Mtoto apigwa na kisha kuwekewa pilipili sehemu za siri na machoni

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,492
9,266
Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa Mlenda wameitaka serikali ichukue hatua kali kwa wazazi waliohusika kumfanyia vitendo vya kikatili mtoto wao Hadija Abdallah (7) baada ya kumpiga kisha kumuwekea Pilipili sehemu za siri kwa kosa la kutokujaza maji kwenye diaba.

Akizungumza na Muungwana Blog Mwenyekiti wa Mtaa wa Mlenda ulioko manispaa ya Tabora Mkoani Tabora m Mwanahawa Koja amesema Serikali ya Mtaa ilipata taarifa ya tukio hilo kwa wasamaria wema juu ya manyanyaso ya mtoto huyo ambapo wasamaria na majirani kwa kushirikiana na serikali walimpeleka hospitali kupata huduma kisha wazazi kushikiriwa na jeshi la Polisi na baada ya muda waliachiwa kwa dhamana na kumtekeleza mtoto huyo.

“Mpaka sasa hatuna taarifa yoyote juu ya wazazi wa mtoto huyo wamemtelekeza na kukumbia ninawaasa wazazi na walezi kuachana na tabia hii ya kunyanyasa watoto kwa mtu yeyote atakaye kamatwa kwa tukio hili tutamchukulia hatua sitahiki,” amesema Mwanahawa

Jirani wa mtoto huyo Bi. Chausiku Saidi amesema licha ya mateso ya mtoto huyo lakini Baba yake amekuwa hachukui hatua yeyote ya kumlinda hasa haki ya Elimu licha ya umri wake wa kwenda shule umefika lakini mtoto hajapelekwa.

“Mtoto amekuwa anapigwa na kufanyiwa vitendo vya kikatili huku baba anamwangalia hasemi lolote kunasiku alikatwa kisu akajiuguza mwenyewe kidonda mpaka kapona amekuwa ana nyanyaswa sana nawaomba wanawake wenzangu tuachane na tabia hiyo,” amesema Chausiku.

Yasini Mfuko amaye pia ni mkazi wa mtaa huo amesema kinababa wanatakiwa kusimama katika malezi ya familia na sio kukaa kimya waonapo mateso ya watoto katika familia na kufumbia macho ili kuweza kutokomeza vitendo hivyo.
 
Wanaume jaman wakat mwingine tujitafakar s kila mwanaume ana sifa ya kuitwa baba kama huwez timiza majukumu yako kama baba tusizae maana na uhakika kama baba angekuwa makini hata mzaz mwenzie asingefanya haya aliyoyafanya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huko Taa bora kuna shida, mara waweke ugoro sirini mara pilipili kwa nini wanavionea hivyo viungo
 
Duuh. Huyo baba bure kabisa
Huyo ni baba wa ajabu kabisa..Mungu mlaani!

Sent using Jamii Forums mobile app
Pole kwa mhanga mtoto Hadija Abdallah. Mungu amjaalie apone haraka na kurejea katika afya njema.

Nachoona hapa ni Wanaume wa Tabora kupiku sifa zisizo rasmi za wanaume wa Dar/Pwani kwa kasi kubwa.

Ipo haja ya WanaTbr kuwakemea wanaohujumu jitihada kubwa zinazofanywa na RC. Vinginevyo TaaBora itabaki na sifa ya Utajiri wa Kunukia na Umaskini wa Kunuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wapelekwe Milembe wajitathimini

Back
Top Bottom