Mume wa mtu ananitesa

Novela E

Member
Feb 5, 2019
28
33
Habari za weekend wakuu

Miaka 7 iliyopita nilikutana na kaka mmoja Muheza Tanga alikuwa kikazi na mimi pia nilikuwa nipo pale kikazi. Tulikuwa marafiki sana nikajikuta nampenda sana ila yeye alikuwa na mahusiano yake.

Basi siku moja uzalendo ukanishinda nikamwambia M, nakupenda sana akasema hata yeye ana hisia na mimi ila ana mchumba wake anamsomesha so hawezi kumuacha. Basi niliumia lakini nilimuelewa tukabaki kuwa marafiki.

Baada ya mwaka nikapata mchumba nikaolewa, nikabahatika kupata watoto wawili na mume wangu ambae naishi nae mpaka sasa kwa kweli Mr ananipenda na wote tuna hofu ya Mungu hatujawahi kuumizana kwa namna yoyote miaka yote mitano tuliiishi wote.

Jamaa yangu yule wa Muheza naye mwaka juzi akaoa, lakini ndoa yao haina amani wanagombana kila siku.

Mwaka jana waligombana M, akanitafuta kuwa wife anamsumbua na wametengana basi tukajikuta tumefall in love tunatumiana picha mpaka za uchi nikajikuta nampenda sana kuliko hata mume wangu na hapo hatujawahi kusex hata siku moja.

Mwaka jana wakapatanishwa na wife wake, akaniambia nikamwambia sawa sababu hata mimi pia nina mume so sio big inshu.

Akaniambia, "Unajua nini V, tulia kwenye ndoa yako Mungu amekupa mume mzuri na mnaishi kwa amani acha mm nipambane na hali yangu. Nilikupoteza kwa ujinga wangu ingawa bado nakupenda lakini mumeo akija kuona chat zetu atakuua."

Niliumia nikamwambia okey lakini umeniteka akili yangu naumia sana juu yako, natamani tukutane hata siku moja tupeane raha halafu tuachane akasema sawa ila mawasiliano na mimi kapunguza anaogopa mke wa mtu na mimi nimeshadata kwake.

Sijawahi kuchepuka hata siku moja namuogopa Mungu, namuogopa mume wangu akijua itakuwaje sababu ananiamini sana.

Yule jamaa wa Muheza nampenda sana tena sana na yeye ananipenda lakini naogopa kuchepuka.

Naombeni ushauri, nifanyeje?



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Una hofu ya Mungu halafu unaogopa kuchepuka halafu unaomba ushauri, unataka ushauri gani sasa? Wakuambiwa chepuka ama, mimi sikushauri uchepuke kwanza mpotezee kabisa huyo jamaa unavyozidi kuchat nae ndiyo hali ya kutaka kuchepuka inakunyemelea, jiheshimu, heshimu ndoa yako, miheshimu mumeo.
 
Back
Top Bottom