Maisha ya ndoa anayo pitia ndugu yangu ni mateso, je amelogwa?

BILGERT

JF-Expert Member
Feb 27, 2015
6,535
10,974
Habari ya asubuhi wakuu.Naomba niende moja kwa moja kwenye mada husika.Mimi nina umri wa miaka 33 na mke wangu ana umri wa miaka 31.Ndoa yetu ina muda wa miaka mitatu sasa ingawa bado hatujabahatika kupata mtoto.

Mimi na mke wangu,wote ni watumishi katika idara ya elimu ambapo mke wangu yupo msingi na mimi nipo sekondari.Yeye ana miaka 10 kazini (2010-2020) na mimi nina miaka 5 kazini (2015-2020)

Turudi nyuma kidogo,Kabla sijafahamiana na mke wangu nilikuwa na maisha yangu tu ya kawaida..ambapo kwa mshahara wangu nilikuwa namudu maisha yangu, nilikuwa nimepanga.

Mwaka 2016 niliweza kukutana na mwenzangu,tulifahamiana na hatimaye tukaanzisha mahusiano.Tuliweza kudumu kwa takribani mwaka mmoja. Mwaka 2017 tulifikia maamuzi ya kufunga pingu za maisha (NDOA).

Niligharamia harusi kwa asilimia 80,ni kipindi ambacho ilinilazimu kuingia kwenye mikopo mirefu,Maana yeye pia nilimkuta ana mkopo. Nilichukua mkopo wa muda wa miaka 7, kiasi cha pesa kiliweza kutumika kwa ajili ya send off na kiasi kingine kwa ajili ya harusi na pia kiasi kingine cha pesa niliweza kuanzisha biashara kadhaa ambazo pia hazikufanya vizuri maana niliishia kupata hasara.Nilikuwa napata take home ambayo kiukweli ilikuwa haitoshelezi mahitaji muhimu.

Mke wangu nilimkuta anaishi nyumba za serikali (KOTA) ambapo ni chumba na sebule.Ameishi hapo tangu alipo ajiriwa mnamo mwaka 2010.

Baada ya harusi mke wangu alinishawishi nihame nilipo kuwa naishi ili niende anapo ishi yeye (KOTA) ili niweze kusave pia gharama za kupanga. Nilikataa sana kufanya hivo lakini aliweza kulazimisha.

Nilikubaliana na uamuzi wa mke wangu,niliweza kuhamia anapo ishi yeye na hatimaye tuliunganisha vitu vyetu,sebule ikaenea vitu kiasi kwamba vingine vilikosa sehemu ya kukaa.Shule anayo fundisha mke wangu na ninapo fundisha mimi ni jirani saana (Takribani mita 100)

Tatizo linaanzia hapa wakuu,ndoa yetu ilikuwa ya furaha saana kwa kipindi cha mwaka mmoja tu.Kuanzia mwaka 2019 mwishoni mke wangu alionyesha mabadiliko makubwa saana.Alianza dharau,majivuno na kashfa..Akiwa anasema kuwa mimi naishi kwake hivyo natakiwa niondoke.

Wakuu ni maumivu makubwa mnoo,ilifikia hatua akawa hataki hata kupika wala kufua nguo zangu na anarudi nyakati anazo zijua yeye mimi nikiwa nimelala.

Ukimuuliza ni ugomvi mwanzo mwisho,ni maisha magumu sana ambayo ninapitia.Mwaka huu mwezi wa tatu bodi ya mikopo ikawa imeanza kunikata pesa yao,maana nilikuwa nimesahaulika kwa kipindi kirefu.Hivyo maumivu yakawa mara dufu,maana kwa sasa pesa inayo ingia ni 140,000/=

Baada ya kumjulisha mke wangu juu ya hilo,akazidi kunidharau na ugomvi ukawa mzito.Msimamo wake ukiwa ni ule ule kuwa nichukue vitu vyangu nimuache.Amesahau kuwa mkopo wangu pia uligharamia harusi pamoja na send off.

Nipo njia panda wakuu,najaribu kuwaza naenda kuanza vipi maisha kwa huu mshahara wangu? Nitalipia vipi kodi na hasa nikiangalia mkopo wangu ndo kwanza nimekatwa miaka miwili bado kama miaka mitano,je ntatoboa?

Saivi hali ni mbaya Zaidi,maana amenifukuza chumbani..hivyo ninalala sebuleni kwa takribani miezi mitano sasa. Ndugu,wasimamizi wa ndoa pamoja na paroko wamejaribu kutusuluhisha lakini mwenzangu ameshikilia msimamo ule ule kuwa niondoke.

Niko frustrated mnoo, kuna wakati nashindwa kutimiza majukumu yangu ya kazi vile ipasavyo.

Baadhi ya ndugu wamenishauri niondoke nikaanze maisha,ukizingatia hatuna mtoto wala mali zozote tulizo chuma pamoja,isipo kuwa tuna kiwanja pekee. lakini kila nikitafakari naona sitoweza kusimama kwa huu mshahara wangu mdogo hasa kumudu gharama za maisha.

