Leo ndio nimejua kwanini waliotumbuliwa walikuwa wanazimia

mzee wa kasumba

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
1,432
2,892
NIMEPOTEZA KIBARUA

Binafsi sikuwa muajiriwa serikalini, lakini nilikuwa kibarua katika kampuni flani. Hii ni sehemu ambayo imenilea kwa muda mrefu kiasi kisichopungua miaka mitatu. Hii ndio sehemu ambayo nilikuwa naitegemea kwa asilimia kubwa kulisha familia yangu.

Wiki iliyopita kuna mambo hayakuwa sawa upande wangu kama mtunza stock. Kiukweli ni kwamba kuna tamaa tulipandikizana na afanyakazi wenzangu na baadhi ya mzigo tukauiba na kuuza. Lengo ni kupata pesa nyingi kwa mkupuo na kusahau kuwa kuna kitu kinaitwa KUUMBUKA.

Daaah, ebwana kama Muvi. Sijui bosi alipenyezewa za chini chini na nani aisee.. Mara akaibuka ghafla eneo la kazi. (Hua anaishi nje ya Mkoa tuliyopo)

Alipofika cha kwanza alitaka tuchukue stock yote. Kiukweli mapungufu makubwa yalionekana. Mtu wa kutakiwa kujibu maswali yale nilikuwa ni mimi, nami sikuwa na cha kuongea zaidi ya kuomba radhi na kuomba kukatwa katika mshahara wangu.

Pamoja na msamaha wangu wote lakini mwarabu yule hakutaka kunielewa na kuanzia muda alinitimua kama mbwa na kutaka nirudi nyumbani na ndio mwisho wa kazi.

SIKUAMINI MASIKIO YANGU WALA MACHO YANGU... Kwakweli nilichanganyikiwa sana sana.

Tangu hapo ndio nikawa nimepoteza kibarua changu na ni wiki ya pili sasa naishi kwa kuungaunga.

  • Familia inanitegemea (Mke, watoto na ndugu)
  • Tamaa zimeniponza
  • Sina pa kushika
  • Kichwa kimechanganyikiwa sana sielewi cha kufanya

Daaah najua nitalaumiwa lakini hiyo ndio hali iliyonikumba ndugu yenu.
Naomba msaada wa kimawazo, ushauri, kazi, kibarua au deiwaka.

Asanteni sana. Ni mimi ndugu yenu mzee wa kasumba zisizokuwa na madhara
 
Usiwaze mwamba, misala kama hiyo huwa ipo, kwakuwa limeshakukuta basi huna budi ukae chini ujitathmini.

Ukijibebesha iyo dhambi hakika hutopata kazi milele, tubu songa mbele.

Next time hakikisha kwenye kila unalofanya una back up plan, mfano hapo ilibidi usipige dili za sumu hadi pale una uhakika wa kipato cha nje chenye uwezo wa kuendesha familia zaidi ya miezi sita. Unaweza mfungulia mkeo biashara au ukafungua biashara yako ya nje.

Pili. Unaposuka ramani yoyote, hakikisha unajua pa kuingilia na pa kutokea, ungekuwa umejipanga kwa hayo, uyo bosi asingekutikisa, kwani ungekuwa na majibu.

Always improvise when necessary...Get away from X
 
hahahah pole sana mwamba ndio ukubwa huo..
when one door is closed 10 will open
Unamjaza tuu

One door ya nyoko

Maninaa..nikm upate ngoma kwa uzembe wako kisa dem ulimuona kajaza mbayaa mweupee, takooo,suraaa

Basi mdogodogo unapitia zile hatua za "Makasiriko""

Utasikia..." Sio mbaya, hata ivo demu mwenyewe alikua kisu sanaaa mzuriii"
 
Malipo ni duniani,,,ila pole kwa mkasa, inakubidi uishi kabla ya miaka hii mitatu wakati una kibarua.
 
Kula utakula na utalala.
Mungu analeta riziki kwa viumbe wake wote walio chini ya dari yako bila wewe kujua zinapotoka hadi utakapopata kazi. Amini hivyo
 
Usiwaze mwamba, misala kama hiyo huwa ipo, kwakuwa limeshakukuta basi huna budi ukae chini ujitathmini.

Ukijibebesha iyo dhambi hakika hutopata kazi milele, tubu songa mbele.

Next time hakikisha kwenye kila unalofanya una back up plan, mfano hapo ilibidi usipige dili za sumu hadi pale una uhakika wa kipato cha nje chenye uwezo wa kuendesha familia zaidi ya miezi sita. Unaweza mfungulia mkeo biashara au ukafungua biashara yako ya nje.

Pili. Unaposuka ramani yoyote, hakikisha unajua pa kuingilia na pa kutokea, ungekuwa umejipanga kwa hayo, uyo bosi asingekutikisa, kwani ungekuwa na majibu.

Always improvise when necessary...Get away from X
Daaah Asante mwamba kwa kunipa moyo
 
Similar Discussions

8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom