Nifanye nini ndevu zisiote kabisa au zichukue muda mrefu kuota?

Heisenberg

JF-Expert Member
Apr 26, 2017
1,683
2,906
Wakuu Habarini.
Nna issue moja inanisumbua sana nimeona nije hapa nipate ufumbuzi.

Nina tatizo la kuota ndevu kwa haraka sana nadhani kuliko binadamu wa kawaida yoyote.

Bahati mbaya sana kazi ninayoifanya inanilazimu nisiwe na Ndevu. Hivyo maisha yangu yote yametawaliwa na kunyoa ndevu tuu

Yani nikinyoa ndevu saa mbili usiku hadi kufika asubuhi saa 12 ni kama sikunyoa ndevu kabisa

Yani nikilala usiku nazisikia kabisa ndevu zinaota

Imefika kipindi inanibidi niwe nanyoa kila asubuhi ili nikienda kazini niwe Nadhifu.

Naomba msaa nifanye nini ili ndevu zisiote kabisa au laa kupunguza tatizo.

Natanguliza shukrani.
 
Uwe unanyoa kila hiyo asubuhi tu ndIo solution... hayo mawazo ya kutaka kujua dawa ya kuzuia zisiote yafyekelee mbali utakuja na shida nyingine tena
 
Wakuu Habarini.
Nna issue moja inanisumbua sana nimeona nije hapa nipate ufumbuzi.

Nina tatizo la kuota ndevu kwa haraka sana nadhani kuliko binadamu wa kawaida yoyote.

Bahati mbaya sana kazi ninayoifanya inanilazimu nisiwe na Ndevu. Hivyo maisha yangu yote yametawaliwa na kunyoa ndevu tuu

Yani nikinyoa ndevu saa mbili usiku hadi kufika asubuhi saa 12 ni kama sikunyoa ndevu kabisa

Yani nikilala usiku nazisikia kabisa ndevu zinaota

Imefika kipindi inanibidi niwe nanyoa kila asubuhi ili nikienda kazini niwe Nadhifu.

Naomba msaa nifanye nini ili ndevu zisiote kabisa au laa kupunguza tatizo.

Natanguliza shukrani.

Ukilala unazisikia zikiota ?? hapa ndo umeharibu mkuu
 
Njia ipo mkuu, siku ukiwa OFF nyofoa moja moja mpaka ziishe au zibaki chache zina maumivu makali n zitakuachia vipele vilivyovimba kutokana na maumivu baadaye vitakwisha na ndevu zako zitachelewa sana kuota.
 
Mungu ana kazi nzito sana. Wengine wanalilia ndevu, wengine tunazichukia!

Nami pia ni muhanga (ingawa mie huwa sizisikii zikiwa zinaota!)....tofauti yangu ni kuwa kazi yangu hainilazimu kunyoa. So wakati mwingine huwa naziacha tu zijiotee kidevu na mashavu yapumzike kidogo.

Btw, ni kwa nini Mungu aliumba mwanaume awe na ndevu? Kazi yake ni nini hasa? Ama ni "urembo" tu?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom