Lisilozungumzwa kupunguza ajali kubwa za barabarani; Double roads

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,574
46,149
Wiki hii zaidi ya takribani watu 20 wamepoteza maisha kwa mpigo katika ajali ya barabarani, hii imekuwa habari kubwa na kufika kwenye vyombo vingi vya habari kwa sababu watu hawa wamefariki kwa mpigo ila huwezi kukosa watu wengi kadhaa waliopoteza maisha kwenye ajali za barabarani hasa barabara kuu.

Matukio ya aina hii sio ya nadra nchini, watu wengi wamepoteza maisha kupata ulemavu kwa ajali za aina hii. Mengi yamefanywa na serikali ikiwemo kuweka speed limit za km 50, matuta, matrafiki wengi barabarani, operations za ukaguzi wa magari n.k .

Haya yote ni sawa ila ukweli ni kwamba barabara za single road ni changamoto kubwa sana kwa safari ndefu za mkoa kwa mikoa au wilaya kwa wilaya.

Kuna wakati gari ni lazima zifanye overtaking, kuna wakati lazima zikwepe muendesha bodaboda, mtembea kwa miguu au mifugo kwa ghafla. Kwenye barabara za single road haya yote hatari kwa sababu kosa au tatizo dogo litakolomfanya dereva atoke upande wake linaweza kuwenda kusababisha ajali kubwa kwa gari ambako liko upande wake sahihi.

Kwenye barabara za double road dereva anakuwa na nafasi kubwa ya kuweza kurekebesha makosa au kuhimili gari katika matukio ya ghafla bila kuleta madhara makubwa kwa abiria na magari mengine.

Pia mwendo wa km 50 kwa sasa kwenye safari ndefu unamchosha dereva na abiria kwa ujumla, ni vigumu sana kuuzingatia.

Serikali sasa inapaswa ije na mkakati wa kuzifanya barabara kuu zote za mikoani na wilayani double roads tena zenye kutenganishwa katikati kwa vizuizi vya blocks.
 
Hiyo ndiyo dawa pekee ya kuepusha ajali,hizi tochi za barabarani na traffic hazisaidii kitu serikali ingeharakisha miradi ya treni za umeme tuachane na mabus
 
Mawazo yako ni mazuri. Tatizo ni uwezo wa kifedha.
Kuna barabara nyingi za muhimu mfano za kuunganisha mikoa au wilaya. Hazipitiki mda wote wa mwaka.
Kwahiyo kipaumbele ni kufanya zipitike kwanza. Halafu wataendelea kuzipanua.
Mfano unao sasa hivi barabara ya chalinze ni njia nane. Uwezo ukipatikana zote zinaweza kuwa hivyo
 
Upo sahihi sana mkuu,ila kumbuka hii ni nchi ya dunia ya 3 kama wasemavyo wengi,yes rasilimali tunazo ila wananufaika wachache........ baadhi ya sehemu barabara ni nyembamba sana
 
Wakope tu pesa kama wanvyokopa kwa mambo mengine, watu wataendelea kusafiri safari ndefu wakiwa wameshikilia roho mkononi mpaka lini?? Maisha ya binadamu yana thamani kubwa kuliko chochote.
 
Ni kweli ,serikali inapenda kutupia lawama kwa mwendo kasi na ubovu wa vyombo vya moto ila ukweli ni miundo mbinu ndio mibovu, barabara moja haiwezi ikahudumia mtembea kwa miguu,maroli,daladala,mabasi ,magari binafsi,bodaboda, bajaji, baiskel,wanyama,punda na tera lake vyote hivyo pasikuwepo na ajali ni ngumu.
 
Naunga mkono hoja. Halafu katikati liwekwe tuta kubwa la kuzitenganisha hizo barabara (ikiwezekana ipandwe ile minazi ya urembo). Hakika ajali zitapungua kwa % kubwa.

Pia kuna vile vibao vya 50 kph! Navyo vingetazamwa kwa jicho la karibu, maana ndiyo vichaka vikuu vya kupokea rushwa kwa askari wetu wa usalama barabarani.
 
Back
Top Bottom