Red Brigade: Kikundi cha mauaji, watekaji, wamwagia sumu na "nchi kutotawalika"

Status
Not open for further replies.

Dr. Mwigulu Nchemba

JF-Expert Member
Feb 25, 2012
416
2,037
IFAHAMU RED BRIGADE YA CHADEMA,ILIPOANZIA,ALIYEILETA CHADEMA,MAFUNZO YA VIJANA WA CHADEMA NA KUBADIRIKA KWA BENDERA YA CHADEMA.

300px-Flag_of_the_Brigate_Rosse.svg.png


Watanzania wenzangu,

Ni dhahiri kumekuwa na mijadala kadha wa kadha kuhusu vyama vya siasa kuwa na vijana wao wa kuwa linda. Nilionesha tofauti baina ya red brigade na greenguard. Wanaojitetea wakakimbilia Dictionary bila kutumia muda kufuatilia historia na chimbuko la kikundi hicho ambacho jina , matendo na malengo yake yako sawasawa na kule kilikoanzia.

Lakini mjadala mkubwa ni kuhusu mpango wa CHADEMA kuanzisha jeshi lao la chama chao, Jeshi ambalo halihitaji msaada wa polisi wala wa Jeshi la wananchi wa Tanzania kwa mjibu wa kauli ya mkt wao mhe Mbowe.

Ni kinyume na katiba ya nchi na hata katiba ya chama chao (pitia katiba yao). Wanavunja katiba hiyo sio kwa bahati mbaya bali ni mpango wao unawabana wa kuhakikisha amani ya nchi inatoweka kama ambavyo .,Jeshi wanalotaka kulianzisha si bahati mbaya,ni mpango wa siku nyingi hasa ukifuatilia walikojifunzia ideology ya Red Brigade na aliyeileta CHADEMA.

images


MAANA HALISI YA RED BRIGADE NA WAANZILISHI WA HIYO TAASISI.

Red Brigade ilianzia ITALIA mwaka 1970 kwa kifupi ni BR,Wanzilishi wake anafahamika kwa jina la Renato Curcio na Margherita(mara) Cagol waliokutana kama wakiwa wanafunzi chuo kikuu cha Trento karibu na chuo alichokuwa akisoma Dr Slaa.

Red Brigade ni kikundi kilichokuwa kinajishughulisha na kuishambulia(kudhoofisha) serikali kwa kufanya mambo mbalimbali ya Mauaji,Kuteka na Kuua wanasiasa, Kuhujumu kazi za serikali, Kuiba mali za watu, Kupandikiza chuki kati ya wananchi na serikali yao na wananchi na vyombo vya dola na Kufanya nchi isitawalike (Rejea kauli ya Dr.slaa "NCHI HAITATAWALIKA"
Kikundi hiki kilikuwa kinatumia mwamvuli wa kuwa na uchungu na mali za umma lakini badala yake kikatumika , kuteka, kua na kumwagia sumu watu.

NOTE: Nazism ya Ujerumani chini ya Hitler ilijipambanua kama Socialist party(lakini matendo yake yalikuwa ni tofauti kabisa,Ugaidi na kuua ndio sifa yao).

Hiki kikundi kilivuma sana miaka ya 1970 hadi miaka ya 1980 (Hiki kipindi Dr.Slaa alikuwa Italia kwenye masomo na maisha yake yalikuwa huko). Red Brigade wakati huo walikuwa na kazi kubwa ya kuidhoofisha serikali iliyopo madarakani chini ya waziri mkuu Aldo Moro wakati huo.

Mwaka 1978 kilianzishwa kikundi kikubwa zaidi ndani ya RED BRIGADE(Ndio hicho chadema wanataka kukianzisha).Baada ya kuanzishwa kwa kikundi hicho kikiwa na watu 1000,kikundi hiki kilifanikiwa kumteka waziri mkuu Aldo Moro na kumuua Kinyama

Kuanzia mwaka 1974 hadi 1988 kikundi hiki kilifanya matukio ya kuteka, kuua,kumwagia sumu watu kwa matukio zaidi ya 50.Na yote haya yalilenga kufanya serikali ya Italy Isitawalike (DESTABALISE)..


images


KUKUA NA KUVUMA KWA RED BRIDGADE.

