Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,308
- 45,614
Kazi ya Rais ni kutengeneza dira na sera za kitaifa kuhakikisha nchi inaenda katika muelekeo sahihi kiuchumi, kijamii na siasa.
Kwa mantiki hiyo Rais muda mwingi anatakiwa awe Ofisini kwake akipokea na akipitia ripoti za kiuchumi, kisiasa, kiusalama n.k huku kwa karibu akiangalia utendaji wa mawaziri wake na viongozi wengine anaowateua kama wanatimiza majukumu yao ipasavyo.
Rais hatakiwi kutembea kila mtaa na kijiji kuhakikisha mambo yanaenda. Kuonekana kwake katika umati kunatakiwa kuwa katika matukio ya kitaifa mfano sherehe za uhuru, muungano na mashuja, majanga makubwa na misiba ya kitaifa,uzinduzi wa miradi mikubwa.
Rais kwenda kukagua miradi sijui ya ujenzi,maji, barabara, zahanati,n.k kila mara na kila mahali ni matumizi mabaya chini ya kiwango cha ofisi ya Urais. Hizo ni kazi za mawaziri, manaibu wao, waziri mkuu, makamu wa Rais, wakurugenzi, makatibu wakuu, wakuu wa mikoa na wilaya.