Naombeni ushauri wenu wadau,nifanye nini katika hii hali ninayo pitia? Maana kiukweli hatuna future yoyote na ninahisi nitakufa kabla ya siku zangu.Nimejaribu kuandika kwa kifupi,lakini mambo ninayo pitia ni mengi mnoo.

HAYA NI MAISHA HALISI ANAYO PITIA NDUGU YANGU WA KARIBU SANA.WANAFAMILIA HATUJUI TUNAMSAIDIA VIPI MAANA HATAKI KABISA KUONDOKA KWA HUYO MWANAMKE MBALI NA MAUMIVU NA MATESO ANAYO PITIA.KUNA MUDA TUNAWAZA ,JE AMELOGWA NA HUYO MWANAMKE? TUMEMSHAURI IMESHINDIKANA.NINI KIFANYIKE?
 
Mwanaume anaogopaje kuanza sifuri?
hajachoka huyo,siku akiwa taabani karibu na kufa ataondoka na kandambili tuu..ila jamani kuna wanawake waajabu hata shetani nahisi anashangaa,.khaa!!! hali hiyo wanaishi kwa KOTA,ingekuwa kwenye bonge la jumba lenye kila kitu??
 
Akufukuzaye hakwambii toka ila huyo mpaka kafikia hatua ya kukwambia toka na chumbani kakutimua sijui asichokielewa hapo ni nini? Mzee amka uondoke hapo tena mwisho wa mwezi huu amka sepa kabla hela hazijaisha.

140,000tsh inatosha ukiishi maisha ya kipato chako, tafuta single room ya 50/40 mdogo mdogo anza mwisho utakuja kusimama vizuri. Tafuta rafiki/ ndugu unayemuamini akuboost hata 200K kwa ajili ya kuweka vitu vya msingi ghetto.

Pole yake, nimecomment kama nakwambia wewe vile thoe title inasema ni ndugu yako.
 
Mwanamke akuambie ukaishi kwake nawe unaenda!! Labda kwa siku 2 tatu lkn sio mazima.. hao ndio viumbe ninaowapenda Sana lkn siwaamini!!.. hii sentensi nitaendelea kuirudia mpk mtaelewa tu.. wanawake nawapenda Sana ila siwaamini.
Hahaha,jamaa alitegemea watasevu hela mkuu.Maana Ni kikota cha serikali.Na mwanamke ndo alokabidhiwa.
 
Turudi nyuma kidogo,Kabla sijafahamiana na mke wangu nilikuwa na maisha yangu tu ya kawaida..ambapo kwa mshahara wangu nilikuwa namudu maisha yangu..nilikuwa nimepanga.
Niligharamia harusi kwa asilimia 80,ni kipindi ambacho ilinilazimu kuingia kwenye mikopo mirefu,
Hivyo maumivu yakawa mara dufu,maana kwa sasa pesa inayo ingia ni 140,000/=

Baada ya kumjulisha mke wangu juu ya hilo,akazidi kunidharau na ugomvi ukawa mzito.Msimamo wake ukiwa ni ule ule kuwa nichukue vitu vyangu nimuache.Amesahau kuwa mkopo wangu pia uligharamia harusi pamoja na send off.

Nipo njia panda wakuu,najaribu kuwaza naenda kuanza vipi maisha kwa huu mshahara wangu? Nitalipia vipi kodi na hasa nikiangalia mkopo wangu ndo kwanza nimekatwa miaka miwili bado kama miaka mitano,je ntatoboa?


Saivi hali ni mbaya Zaidi,maana amenifukuza chumbani..hivyo ninalala sebuleni kwa takribani miezi mitano sasa. Ndugu,wasimamizi wa ndoa pamoja na paroko wamejaribu kutusuluhisha lakini mwenzangu ameshikilia msimamo ule ule kuwa niondoke.

akini kila nikitafakari naona sitoweza kusimama kwa huu mshahara wangu mdogo hasa kumudu gharama za maisha.

Naombeni ushauri wenu wadau,nifanye nini katika hii hali ninayo pitia?
Dah......tatizo liko wazi kabisa kutokana na hayo maneno hapo juu tu....ni PESA....ushauri wangu kwako Dogo ni simpo sana.......
Kama unapenda mkeo…...na yeye ndiyo furaha yako...na ndivyo inavyoonekana ..basi .. kaa utulie ufikirie namna ya kutafuta PESA...tena tafuta pesa ya maana...ikiwezekana hata ufe wakati ukijaribu kuzitafuta......
Kama haumpendi...basi piga chini huyo mke...Kisha omba sana kwa mola wako akujalie umpate atakayeweza ishi nawe kwa 140,000 kwa mwezi🤣….full stop 🤭
 
Hahaha,jamaa alitegemea watasevu hela mkuu.Maana Ni kikota cha serikali.Na mwanamke ndo alokabidhiwa.
Jamaa yupo kwenye hizi traps.. financial traps, woman traps na ushamba traps!!.. akitoka kwenye hizo traps hatakuja kujuta.

Ushamba ninaouzungumzia sio ushamba wa kawaida ila ni ile kushindwa kuangalia vitu kiundani zaidi!
 
Back
Top Bottom