Matukio ya kuua na kuteka,kumwagia sumu na kuleta vurugu kila kona ya Itali kiliwafanya Red Brigade kusikika sana nakuleta hofu kwa watu.

Walikuwa wanaua na kuteka kwa USIRI mkubwa tena wakiwa wanatembea chini ya mwavuli wa chama cha kisiasa LOTTA CONTINUA na Potere Operaio.

Pia kilivuma sana kupitia Movement for Change MFC waliyoianzisha na baadaye kuipa jina la MOVIMENTO SOCIALE ITALIANO(MSI) bila shaka ndio M4C ya CHADEMA.

Ilikuwa ni miaka ya 1980 ambapo hiki kikundi kilizimwa kabisa kabisa na serikali.Serikali iliamua kuchukua hatua nzito kwa kuanzisha slogan ya ANTI-BR.

Yapo mengi sana ya kuelezea kuhusunia na kikundi hiki,(Pitia link hapa chini).

images


VIONGOZI WA RED BRIGADE WAKIMBIA ITALI.

Baada ya kusambaratisha Italia,RED BRIGADES wakakimbilia nchi zingine,Mfano Antonio Negri na Cesare baltisti walikimbilia France.

Wengine walikimbilia Palestina.

Takwimu zinaonesha zaidi ya watu 780 waliuawa na kumwagiwa sumu Italia chini ya BR,Lakini pia walifanya matukio zaidi ya 1400 ya uvunjifu wa amani na kuifanya Italia isitawalike.
Tafiti zinaonesha Red Brigade inaendelea kuishi kwenye nchi mbalimbali kupitia vyama vya siasa,Na moja wapo ni India,Tanzania(CHADEMA) Amerika kusini n.k

Pitia Link hii>>https://en.wikipedia.org/wiki/Red_Brigades na hii https://en.wikipedia.org/wiki/Red_Brigades.

ALIYEILETA CHADEMA KIKUNDI CHA RED BRIGADE NA MABADIRIKO YA BENDERA YA CHAMA.

images


Wakati wote haya ya RED BRIGADE yakiendela huko Italia,Kulikuwa na Mtanzania mwenzetu akiishi na kusoma huko (mambo ya kanisa),Ni katibu mkuu wa sasa wa CHADEMA Dr.slaa, Huyu ndiye aliyeleta falsafa ya kuanzishwa kwa kikundi hicho cha kihalifu chini ya mwavuli wa chama.

Historia inatuambia
Mwaka 1977 Dr Slaa alifanikiwa kupata upadirisho, Aliamua kujiendeleza kimasomo kwa kujiunga katika chuo kikuu cha Ponfical Urban Cha Roma cha huko Italia karibu na chuo walipokuwa wakisoma waanzilishi wa Red Brigade kipindi hicho Italy .

Alipokuwa Italia masomoni ndipo alipojifunza mbinu hizi za RED BRIGADE na hatimaye kuzileta CHADEMA.

Baada ya Dr.slaa kujiunga CHADEMA akaongoza ubadilishaji wa bendera ya chama (Bendera ya CHADEMA imebadilishwa na kuwekwa rangi nyekundu kama mwagaji damu Italy na aliyeasisi mabadiriko haya ni Dr.slaa akichukua sehemu ya bendera ya Red Bridgade wa Italy)na uundwaji wa katiba mpya ya chama yenye Red Bridgade(jina hili alilitoa Dr.slaa kwa kuiga lile la kikundi cha Italy) ndani.

Dr. Slaa alipojiunga CHADEMA amekuwa mstari ma mbele kutengeneza mahusiano na Italia ya kisiasa.

