Msaada: Nimepewa siku 30 niondoke nyumbani kwa Baba mkubwa

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,179
3,539
Wana JF wenzangu, nilikuwa nimepanga maeneo ya Kimara miaka kadhaa iliyopita. Kutokana na changamoto ya maisha, kazi nilikuwa sina nikaenda kuishi kwa bamkubwa ili nijipange upya.

Kwa sasa nimekaa miezi minne kwake leo asubuhi kaniambia “nimekupa siku 30 uondoke kwangu”.

Wakuu naombeni msaada wapi pakuanzia? Nifanye nini? Nianzie wapi?
 
Wana jf nilikuwa nimepanga maeneo ya kimara miaka kadhaa iliopita kutokana na changamoto ya maisha kazi nilikuwa sina nikaenda kuishi kwa bamkubwa ili nijipange upya akanikubalia kwa sasa nimekaa miezi minne kwake Leo asubuhi kaniambia nimekupa siku 30 uondoke kwangu wakuu naombeni msaada wapi pakuanzia nifanye nini nianzie wapi
Programmer unafeli wapi? Huna marafiki kwani?
 
Wana jf nilikuwa nimepanga maeneo ya kimara miaka kadhaa iliopita kutokana na changamoto ya maisha kazi nilikuwa sina nikaenda kuishi kwa bamkubwa ili nijipange upya akanikubalia kwa sasa nimekaa miezi minne kwake Leo asubuhi kaniambia nimekupa siku 30 uondoke kwangu wakuu naombeni msaada wapi pakuanzia nifanye nini nianzie wapi
Umejisaha sana mkuu
 
Acha kugombania nyama saa ya Kula na vitafunio vya chai asubuhi na watoto wake......atakuwa Tu kapata maelezo kutoka Kwa mama yako mkubwa.....akiwaekea cartoon akina junior kwenye DStv wewe unatoa na unasema unataka mpira kama huwa unalipia king'amuzi Chao.....
 
Wana jf nilikuwa nimepanga maeneo ya kimara miaka kadhaa iliopita kutokana na changamoto ya maisha kazi nilikuwa sina nikaenda kuishi kwa bamkubwa ili nijipange upya akanikubalia kwa sasa nimekaa miezi minne kwake Leo asubuhi kaniambia nimekupa siku 30 uondoke kwangu wakuu naombeni msaada wapi pakuanzia nifanye nini nianzie wapi
Bamkubwa naamini si mwendawazimu, tueleze jambo baya ulilolitenda na akashindwa kukurejesha kwenye mstari, inaeezekana ulikuwa na tabia ya kumchungulia dada wa kazi aogapo, au kudai chakula kabla wengine hawajafika.

Ninaamini ukiwa mkweli utapata ushauri na msaada mzuri.
 
Wana JF wenzangu, nilikuwa nimepanga maeneo ya Kimara miaka kadhaa iliyopita. Kutokana na changamoto ya maisha, kazi nilikuwa sina nikaenda kuishi kwa bamkubwa ili nijipange upya.

Kwa sasa nimekaa miezi minne kwake leo asubuhi kaniambia “nimekupa siku 30 uondoke kwangu”.

Wakuu naombeni msaada wapi pakuanzia? Nifanye nini? Nianzie wapi?
Nenda Ofisi za CUF Buguruni pale kuna room ipo wazi mwambie Magdalena Sikaya akupe moja.
 
Wana JF wenzangu, nilikuwa nimepanga maeneo ya Kimara miaka kadhaa iliyopita. Kutokana na changamoto ya maisha, kazi nilikuwa sina nikaenda kuishi kwa bamkubwa ili nijipange upya.

Kwa sasa nimekaa miezi minne kwake leo asubuhi kaniambia “nimekupa siku 30 uondoke kwangu”.

Wakuu naombeni msaada wapi pakuanzia? Nifanye nini? Nianzie wapi?
Mwaka fulani, nilipoteza kazi nikiwa sina chochote! Nyumbani kwetu kuna nyumba kubwa sana, na kwavile watoto wote ni wakubwa karibu, except huyu dogo, wana "kwao"! Hata huyu dogo bado yupo home kwavile, as a big brother, nilimwambia asitoke lakini uwezo wa kupanga anao! Ninachotaka kusema ni kwamba, ingawaje nyumba ni kubwa sana lakini ilikuwa inaishi baba, mama, mfanyakazi wa ndani, na huyu dogo huku chumba kimoja na sebule (uani) kukiwa hakuna mtu, na chumba kimoja wakaamua kuweka kuku kwavile na chenyewe kilikuwa hakina kitu! Aidha, kulikuwa na banda lingine kubwa la uani (upande mwingine wa nyumba) ambako walikuwa wanaishi wapangaji ambao ni MMOJA TU ndie alikuwa analipa kodi kwa wakati! Wengine wote walikuwa na sifa ya kutimuliwa!!!

Unaona jinsi ambavyo nilikuwa na "utajiri" wa makazi?! Lakini pamoja na yote hayo, nikagoma katakata kurudi home kwenye nyumba ya bure! Nilichofanya ni kuuza pikipiki yangu na kwenda kupanda sehemu iliyokuwa nafuu zaidi! Usidhani ilikuwa rahisi! Niliishi kwa shida SANA! Mlo mmoja ilikuwa kawaida! Nikipika chai, majani nilikuwa simwagi! Amini usiamini, sufuria ya chai ilibadilika rangi kutokana na kutoisafisha kwa hofu ya kumwaga majani! Mboga yangu ilikuwa maharage, na wala sikuwa na uhakika wa kuyapata! Niliachana na jiko la gesi na kuanza kutumia mafuta ya taa sababu ilikuwa ni rahisi kupata buku 2 ya mafuta ya taa kuliko 15K hadi 18K ya gesi! Si mara moja wala mara mbili kukaa na njaa lakini nikakomaa ingawaje wazazi wapo hai Dar, Sister wangu (hana mume) yupo hai Dar na ana nyumba yake, uncle wangu, yupo hai Dar na ana nyumba yake, Bro wangu akanipatia banda la uani pale kwake Charambe! Lakini kote huko NILIGOMA kwenda!

Leo sina cha kujivunia lakini naweza kulipa kodi ya mwaka mzima! Najua unajua huwezi kulipa kodi mwaka mzima wakati hauna uhakika wa kula!!!

Ninachotaka kusema ni kwamba, ONDOKA hapo unapotimuliwa! kapambane mtaani uingie akili! Huwezi kuwa kula kulala bure halafu ukapata akili ya ku-fight!!
 
Mwaka fulani, nilipoteza kazi nikiwa sina chochote! Nyumbani kwetu kuna nyumba kubwa sana, na kwavile watoto wote ni wakubwa (the youngest is now 26), karibu, except huyu dogo, wana "kwako"! Hata huyu dogo bado yupo home kwavile, as a big brother, nilimwambia asitoke lakini uwezo wa kupanga anao! Ninachotaka kusema ni kwamba, ingawaje nyumba ni kubwa sana lakini ilikuwa inaishi baba, mama, mfanyakazi wa ndani, na huyu dogo huku chumba kimoja na sebule (uani) kukiwa hakuna mtu, na chumba kimoja wakaamua kuweka kuku kwavile na chenyewe kilikuwa hakina kitu! Aidha, kulikuwa na banda lingine kubwa la uani (upande mwingine wa nyumba) ambako walikuwa wanaishi wapangaji ambao ni MMOJA TU ndie alikuwa analipa kodi kwa wakati! Wengine wote walikuwa na sifa ya kutimuliwa!!!

Nadhani atakuelewa
 
“Niliuza pikipiki”
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom