Kadiri unavyoukimbia mwangwi ndivyo unavyoukaribia

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,751
Utotoni tulifurahia sana tulipokuwa tunaenda mapangoni kusikiliza sauti zetu kupitia mwangwi mapangoni. Yaani Ilikuwa ni kama vile mapango yanatugeza sauti zetu na kutusikilizisha kwa sauti ya juu zaidi.

Siku hizi mapango yamepungua sana na mwangwi hakuna tena. Kuna wengine hapa wanaweza hata kushangaa mwangwi ni nini.

Tulienjoy sana tulipokuwa tukipiga ukunga wa uuuuuuuuuu. Na tunapoishia tu mwangwi nao unakupokea uuuuuuuuuu uuuuuuuuu. Mwangwi unaanzia mbaali unakuja karibu kabisa halafu unaishia hukooo unatokomomea kabisa.

Kuna mwangwi wa kifo ujue. Kadiri unavyoukimbia ndio unavyozidi kuukaribia Mwangwi asili yake ni wewe mwenyewe. Kuukimbia ni kujikimbia. Mwisho watu wataanza kukushangaa. Huyu anakimbia nini?

Unaweza kutoka kwako kwa hofu tu na kero ya mwangwi ukaenda kwa jirani ili usiusikie. Ukifika hapo unaukuta. Unaona hapa hapafai unaondoka tena unaenda nje ya mji upo. Unaona kero tena. Unahama mji bado mwangwi upo. Unaamua kwenda mbali.. Mwisho unamaliza miji na kuamua kuingia mwituni. Mwangwi haukimbiwi. Unaweza kuingia mwituni na usirudi. Mwituni kuna mengi.

Wataalamu wa madawa wanaweza kutusaidia kwenye hili. Ukitumia madawa makali kwa muda mrefu huleta athari kwenye mfumo wa fahamu. Mfumo wa fahamu ukiathirika huweza kuathiri hata uwezo wa mtu kwenye maamuzi hasa yale muhimu.

Tumejaaliwa kuwa na mgonjwa ghali zaidi duniani. Ambaye anaweza kuingia kwenye Guinness Book of Records. Lakini kwa anayofanya sasa nadhani anatafuta rekodi nyingine.

Halafu nimepita mahali watu wanapongezana. Huyu anasema kama sio mimi kusema hivi. Hali ingekuwa vile. Halafu yule mwingine anamshukuru. Mmoja ni mkubwa kuliko mwingine. Wanapongezana kuficha ukweli.

Tabia ya uvundo hauvundi mpaka unuke sana. Na kadiri unavyoufutika mchagoni ndio kadiri unavyotoa harufu kali. Ni kama pembe la ng'ombe -- HALIFICHIKI!

Jr
 
Back
Top Bottom