Kwa mara ya kwanza CHADEMA walipeleka vijana zaidi ya 50 kwenda masomoni Italia kujifunza mambo ya Red Bridgade kwa mwavuli wa mafunzo ya siasa na utawala.

lwakatare-case-april16-2013(1).jpg



RED BRIDGADE YA ITALIA(CHADEMA) NA KINACHOTOKEA NDANI YA NCHI YETU.

hqdefault.jpg


Ni wazi kabisa kabisa,Nchi yetu imekuwa ikikumbwa na mikasa ya uvunjifu wa Amani, kutekwa kwa watanzania wenzetu,Kuuawa kwa wananchi, Kutekwa na kuuawa kwa wanasiasa wenzetu kama ndago na mipango ya kuteka wandishi. Kubwa zaidi tumeshuhudiwa Kiongozi mkubwa wa chadema akisimama jukwaani na kujinasibu "NCHI HAITATAWALIKA"(DESTABALISE). Na kuwambia maaskofu wasiombee Amani

images


Ni ushuhuda ambao kila mtanzania anaweza kuusema, Mikutano inayoua ni ya chadema, Wanaoteka na kumwagia tindikali (sumu) ni vijana wa CHADEMA,Wanaojiita RED BRIDGADE ni CHADEMA,wanaoteka watu hao hao wanahusishwa ni CHADEMA, Chama maarufu kwa maandamano Afrika Mashariki na kati ni CHADEMA,Uvunjifu wa amani na matukio ya kigaidi yanatokea kwneye mkitano ya CHADEMA

Na hayo yote ni yale yale waliyokuwa wanayafanya RED BRIGADE wa Italia kuhakikisha serikali na chi haitawaliki.

images


Slogan ya MOVEMENT for Change na Peoples Power ni mwavuli tu ambao ulichukuliwa toka Magharibi kuwa ni wanademokrasia,Ili hali ni wanademogasia

313701_250604634977789_100000847625338_687930_911968435_n-560x373.jpg


Kwahiyo niseme wazi,mpango huu wanaotaka kuufanya chadema wa kuunda RB kubwa zaidi tena isiyohitaji msaada wa jeshi la polisi na Jeshi la Wa Tanzania, ni uhaini, ni ugaidi,ni maandalizi ya kupindua nchi au kuvuruga kabisa kabisa amani tuliyonayo. Kama wanavuruga amani na hii Redbrigade ndogo,itakuwaje wakiwa na jeshi.

lema_mjeshi1.jpg


Naunga mkono kauli ya Rais Mh.Jakaya kikwete hakuna kuundwa kwa jeshi hilo,na serikali itachukua hatua stahiki kuhakikisha nchi inafuata misingi ya katiba yake.

Hivyo basi,nawaomba watanzania tuamke, tusome nyakati kuhusiana na upinzani huu wa CHADEMA wenye mwavuli wa kisiasa kumbe ni kundi la RedBrigade wa Italy ni hatari kwa nchi yetu.

"KWA HABARI ZAIDI INGIA GOOGLE SEARCH RED BRIGADE"

====Majibu ya Dr. Slaa====
wanaJF,
Jitihada za Mwigulu kuhusianisha Red Brigade ya CHADEMA na Brigate Rosse ( neno la ki Italiano. Lenye maana ya Red Bigades) ni propaganda ya Kipuuzi. Red Brigade ( inaitwa brigedi Nyenyekundu) ya CHADEMA, ambayo ipo kwa mujibu wa Katiba ya Chadema na Kanuni zetu. Fasili na Ufafanuzi wa Brigedi Nyekundu ni "..Chombo cha ulinzi na usalama wa mali na maslahi ya Chama na viongozi"( Rejea Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama... kif. B " Fasili na Ufafanuzi". Wajibu wa kujilinda ni wa kila mtu na chama nacho kina wajibu wa kulinda Mali zake, wanachama wake na viongozi wake.

Aidha Mwigulu anazungumzia "Brigate Rosse". Ni dhahiri Mwigulu anafanya siasa ya maji Taka. Kwanza ni vema Mwigulu wajulishe wasomaji Kama neno hilo Lina maana ile ile ya "Red Brigade", na je Red Brigade ya CHADEMA in a fasili na Tafsiri ile ile ya CHADEMA? Kama ndivyo atuwekee Katiba ya Brigate Rosse hadharani ili wanaJF na GT wote wafanye uchambuzi wa kina na kuona Kama anachosema Mwigulu ni sahihi au ni Propaganda tu!

Ni kweli Dr. Slaa nimesoma Roma Italia toka 1979 hadi 1981. Hivyo siyo tu ninajua na kuzungumza Kiitalia, lakini pia ninafahamu Brigate Rosse ya Italia kwa kuwa miaka hiyo ndio kipindi kulikuwa na umafia na uhalifu mkubwa na kulikuwa na kesi denying dhidi ya Mafia. Katika Masomo yangu ya Sheria,kesi hizo Mara nyingi zimekuwa rejea ya Maprofesa. Hivyo ninaijua si kwa kuwa nimeishi katika utamaduni wa Italia wa wakati huo.

Hata hivyo, Ndio maana sikuzote, Sina sababu ya kujibu upuuzi wa Mwigulu. serikali iliyoko madarakani ni ya CCM. Kama ni kweli anayosema Mwigulu na anayaamini, Anashangaza sana. Dr. slas nimemaliza masomo yangu mwaka 1981. Tangu wakati huo sijarudi Roma isipokuwa kipindi nilipokuwa Katibu Mkuu wa TEC. Sasa Mwigulu anataka kusema TEC nayo ilikuwa inanzisha Brigate Rosse kwa kuwa Kama Katibu wajibu wangu ulikuwa kuunganisha Baraza letu na Nchi zingine duniani.kauli ya Mwigulu,unaweza kutolewa tu na mtoto wa darasa la pili.

Aidha, Kama Anachosema Mwigulu ni kweli anapaswa kukamatwa,kwani Kama Raia Mwema, toka mwaka 1981 Mwigulu alikuwa na Taarifa ya mtu aliyejifunza mbinu za Brigate Rosse, ambazo ni makundi ya uhalifu na Umafia na Mwigulu amekaa na Taarifa hizo za kihalifu na kwa kuwa kwa mujibu wa sheria za nchi yetu, mwenye kukaa na Taarifu za uhalifu na yeye ni mhalifu. Anapaswa akamatwe kwa ushiriki wake kwenye uhalifu huo. Katika Hali ya kawaida sina hakika Kama Mwigulu aliwahi kujifunza kitu kinachoitwa logic katika maisha yake. Kuelewa kuwa Kaulinzako zinajikanyaga huhitaji sana kwenda shule kubwa kubwa, unless mnatuambia Chuo Kikuu kilichompa Degree ni hovyo kiasi hicho. Kwa maana nyingine, Kama kweli Mwigulu ni Naibu Katibu Mkuu, Serikali aliyoko ni hiyo hiyo ya CCM toka miaka 1977, maana yake ni kuwa Serikali hiyo ambayo inamjua mhalifu muda wote tcoka 1981, inaibuka Leo na kauli tata hivi, wakati Katiba ya CHADEMA ipo kwa Msajili toka mwaka 2006 basi wakubali Serikali ya CCM imeshindwa kuongoza na ilipaswa kujiuzulu siku nyingi sana.

Nadhani nimejieleza ya kutosha. Nawaomba wasomaji wetu wapuuze upuuzi huu wa Mwigulu nchemba.


 
Mwigulu Nchemba ni wa kwanza katika watu nitakao waweku huku:
Miaka ya nyuma kwenye toleo la siku hizo la JF tulikuwa na kitufe cha "potezea" Kwangu mimi hiki kitufe kilikuwa msaada sana kutumia muda vizuri ninapotembelea JF maana niliweza kusoma michango ya wachangiaji wanaosaili na kaulimbiu ya JF. Wale walioandika upuuzi au kuchangia kwa kuleta mizaha niliwaweka kwenye "Ignore List" na sikupata kuona au kusoma upuuzi wao.

Hivi sasa kuna mafuriko ya ongezeko la socialtrapreneurs walioajiriwa na kambi hasimu humu ndani ya JF kwa kazi maalumu ya kutetea kambi zao na kuchafua za wengine. Wako kazini na ujira wao unahesabika kwa idadi ya mabandiko. Ili kuwa na hesabu kubwa wanaandika na kuchangia mijadala kwa style ya "If you can't convince, confuse them" Matokeo yake sasa hata mijadala yenye hoja za msingi inahamishwa kujadili upuuuzi na wapuuzi.

Ombi langu kwa Mods turejeshewe kitufe cha "Ignore" ili IDs zitakayopata ignore kama zaidi ya 100 zifungiwe ili kusafisha JF.

Asante
 
mbona wewe hujaeleza kundi lako la Green guard linafanya nin? nyani haöni kundule umekua ukileta propaganda kila uchwao lakn kumbuka ccm haitaongoza milele ipo cku itadondoka cjui utakimbilia wap mana umemwaga damu nying zisizo na hatian ila Mwigulu kumbuka what goes up must come down...we shall overcome!
 
kwa kweli wewe Mwigulu Nchemba ; nashindwa kujua uwezo wako wa kufikiri. Jana ulileta uzi wenye maudhui haya haya na picha hizi hizi; tulipoanza kukuuliza maswali ukakimbia kivuli chako. Sasa leo unadhani tushasahau, umeleta uzi kama ule ule ulichoongeza ni idadi ya picha na maelezo ya wikipedia. Maskini mwenzetu hujui hata kuwa wikipendia ni kama JF, ambapo yeyote aweza kuandika chochote.Hata hivyo unachofanya ni upotoshaji wa makusudi na kuanzia leo mimi natangaza kutochangia thread zako tena mpaka hapo utakapoamua kuwa muungwana na ukaacha kufanya upotoshaji wa makusudi hali unajua.



  • Ndugu zangu watanzania; Kama Red brigade ni kundi la kihalifu tena linalotumia silaha za moto na ndilo linaloendesha mauaji nchini, na lipo toka Dr.W.Slaa ,alivyojiunga na na CHADEMA na mauaji na utesejaji ndio kazi yake (kama anavyodai huyu kiongozi mwandamizi wa CCM), Ni kwa nini Kundi hili limeachwa likaendelea kuwepo nchini mpaka sasa licha ya kuwa limekuwa likifahamika kwa muda wote huo na muasisi wake amekuwa akifahamika fika kuwa ni Dr.W.Slaa? Kama Hili ndilo kundi linalotekeleza mauaji ya Kisiasa nchini (kwa mujibu wa kauli ya Mwigulu;kiongozi wa chama kinachoongoza serikali) JE! Kamanda Chagonja na Wenzake wako Arusha kuwasanifu Watanzania?

  • Ikitokea mwanafamilia anavamia wanafamilia wenzake, na kuwashambulia; Ni nani (chombo gani) anaepaswa kumkamata? .Jaalia CHADEMA wamekuwa na tabia ya kujishambulia wenyewe (Kama mnavyodai) na kule Arusha wamejishambulia wenyewe pia,(mwana familia kaamua kuwashambulia wanafamilia wenzake kwa sababu yeyote ile) ni nani alipaswa kumdhibiti? Je! aliepaswa kumdhibiti na hakumdhibiti ninyi mnamtafsiri je? Je; Mnadhani wanachadema walioshambuliwa (hata kama wameshambuliwa na mwanachedema mwenzao) hawapaswi kuchukua hatua?

Kama ni ninyi kwa mfano; Kuna Mtu anawavamieni ndani kwenu, anawashambulia na kuwaibia; na chombo kinachotakiwa kumdhibiti hakifanyi hivyo (kwa sababu zozote zile), mkikiuliza kinasema anayewavamia huwa ni mwanafamilia mwenzenu, ninyi mngechukua hatua gani? Mfano kama mkisema mtakuwa mnajificha nyuma ya mlango halafu mvamizi akifungua mlango tu mnamkamata; Halafu ikatokea chombo ambacho ndicho kilitakiwa kiwe kinamkamata (Japo hakifanyi hivyo) Kinaibuka na kusema "ole wenu muwe mnamvizia muhalifu nyuma ya mlango", (Huku kikisisitiza kuwa kitahakikisha kinawadhibiti kama mtachukua hatua ya kudhibiti uhalifu mnaofanyiwa), nyinyi mtakitafsiri vipi chombo hiki ? Je; Mnadhani wanaofanyiwa hivyo sasa nao wakijiwa na fikra/tafsiri inayokuja kichwani kwako sasa; watatakiwa kulaumiwa?
WENZETU WA CCM MNAJISIKIA JE?

1. Mnajisikiaje ikiwa mnashambuliwa (bila kujali mshambuliaji ni nani) kisha mshambuliaji hakamatwi halafu ukitaka kujilinda, alietakiwa kumkamata mhalifu (aliyeshambulia) anakukabili kwa nguvu zote?

