Kujitegemea wenyewe na kufanya jitihada kwa ushupavu dhidi ya wapinga maendeleo bila kusababisha taharuki miongoni mwa wengine / umma

Joselela

JF-Expert Member
Jan 24, 2017
5,676
6,961
Nimeona na mimi niandike kidogo juu ya mambo ya kutimia nguvu na utekaji wa watu mashuhuri na wanasiasa aidha wanaopinga moja kwa moja jitihada za kimapinduzi ya uchumi au wale wanaohisiwa kutokana na intelijinsia ya vyombo vyetu.

Naandika hivi ili tujue au tutambue chanzo cha haya yote ni nini na msingi au mzizi wake umetoka wapi?

Karibu ambatana nami uweze kutambua sasa kwa nini tumefikia hatua hii ingawa wengi au baadhi watashindwa kuhusianisha.....

HEBU SOMA NA ELEWA KIPANDE HIKI KUHUSU KUJITEGEMEA NA KAFANYA JITIHADA KWA USHUPAVU.

Siasa yetu iwekwe juu ya msingi gani?
Inatakiwa iwekwe juu ya msingi wa nguvu zetu wenyewe, na hiyo ina maana ya kujitegemea wenyewe. Hatuko peke yetu; nchi zote na watu wote wa dunia nzima wanaopinga ubeberu ni marafiki zetu. Hata hivyo, tunatilia mkazo wa kujitegemea wenyewe. Kwa kuzitegemea nguvu tunazozikusanya sisi wenyewe, tunaweza kuwashinda wapinga maendeleo wote wa kitanzaniana wa kigeni.

Sisi tunatetea kuzitegemea wenyewe. Tunatumainia kupata msaada wa nchi za nje lakini hatuwezi kuutegemea msaada huo; tunategemea juhudi zetu wenyewe, nguvu za busara za jeshi lote na watu wote.

Kupata ushindi wa nchi nzima ni hatua ya kwanza tu katika mwendo mrefu wa li elfu kumi. .......Mapinduzi Tanzania ni makubwa, lakini njia ya baada ya Mapinduzi itakuwa ndefu zaidi. Jambo hili lazima sasa liwekwe wazi katika chama. Makomredi lazima wasidiwe kuendelea kuwa wanyenyekevu, wenye hadhari na kujiepusha na majivuno na papara katika mtindo wao wa kufanya kazi. Makomredi lazima wasaidiwe kuendelea na mtindo wa kufanya jitihada kwa ushupavu sio mabavu.

Lazima tuyaondoshe kwa ukamilifu miongoni mwa makada wetu mawazo yote ya *kupata ushindi kwa urahisi kwa kutegemea bahati nzuri, bila ya mapigano magumu na makali, bila kutoa jasho na damu wala kuichafua sura ya nchi.

Inataka tufanye uenezi habari kwa mfululizo miongoni mwa umma juu ya ukweli wa maendeleo ya dunia na mustakabali mzuri ulio mbele ili wajenge imani ya ushindi wa haki. Kwa wakati huo huo, lazima tuwaambie umma na tuwaambie makomredi wetu kwamba patakuwepo mazonge mengi kwenye njia yetu. Bado vipo vingi ni shida nyingi kwenye njia ya Mapinduzi. Mkutano mkuu wa chama lazima ufikirie kuwa kutakuwa na shida nyingi, kwani tunaona bora kufikiria shida nyingi zaidi kuliko kidogo.
Baadhi ya makomredi hawapendelei kufikiria sana shida. Lakini shida ni mambo yaliopo; lazima tuzitambue shida nyingi kama zilizopo sasa na tusifuate "siasa ya kutotambua".Lazima tuzitambue shida, tuzichambue na tupambane nazo. Hakuna njia zilizonyooka katika dunia; lazima tujitayarishe kufuata njia amabayo ina mizunguko na mapindo na tusijaribu kupata vitu kwa urahisi. Isiwazwe kwamba mnamo asubuhi moja nzuri wapinga maendeleo na vijibwa vyao vyote watapiga magoti kwa hiari yao. Kwa ufupi, mustakabali ni mzuri, na njia ina mazonge mengi. Bado ziko shida nyingi mbele yetu na tusizipuuze. Kwa kuungana na umma mzima katika juhudi ya pamoja, hakika tunaweza kuzishinda shida zote na kupata ushindi wa haki.

*Mtu yeyote anayeona upande mzuri tu lakini haoni upande wa shida basi mtu huyo hawezi kupigana vyema katika kutimiliza kazi za chama na nchi.*

Utajiri wa jamii unaletwa na wafanyakazi, wakulima na wataalamu wafanyao kazi. Ikiwa watachukua maisha yao katika mikono yao wenyewe, wakafuata msimamo wa kimarx-lenin na kuchukulia bidii katika kuyatanzua matatizo badala ya kuyakwepa na kutimia nguvu, hapa to hapatokuwa na shida yoyote katika dunia ambayo hawataweza kuishinda.

Makomredi katika chama chote lazima wazizingatie vyema shida zote na kujiweka tayari kuzishinda kwa moyo usiovunjika na kwa njia ya mpango. Nguvu za kipinga maendeleo zina shida zao na sisi tuna zetu. .Lakini shida za nguvu za kipinga maendeleo haziwezi kushindwa kwa sababu hizo ni nguvu zinazokaribia kifo na hazina mwisho mwema. Shida zetu zinaweza kushindwa kwa sababu sisi ni nguvu mpya ambazo zinachomoza na zina mustakabali mzuri.

Katika nyakati za shida, sisi makomredi tusisahau mafanikio yetu, lazima tuuone mustakabali mzuri ulliombele yetu na tupige moyo konde.

Mambo mapya siku zote lazima yakutane na shida na vipingamizi wakati yanapokua. Ni ndoto tu kuwaza kwamba jihadi ya usoshalisti itafanikiwa kwa urahisi katika hali shwari, pasipo na shida na vipingamizi au bila ya kutumia jitihada kubwa.

Katika nyakati fulani za mapigano ya kimapinduzi, shida zinakuwa zimezidi hali nzuri na kuwa ndio upande wa nguvu wa hitilafu, na hali nzuri kuwa ndio upande dhaifu. Lakini wana -mapinduzi kwa jitihada zao wanaweza kuzishinda shida hizo hatua baada ya hatua na kuleta hali mpya ya mwafaka bila kutumia nguvu na mabavu; kwa hivyo hali ya shida inaondoka kuipisha ile ya mwafaka.

Nini maana ya kazi? Hapa kazi tu? Kazi ni mapigano. Popote pale penye shida na matatizo, inatuwajibikia kwenda kuyatanzua kwa njia iliyosalama isiyoumiza wengine yenye kutenda haki na usawa miongoni mwa umma. Tunakwenda kufanywa kazi na kupigana ili tuzishinde shida hizo. Komredi mzuri ni yule mwenye hamu kubwa ya kwenda pale penye shida kubwa zaidi.

Wa salaam,
Joselela.
 
AFTER THOUGHT 1
"Nguvu za busara za jeshi lote na watu wote"

Huwezi kwenda kupigania uchumi kama hujaweza kuandaa wale watakao weza kuulinda uchumi kwa nguvu za busara za jeshi lote na watu wote aidha kisera au kwa vifaa vya kisasa vinavyoendana na wakati tulionao sasa.

Matokeo yake.
Jaribio dogo tunashindwa kullitatua kwa muda mfupi na kuzua taharuki kwa umma kwa sababu tunajua mapinduzi ya kiuchumi yatakuja na mambo mengi hivo ni muhimu kuuandaa umma kwa kuwapa sera na expected thingy na kuimarisha nguvu za busara za jeshi letu.
 
AFTER THOUGHT 2
"Kupata ushindi wa nchi nzima ni hatua ya kwanza tu katika mwendo mrefu wa li elfu kumi. . . . . . . "

Rais wetu anapambania katika kile nitakachokiita kutupandisha chart kimataifa, na kiuchumi....Leo hii au kesho ikitokea tumepanda chart na kwakuwa yeye ni kiongozi na binadamu na sifa za binadamu yeyote ni pamoja na kukua na kufa. Lakini yeye anammlaka ya kupanda mbegu mbaya au nzuri, ikiwa atapanda mbegu nzuri tutaendelea kuvuna hivo hivo muda wote na vice versa hata pale sifa ya kuwa binadamu inapokoma.
 
AFTER THOUGHT 3
"lazima tuyaondoshe kwa ukamilifu miongoni mwa makada wetu mawazo yote ya kupata ushindi kwa urahisi kwa kutegemea bahati nzuri "
Makada wa chama wanapenda kupata matokeo haraka kwa njia rahisi bila kufikiria kwamba ushindi halali na wa haki unakuja kwa kufanya kazi kwa bidii na kulia juhudi kubwa zaidi kwa kutumia akili na nguvu kidogo au kutotumia nguvu kabisa..

Hili limeonekana kwa uwazi zaidi katika chaguzi mbalimbali za marudio kuwepo kwa matumizi makubwa ya nguvu kana kwamba watu wale walipanga kufanya vurugu.

Hili linatokana na kutojiamini makada hawa.
 
AFTER THOUGHT 4
"Makomredi katika chama chote lazima wazizingatie vyema shida zote na kujiweka tayari kuzishinda kwa moyo usiovunjika kwa njia ya mpango. "

Wakati fulani fulani makada hawa huwa kana kwamba hawaoni wala hawasikii, wa me wamekuwa na ubaguzi wa kutochukulia shida zote katika usawa wanatazama chama Chao tu na matumbo yao (shida za watu wanao husiana wenye maslahi ya pamoja ) makada hawa wamesahau kabisa utu wa binadamu mwenzake na mustakabali mzuri ulio mbele kwa ajili ya umma.

Tumeona ubaguzi kwa wanasiasa, viongozi ,waandishi wa habari na watu wa kawaida wenye mlengo fulani fulani.

Je kwa mtindo huu tutawezaje kufikia uchumi wa juu na kupanda chati za kimataifa bila kuwa wa moja na wenye upendo miongoni mwetu?

Je mnategemea wapinga maendeleo wote na vijibwa vyao vyote wataacha kutuvuruga wakati huo huo wanaona kuna mwanya huo, upendo na umoja na mshikamano miongoni mwetu wenye dhamana ya uongozi na umma kwa ujumla unapokosekana?
 
AFTER THOUGHT 5
"Komredi mzuri ni yule mwenye hamu kubwa ya kwenda pale penye shida kubwa zaidi ."

Shida kama nchi inayoibukia katika maendeleo zipo nyingi sana, kiongozi mzuri anaenda penye shida kubwa zaidi inayopigiwa kelele nyingi na umma wa watu ili aweze kuziba loop holes au mianyaa ya kutendeka mengine kupitia shida hiyo yenye kuleta mianyaa hiyo.
 
AFTER THOUGHT 6
"NI ndoto tu kuwaza kwamba jihadi ya usoshalisti itafanikiwa kwa urahisi katika hali shwari, pasipo na shida na vipingamizi au bila ya kutumia jitihada kubwa "

Ni kazi ngumu viongozi au watawala kuamini kwamba kila jambo litakwenda kama walivo panga, ni lazima watambue haijawahi kutokea ,haiwezi kutokea wala haitatokea hapa dunia na tangu dunia iumbwe.

Hivyo matumizi ya nguvu sio mbadala wake bali mienendo bora ya kiongozi ndio itaweza kuwashinda wapinga maendeleo wote wa kitanzania na wageni badala yake utamaliza kizazi chote bila matokeo mwafaka.
 
Mbona gazeti zima umehamishia hapa? Umeona takwimu ya 2018 ya viwango vya furaha kwa wananchi wa nchi mbalimbali duniani? Kati ya nchi 156, Tz inashika namba 153, ikizitanguliaa nchi 3 tu. Ina maana waTZ hawana furaha kabisa.. Unajua sababu??
 
Hakuna maendeleo kwenye mfumo wa ujamaa dunia ilishatoka huko ambako sie ndo tunaelekea
 
Hakuna maendeleo kwenye mfumo wa ujamaa dunia ilishatoka huko ambako sie ndo tunaelekea
Kutokua wajamaa kuna weza sababisha ugomvi wa wenyewe kwa wenyewe na kushindwa kuvumiliana, nazungumzia ujamaa ambao utatufanya tuwe na utangamano wa kitaifa hivo ndivo tutaweza dumisha amani na kujenga uchumi wa nchi bila hivo hakuna....

Ujamaa huu nauzungumzia katika mktadha wa umoja.

Nenda uingereza au america ukaone ujamaa ninaouzungumza mie katika mktadha wa umoja kama haupo.
 
Back
Top Bottom