa. Kuna bwana mdogo mmoja hapa dar mwananyamala ana mashine ambapo anasaga unga wa sembe na kuuza takriban viroba 120 kila siku. Pumba anauza kwa jumla.

Jiandae mkuu hii project ni nzuri sana na siyo ya kumuachia mtu anaye zuba zubaa, itakupeleka mbali I promise you
 
Hellow wa jf na wazo la kuanzisha biashara ya kusaga unga wa sembe na ku pack kwa ajil ya kuuza, jaman naomben mawazo yenu .

Kwa ushauri wangu hilo eneo la kimara ungelifanya eneo la kusambazia yaani front office, na eneo ambapo malighafi zinapatikana ukaweka mitambo kwa ajili ya kupack hivyo vifurushi yaani back office.
 
Mkuu asante sana kwa ushaur wako nitaufanyia kaz soon then tutapeane updates, I hope mambo yataenda shwari.
 
Na je, naweza kuweka mashine ya kutumia mafuta badala ya umeme
Je, mashine zinazotumia solar zinapatikana? (Msinicheke jamani ktk swali hili)

- Unatakiwa uwe na machine nzuri sana ya kukoboa na kusaga (unaweza kusaga unga kwa mara ya pili ili kupata unga laini zaidi)
- Uwe na mahindi mazuri ambayo hayajaliwa na wadudu (lengo unga usiwe na harufu ya uozo)

- Sehemu nzuri ya kuhifadhi unga ili usiharibike (kusiwe na joto sana wala unyevunyevu), njia nzuri na rahisi ya kumaintain quality ya unga ni kuuanika juani baada ya kusaga kabla ya packaging (ukipigwa jua siku 3 au 4 utadumu muda mrefu sana)
- machine za mafuta zipo (kerosine) huwa zinatumika sana vijijini.

- Solar machine sijawahi kusikia & am sure haiwezekani c'se energy consumption ya machine ni kubwa sana, kupunguza consumption unatakiwa kusaga mahindi mengi bila kuzima zima machine

Challenge: Unahitaji watu waaminifu sana kusimamia machine yako na watu wa kuyasafisha mahindi vinginevyo utaibiwa vibaya sana
 
Safi mkuu n vizuri kama una wazo kama langu na unatakiwa uwe na mashine mbili moja ya kukoboa na nyingine ya kusaga, then mashine nzur yenye horse power 50 at least pia viroba ya ku pack unga +plus log na muonekano mzur wa packaging style, pia packaging machine, ma tank ya kuweka maji ya kutosha kwa ajil ya kusafisha yale mahind yawe saf pia itasaidia ata unga uwe saf, store saf .

Alafu mkuu me naona pia ku pack na unga wa dona coz kuna watu wengine hawapend sembe.n hayo mkuu mengine n marketing techniques ambayo hapa JF tumeshapata na tutaendelea kupata.

Thanks
 
Bila kusahau kuweka machine ktk location nzuri iliyo mbali na makazi ya watu. Lengo ni kuondoa matatizo na majirani ambao ni lazima watalalamia kuhusu kelele za machine yako, kusababisha nyufa kwenye nyumba zao na uchafuzi wa mazingira.
 
bila kusahau kuweka machine ktk location nzuri iliyo mbali na makazi ya watu. Lengo ni kuondoa matatizo na majirani ambao ni lazima watalalamia kuhusu kelele za machine yako, kusababisha nyufa kwenye nyumba zao na uchafuzi wa mazingira

Yap hiyo nayo wazo lingine mkuu much respect.
 
Back
Top Bottom