2. Unajisikiaje siku umevamiwa ndani ya familia yako, ukashambuliwa, (mtoto wako mdogo akafariki kwa kupigwa) halafu ukaripoti kwa vyombo husika vikakuambia utakuwa umejishambulia mwenyewe ili upate misaada na huruma?Utajisikia je?

3.Utajisikia je siku ukiwa unaumwa pengine na malaria (Si unajua wanadamu tumeumbwa kwa nyama) halafu umelazwa muhimbili, Ghafla unasikia sauti ikikupa pole na kisha unafungua macho; mbele yako unamuona mtu asiye na meno ya mbele,anatembea anachehemea huku ana makovu mengi usoni.Mkononi kabeba sabuni na chupa ya uji. Kwa mbali unakumbuka ni miongoni mwa watu ambao wewe uliwatuma askari wampige na kumsababishia hali hiyo (eti tu kwa kuwa alikuwa na mawazo tofauti na yako) Unajisikia je? Hivi unajisikiaje?


4. Unajisikiaje unapotembea njiani, halafu ukakutana na watu; watu wanaojua kwamba kuna uhalifu unatokea hata kusababisha mauaji na wewe wakati wote hoja zako ambazo umekuwa ukizitoa zinakuwa za kuukadhamiza upande wa wahanga na kuwatetea upande wa wahalifu; Hivi unajisikia je? Unadhani wanaokuona na kukutizama nao wanajisikia je?

5. Unaonaje ukijikuta katia mazingira ambayo kuna watu watatu. Mmoja anahisi anaweza kudhuriwa (kwa kuwa alishawahi kudhuriwa mara kadhaa) na hivyo anafikiri kujilinda (defensive) na wa pili anataka kudhuru (offensive) Hivyo hataki wa kwanza ajilinde (ili asije akapata upinzani), Na huyu wa tatu yeye anapingana na wa kwanza na hivyo kuungana na huyu wa pili. Wewe utajisikia je? na utachukua upande gani hata kimoyo moyo tu?


Mambo haya kimsingi yanahitaji diplomasia kubwa sasa ya kisiasa kwa sasa (vinginevyo ni hatari sana) na hilo linawezekana tu, ikiwa kutakuwa na nia njema hasa kutoka kwa upande unaowatenda wenzao.Hata hivyo Kwa haya wanayoendelea kuyazusha viongozi wa CCM, kwenye vyombo vya habari badala ya kushughulikia tatizo la msingi, sioni kama wana nia njema katika hili.Ndugu zangu; Tunajenga vizazi vyenye mafundo ya chuki, hasira na roho za visasi; Hivi nani anajua vizuri saikolojia ya mtu anaedhani anadhulumiwa, anaonewa anakandamizwa na akijaribu kujitetea anazimwa kwa nguvu?

Hivi ninyi wenzetu wa CCM, kwa nini mnawafanyia wenzenu na mnapenda wenzenu wafanyiwe vile msivyovipenda kufanyiwa ninyi? Kwa nini mnapenda kuwa na vitu ambavyo hampendi wenzenu wawe navyo? Kwa nini mnapenda wenzenu wafanye vitu ambavyo ninyi hamfanyi na msingependa kufanya? Wakati fulani mnawasababisha watu wapate jazba na mimi naona jazba ishaanza kunivizia.Ngoja ni ache.....

Wenzetu wa CCM, kwa nini mnazusha mambo ambayo mnajua wazi kuwa ni uongo, uzushi na uchochezi na kuacha kushughulikia tatizo la msingi, huku wenzenu wamewapoteza wapendwa wao? Hakika huku ni kupoteza ubinadamu kwa ulafi wa madaraka.

Kilichobaki kwenu ni mungu kuwatamkia kauli moja tuu...

"Mene Mene tekeri na Perese!" Maana yake; Utawala wenu umepimwa na umeonakana na mapumgufu makubwa! Na kisha ukachunguzwa ukakutwa umepungua na tena umegawanjika!. Na sasa watapewa watu wengine na mtaishia kudhalilika! .

 
Last edited by a moderator:
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom