Ukwelinasema
JF-Expert Member
- Feb 10, 2021
- 364
- 380
Habari za asubuhi wakuu wote wa JF na hongereni kwa shughuli mbalimbali za kujenga taifa.
Kilichonileta kwenu asubuhi hii ni kunisaidia mawazo ya hili nalopitia kwa sasa, mimi na mwenza wangu tuna miaka mitatu sasa tunaishi pamoja na ni mwaka mmoja wa kuchumbiwa.
Kama mjuavyo, desturi zetu za Kiafrika baada ya mahari mnaulizwa tarehe ya Ndoa ndivyo ilivyokuwa na kwetu pia ila mwenzangu aliomba ajipange sababu hakuwa vizuri kwa kipindi hicho hivyo wazazi walimkubalia.
Sasa napata maswali mengi kutoka kwa wazazi na ndugu wakiniuliza ndoa lini mpaka nakosa majibu sababu nikimuuliza mwenzangu ananiambia nina haraka gani nisubiri.
Kilichonifanya nije kwenu ni kuomba ushauri je niko sahihi kuendelea kutumikia majukumu yangu ya ndoa kwa mgongo wa kuchumbiwa au nimechutama choo cha kiume?