Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Mbunge wa Nzega Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hussein Bashe, amesema kua kuna watu wamemtumia ujumbe yeye ni miongoni mwa watu 11 waliopo katika hatari ya kufanyiwa vitu vibaya popote pale walipo.
Mbunge huyo ameeleza kuwa amefahamishwa na baadhi ya Mawaziri kuwa ndani ya Idara ya usalama wa Taifa kuna kikundi ambacho kinahusika na utekaji wa watu.
Bashe aliendelea kusema kuwakuna wabunge 11 wapo kwenye orodha ya kutekwa na kuondolewa uhai.
Kufuatia vitisho hivyo alivyo pewa Husein Bashe ameitaka serikali na bunge lake kuto fumbia macho vitendo hivyo viovu vya wananchi kutekwa na watu wasio jilikana.
Kwa hapa tulipofika, ni wazi kuwa JPM ajitafakari na baadhi ya watu wanaomzunguka. Kuna hali ya tahayari katika Taifa.