Jeshi la Polisi Wilaya ya Kigoma limezuia mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Zitto Kabwe

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,802
11,961
JESHI LA POLISI KIGOMA LAZUIA MKUTANO WA ZITTO KABWE.

Jeshi la Polisi Wilaya ya Kigoma limezuia mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Ndugu Zitto Kabwe uliopangwa kufanyika leo katika viwanja vya Mwanga Center, Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Kwenye barua yao kwa Ofisi ya Mbunge huyo, Jeshi la Polisi Wilaya ya Kigoma linadai kuwa limezuia mkutano huo "..kwa sababu za kiusalama kutokana na taarifa za kiintelijensia zilizopo".

Sababu iliyotajwa bila shaka haina mashiko na inalenga kumzuia Ndugu Zitto Kabwe kutekeleza shughuli zake halali za kutumikia wananchi wa Jimbo lake.

Ado Shaibu, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano na Umma, ACT Wazalendo.
17 Januari 2020.

Zaidi soma: Bashiru aanza ziara Kigoma, Zitto Kabwe azuiwa kufanya mkutano

1579240845745.png
 
Jeshi la polisi Kigoma linashindwa kusema ukweli,hakina cha Intelijensia wala usalama .
Kilichofanya wazuie ni Ziara ya Katibu mkuu wa CCM Dr.Bashiru Ally.

Bashiru atakuwa na ziara ya siku tatu,leo anatua Airport na kwenda Uvinza,kesho atakuwa Kigoma Kaskazini kwa Serukamba na Kesho kutwa atakuwa Kigoma mjini.

Sasa Zitto yupo Jimboni kwake,kwanini azuiliwe ?

Ni juzijuzi Diamond akiwa na timu yake walikesha pale Lake Tanganyika Stadium,watu hao hao aliokesha nao Diamond ndio hao hao watakaohufhuria mkutano wa Zitto,but no intelligency question.

Hii ni red alert kuelekea uchaguzi mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona barua haina muhuri wa ofisi ya jeshi la polisi?
Hawajaweka muhiri kwa makusudi ili ikitokea mkutano unataka kufanyika wakapige mabomu na kuwatawanyisha watu lkn,chama kikiahirisha mkutano jeshi la polisi watasema "sisi hatukuzuia mkutano huo na hiyo barua siyo yetu si unaona hata haina muhuri?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanatekeleza agizo la katibu Mkuu Daktari Bashiru. "Tutatumia mbinu zilezike tulizotumia uchaguzi wa serikali za mitaa kushinda zaidi ya 99% uchaguzi mkuu" Mwisho wa kunukuu.
 
JESHI LA POLISI KIGOMA LAZUIA MKUTANO WA ZITTO KABWE.

Jeshi la Polisi Wilaya ya Kigoma limezuia mkutano wa hadhara wa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini Ndugu Zitto Kabwe uliopangwa kufanyika leo katika viwanja vya Mwanga Center, Manispaa ya Kigoma Ujiji.

Kwenye barua yao kwa Ofisi ya Mbunge huyo, Jeshi la Polisi Wilaya ya Kigoma linadai kuwa limezuia mkutano huo "..kwa sababu za kiusalama kutokana na taarifa za kiintelijensia zilizopo".

Sababu iliyotajwa bila shaka haina mashiko na inalenga kumzuia Ndugu Zitto Kabwe kutekeleza shughuli zake halali za kutumikia wananchi wa Jimbo lake.

Ado Shaibu, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano na Umma, ACT Wazalendo.
17 Januari 2020.

Polisi wapo sawa nimeamini mazuio wanayoyafanya ni kweli Kabisa, Maana hawa majitu walipanga kuuana kwenye Mkutano kutokana na kutokukunaliana kuhusu Kumn'g'oa Meya. Walipanga kumtandika Bakora Zitto na Meya mbele za Wananchi. Kwenye vijiwe mbalimbali vijana walijipanga kumshikisha adabu Zitto kutokana na kuwatumia kama toilet paper.
Vijana walikuwa na hasira. Mbaya zaidi alikuwa anataka kumtumia kijana kwa manufaa ya kisiasa ambaye nusura ale kichapo maeneo ya Gungu sokoni. Hali huku Kigoma Mjini ilikuwa ni Mbaya saaana. Walipanga Wilson Mogha kuwa Chambo kwao 😆😆😆😆😆😆😎😎😎😎😎😎
 
Wakati wanazuiya huo mkutano bashiru anakuja kigoma kwa ziara.

Wakati upinzani ukidai tume huru ya uchaguzi, mi na sema hio haitoshi

Tunataka jeshi la police pia huru
Vyombo vya usalama pia huru
Office ya msajili wa vyama vya siasa pia huru
Na tume ya uchaguzi huru,
Book la wapiga kura huru

Bila ya hivyo ni kupoteza muda
 
Polisi wapo sawa nimeamini mazuio wanayoyafanya ni kweli Kabisa, Maana hawa majitu walipanga kuuana kwenye Mkutano kutokana na kutokukunaliana kuhusu Kumn'g'oa Meya. Walipanga kumtandika Bakora Zitto na Meya mbele za Wananchi. Kwenye vijiwe mbalimbali vijana walijipanga kumshikisha adabu Zitto kutokana na kuwatumia kama toilet paper.
Vijana walikuwa na hasira. Mbaya zaidi alikuwa anataka kumtumia kijana kwa manufaa ya kisiasa ambaye nusura ale kichapo maeneo ya Gungu sokoni. Hali huku Kigoma Mjini ilikuwa ni Mbaya saaana. Walipanga Wilson Mogha kuwa Chambo kwao
Shida ya meya na madiwani hasa ni nini? Ongeza nyama mkuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom