Baba nifundishe kuukabili uhalisia.. Nisiukimbie ukweli

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,791
Professor Kabudi kanywaje dawa isiyothibitishwa,?
Poleni watanzania... Poleni sana wananchi wanyonge wa mwili imara wa roho na thabiti wa ufahamu
Dawa ya Corona iliyofuatwa haraka haraka kwa ndege maalum ya mkuu wa nchi haiwezi kutumika hadi baada ya utafiti utakaochukua takriban siku 180.. Hii sio dawa ya maabara ni dawa ya asili.. Tuwe watulivu tutajulishana aina ya kipimo kitakachotumika kuthibitishwa ubora wake na kama haina side effects.. Hapa TBS na TMDA (TFDA) pengine hazirahusika...

Prof Kabudi anatuchanganya.. Tena sana.. Kwanini sasa asingeagiza kiasi kidogo kwanza kwa ajili ya sampling na kuthibitishwa ndio tutume lidege letu kuleta mzigo wa kutosha?

Nadhani muda utasema lakini naona kuna jambo si la kawaida sana hapa.. Kuna mkanganyiko mkubwa kwenye hili.. Kimamlaka na maamuzi.. Kuna hofu ya wazi pengine hiyo dawa ina madhara makubwa kiafya ama la haina uwezo wa kutibu Corona

Ni muhimu pia kujikumbusha alichosema Waziri wa afya huko inakotoka dawa.. Yeye alisema ile dawa ni kwa ajili ya kinga na si kwa ajili ya tiba kwa waliokwisha ambukizwa.. Ila ndio hivyo tena tumeshaulipia mzigo ambao hatutautumia hadi siku 180 zipite.

Baba nifundishe kuukabili uhalisia nisiukimbie ukweli.. Wahenga walituasa: kwa mwoga kulienda kicheko kwa shujaa kulienda kilio.

Hofu ni adui number moja kwenye kuukimbia ukweli.. Lakini hofu ni silaha number moja kwenye kuukabili uhalisia... Hofu na mashaka huleta mbinu na tahadhari. Ujasiri huleta majigambo na kutojali

Tusitoane hofu katikati ya hatari kubwa.. Tusifiche uhalisia kwa kufutika uvundo kibindoni.. Tuambiane ukweli.. Tutaokoa maisha mengi

Tukiwatoa watu hofu huku sisi tumefichama tunatengeneza tatizo kubwa zaidi.. Wananchi wanakuwa sio makini tena na tahadhari inakuwa ndogo.

Tumepigwa tena kwenye dawa isiyothibitishwa na ambayo hatutaweza kuitumia kwa miezi sita

Mungu wabariki waja wako.. Na watesi wa wana wako... Wabariki pia

Jr
 
Professor Kabudi kanywaje dawa isiyothibitishwa,?
Poleni watanzania... Poleni sana wananchi wanyonge wa mwili imara wa roho na thabiti wa ufahamu
Dawa ya Corona iliyofuatwa haraka haraka kwa ndege maalum ya mkuu wa nchi haiwezi kutumika hadi baada ya utafiti utakaochukua takriban siku 180.. Hii sio dawa ya maabara ni dawa ya asili.. Tuwe watulivu tutajulishana aina ya kipimo kitakachotumika kuthibitishwa ubora wake na kama haina side effects.. Hapa TBS na TMDA (TFDA) pengine hazirahusika...

Prof Kabudi anatuchanganya.. Tena sana.. Kwanini sasa asingeagiza kiasi kidogo kwanza kwa ajili ya sampling na kuthibitishwa ndio tutume lidege letu kuleta mzigo wa kutosha?

Nadhani muda utasema lakini naona kuna jambo si la kawaida sana hapa.. Kuna mkanganyiko mkubwa kwenye hili.. Kimamlaka na maamuzi.. Kuna hofu ya wazi pengine hiyo dawa ina madhara makubwa kiafya ama la haina uwezo wa kutibu Corona
Ni muhimu pia kujikumbusha alichosema Waziri wa afya huko inakotoka dawa.. Yeye alisema ile dawa ni kwa ajili ya kinga na si kwa ajili ya tiba kwa waliokwisha ambukizwa.. Ila ndio hivyo tena tumeshaulipia mzigo ambao hatutautumia hadi siku 180 zipite..
Baba nifundishe kuukabili uhalisia nisiukimbie ukweli.. Wahenga walituasa: kwa mwoga kulienda kicheko kwa shujaa kulienda kilio...
Hofu ni adui number moja kwenye kuukimbia ukweli.. Lakini hofu ni silaha number moja kwenye kuukabili uhalisia... Hofu na mashaka huleta mbinu na tahadhari. Ujasiri huleta majigambo na kutojali
Tusitoane hofu katikati ya hatari kubwa.. Tusifiche uhalisia kwa kufutika uvundo kibindoni.. Tuambiane ukweli.. Tutaokoa maisha mengi
Tukiwatoa watu hofu huku sisi tumefichama tunatengeneza tatizo kubwa zaidi.. Wananchi wanakuwa sio makini tena na tahadhari inakuwa ndogo..
Tumepigwa tena kwenye dawa isiyothibitishwa na ambayo hatutaweza kuitumia kwa miezi sita
Mungu wabariki waja wako.. Na watesi wa wana wako... Wabariki pia

Jr
Tumekwisha ila taifa hili lipo imara sana kuna viumbe nyuma yakiti wananguvu kuliko mwenye kiti.... Keep cool
 
itachunguzwa uku viongozi wakiendelea kunywa mi nadhani chato ishafika siku ileile mda sio mrefu mkuu ataingia DSM
Baada ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Paramagamba Kabudi kwenda Madagascar kuichukua dawa ya mititishamba inayoaminiwa kuwa inaweza kukinga na kutibu Covid-19, Tanzania imesema dawa hiyo itachunguzwa zaidi.

Akielezea kuhusu ''dawa'' hiyo leo. Mkuu wa Taasisi ya utafiti wa magonjwa ya binadamu (NIMR) chini humo Profesa Yunus Mgaya amesema kuwa dawa hiyo itafanyiwa uchunguzi wa kikemiana wa kibaiolojia kubaini utendaji wake.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Paramagamba Kabudi ambaye alikwenda madagascar kuchukua dawa hiyo amesema:''Hatujachukua dawa kutoka kwa sangoma'' na kuongeza kuwa:''Nilikwenda Madagascar kwa ndege ya rais kupokea zawadi kutoka nchini Madagascar ''

Rais Magufuli aliniruhusu niende na wataalam, na tulipofika kule walikua na mkutano wa saa nne wa kuzungumza na wenzao kuhusiana na dawa hii '', amesema Profesa Kabudi.

Alipokua akipokea dawa ya mitishamba iliyotolewa na Madagascar kwaTanzania Ijumaa , alisema kuwa Tanzania haijalegalega katika mapambano dhidi ya ugonjwa wa Covid-19.

Waziri wa mambo ya nje Prof. Palamagamba Kabudi anasema dawa hizo ni kwa ajili ya Utafiti, na sio za kugawanywa kwa Watanzania.

'' Dawa zimekuja chupa mbili kwa ajili ya utafiti na kuna fomula ambazo zimetolewa kwa wataalamu wetu'', amesema Profesa Kabudi na kuongeza kuwa Vilevile kuna box kwa ajili ya raia wa Madagascar ambao wamepewa zawadi kutoka kwa ndugu zao huko Madagascar.

Sera ya Tanzania kuzingatiwa

Mkemia mkuu wa serikali anasema Dkt. Fidelice Makumiko amesema : ''Dawa hizi ni msaada, na hawawezi kukataa kitu ambacho wamepewa...dawa hii tumeipokea kama msaada na sio kwa ajili ya kugawa kwa wananchi ... dawa hii tumeipokea kama zawadi kwa ajili ya kufanya utafiti wakatuonyesha kuwa ni salama na haina madhara kwa wananchi wao''

''Sera ya Tanzania ilivyo lazima kuipima na kuangalia ubora wa hii dawa na kuona kuwa ina usalama unaohitajiwa. Tumepanga kuwa na makundi matatu ya wagonjwa kwa hiari yao'', amesisitiza Dkt. Fidelice Makumiko.

Akipokea msaada huo Jumamosi, Prof. Palamagamba John Kabudi alisema ''Madai yanayotolewa kuwa Tanzania imelegalega ama kujitenga katika kupambana na ugonjwa wa COVID -19 si ya kweli kwa kuwa Tanzania imetoa uongozi madhubuti katika eneo iliyopewa dhamana ya uongozi ya Uenyekiti wa nchi SADC na imeifanya na inaendelea kuifanya kwa heshima na bidii zote.'',

Bwana Kabudi aliongeza kuwa Tanzania imetoa uongozi madhubuti katika kuratibu na kuunda timu ya wataalamu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika SADC kuandaa muongozo na utaratibu wa kukabiliana na ugonjwa huo ikiwa ni pamoja na kutafuta njia za kupunguza nguvu ama kuleta tiba ya COVID - 19.

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Madagascar Tehindrazanarivelo Djacoba As Oliva alizitaka nchi za Afrika kuungana kwa pamoja kupata suluhisho la maradhi ya COVID 19 ambayo pia itakuwa suluhisho na faraja kwa dunia nzima, imesema taarifa ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki nchini Tanzania.

Jr
 
Mkemia mkuu wa serikali anasema Dkt. Fidelice Makumiko amesema : ''Dawa hizi ni msaada, na hawawezi kukataa kitu ambacho wamepewa...dawa hii tumeipokea kama msaada na sio kwa ajili ya kugawa kwa wananchi ... dawa hii tumeipokea kama zawadi kwa ajili ya kufanya utafiti wakatuonyesha kuwa ni salama na haina madhara kwa wananchi wao''
732c987ba1181878ab8bbe3a7fcc3282.jpg
_112207667_whatsappimage2020-05-08at15.12.55.jpg

Jr
Prof kanywa sample ya utafiti
 
Mkemia mkuu wa serikali anasema Dkt. Fidelice Makumiko amesema : ''Dawa hizi ni msaada, na hawawezi kukataa kitu ambacho wamepewa...dawa hii tumeipokea kama msaada na sio kwa ajili ya kugawa kwa wananchi ... dawa hii tumeipokea kama zawadi kwa ajili ya kufanya utafiti wakatuonyesha kuwa ni salama na haina madhara kwa wananchi wao''View attachment 1445485View attachment 1445487

Jr
Prof kanywa sample ya utafiti
Jr

Prof kanywa sample ya utafiti
Kama mzima asiye na corona amekunywa sample basi inafaa kuwapa wagonjwa nawao wakanywa ili iwe ni moja tafiti zao
 
Mshana Jr kila mara tunakaribiana sana kimawazo sema wewe una uwezo mkubwa wa kiuchambuzi.

Kwanza kuna dege lilituletea vyombo vya maabara ya hilo gonjwa kutoka china, nilisema hakuna binadamu aliyepotezs raia wake vile akupende wewe ili usife lazima ajitahidi kubalance hesabu zake ufe kama tulivyokufa.

Sawa vifaa vimepokelewa matokeo yake hata matunda yana korona, huku shamba mapapai tumeachia ndege hatuli tena.

Imefikia wameenda kubeba midawa ya miti shamba, miti huku tz ipo kibao huku hakuna tofauti na bustani ya Mungu, ila hawaikubali wanaona haifai, wanatoa gharama kuchukua miti shamba ya nchi ya mbali.

Bila shaka serikali iliweka oda ya hayo mabokisi yaliyoonekana pale, ok sawa, na haikutosha waomi wetu na wataalam wamefika huko ughaibuni wakapewa dawa ndani ya glass pasi na shaka wakanywa na picha wakaturushia wakisema mkome nyie huko tz sie huku dawa tunakunywa.

Sawa, nani aliwaambia hicho walichokunywa ndicho walichobeba, walikuwa na haraka gani kuibugia ile dawa.

Hawakumbuki ile ya mwalimu (R.I.P) ya kubadili glass, wao walipewa mkononi kiasi kwamba you are targeted, hapo maprofesa mlituangusha vibaya sana.

Hawasomi hata vitabu vitakatifu kuwa Mwana wa Mungu alijaribiwa na mikate akiwa ndani ya mfungo wa siku 40?.

Sawa, dada wa afya alisema maabara inaoshwa kwa maana wanaanza kazi ya kupima hiyo miti shamba, sawa je, hao watoa miti shamba walijipangaje na wale watoa vyombo vya maabara.

Nina mambo mengi ninayoyaana yakitokea huko mbele.

Muda utaongea tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Professor Kabudi kanywaje dawa isiyothibitishwa,?
Poleni watanzania... Poleni sana wananchi wanyonge wa mwili imara wa roho na thabiti wa ufahamu
Dawa ya Corona iliyofuatwa haraka haraka kwa ndege maalum ya mkuu wa nchi haiwezi kutumika hadi baada ya utafiti utakaochukua takriban siku 180.. Hii sio dawa ya maabara ni dawa ya asili.. Tuwe watulivu tutajulishana aina ya kipimo kitakachotumika kuthibitishwa ubora wake na kama haina side effects.. Hapa TBS na TMDA (TFDA) pengine hazirahusika...

Prof Kabudi anatuchanganya.. Tena sana.. Kwanini sasa asingeagiza kiasi kidogo kwanza kwa ajili ya sampling na kuthibitishwa ndio tutume lidege letu kuleta mzigo wa kutosha?

Nadhani muda utasema lakini naona kuna jambo si la kawaida sana hapa.. Kuna mkanganyiko mkubwa kwenye hili.. Kimamlaka na maamuzi.. Kuna hofu ya wazi pengine hiyo dawa ina madhara makubwa kiafya ama la haina uwezo wa kutibu Corona
Ni muhimu pia kujikumbusha alichosema Waziri wa afya huko inakotoka dawa.. Yeye alisema ile dawa ni kwa ajili ya kinga na si kwa ajili ya tiba kwa waliokwisha ambukizwa.. Ila ndio hivyo tena tumeshaulipia mzigo ambao hatutautumia hadi siku 180 zipite..
Baba nifundishe kuukabili uhalisia nisiukimbie ukweli.. Wahenga walituasa: kwa mwoga kulienda kicheko kwa shujaa kulienda kilio...
Hofu ni adui number moja kwenye kuukimbia ukweli.. Lakini hofu ni silaha number moja kwenye kuukabili uhalisia... Hofu na mashaka huleta mbinu na tahadhari. Ujasiri huleta majigambo na kutojali
Tusitoane hofu katikati ya hatari kubwa.. Tusifiche uhalisia kwa kufutika uvundo kibindoni.. Tuambiane ukweli.. Tutaokoa maisha mengi
Tukiwatoa watu hofu huku sisi tumefichama tunatengeneza tatizo kubwa zaidi.. Wananchi wanakuwa sio makini tena na tahadhari inakuwa ndogo..
Tumepigwa tena kwenye dawa isiyothibitishwa na ambayo hatutaweza kuitumia kwa miezi sita
Mungu wabariki waja wako.. Na watesi wa wana wako... Wabariki pia

Jr
Umewaza kama mimi. Iweje tutumie gharama kuuubwa kiasi kile (mafuta yaliyotumika, posho za wasafiri na cabin crew na posho zao, gharama za chakula na malazi) kwenda kufuata chupa mbili😀😀😀 zenye ujazo wa 500mls@. Yaani tukashindwa hata kupiga simu tu kuwaambia "wazee, tunaomba mtuwekee kwenye buti ya meli/ndege ya mizigo hizo chupa mbili pesa tunatuma mpesa na ya kutolea." Ama hata angetumwa mfanya usafi tu wa wizarani akimbie faster.

Aliyesema maajabu ya dunia yako 7 pekee, apimwe akili.
 
Back
Top Bottom