Je, Mungu kalipa kisogo taifa lake pendwa?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,784
Paliondokea ugonjwa wa ajabu unaopukutisha wana wa Mungu na wana wa shetani kwa kasi ya aina yake wala tiba haikuwahi kupatikana popote..watu wakafa sana na wa kufaana nao wakafaidika hasa

Katika nchi moja ya kufikitiks..taifa pendwa sana akaondokea nabii mbeba maono mtiwa mafuta kwa muhuri wa moto..akatoa ufunuo uliowapa ujasiri na uponyaji watu wake...akawaambia hakuna ugonjwa bali hofu ndio ugonjwa wenyewe ...watu wakaamini na ikawa hivyo..hata wale waliokufa ikasenekana ni hofu ndio ilitembea nao.

Kikapita kitambo maisha yakasonga na nabii mteule sana akasifiwa kwa umahiri wa kiimani, kwakuwa alitangaza maombi ya nguvu kwa siku kadhaa mpaka ugonjwa ukatoka baru.

Siku zimepinduka mpaka zikapindika kumetokea shida ya changamoto za kupumua katika taifa teule ..watu wanapukutika kwa kasi ya tano g.

Ewe nabii mteule wa Mungu mbeba maono makuu uko wapiii maombi yako wapiiii ni vilio kila kona. Mungu yule aliyekusikia kipindi kile yuko wapi asikie hata sasa!? Au kakupa kisogo? Kwanini?
 
Tuacheni HOFU na chuki za wachache wasiolitakia mema taifa letu, tuchape kazi huku tukimtanguliza Mungu. Ustawi wa nchi yetu kwa sasa uko thabiti kabisa. Pongezi zote JPM kwa maono na weledi wako katika uongozi na utawala bora. Kamwe usisikilize kelele za washamba, waoga, na walaghai kama hawa.
 
IMG-20210211-WA0162.jpg
 
hmmmmm sijui mpaka number zisome ngapi ndio atashtuka usingizini...au anajua current state sema PRIDE ndio inamfanya asionekane kwenye hili sakata?
Hivi eti ni kweli maiti zitatapakaa mpaka barabarani kwa mujibu wa wale wa wale watabiri wetu kule mbali sana?
 
Mwenyezi Mungu sio dhalimu Ukimtegemea Mr Mshana. Hili janga linakuzwatu. Na sio kweli kwamba watu wanaofariki sasa ni corona.

Napenda mjue kabla corona haijaja watu walikua wanakufatu. Ila tumeaminishwa na baadhi ya vibaraka wa waliotengeneza corona kwamba Tanzania watu walikua hawafi kabisa hivyo sasa hivi wanakufa kwa sababu ya corona.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom