Blue Bahari
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 1,229
- 1,141
Ndg wana JF habarini.
Mimi ni mwalimu wa masomo ya Sanaa ktk idara ya sekondari. Nalazimika kuandika mada hii kwa kuwa naguswa na majukumu mazito waliyonayo walimu wa masomo ya Sayansi (chemistry, biology & physics).
Kiukweli tuliopo humu jukwaani hakuna ambaye hakufundishwa na mwalimu wa Sayansi kulingana na mitaala yetu ya Elimu (aidha kidato cha kwanza na cha pili au mpaka kidato cha nne na kuendelea... Linapokuja suala la majukumu kwa walimu tajwa-walimu wa Sayansi wanamajukumu mengi kama vile:-
MAPENDEKEZO.
Ni wakati muafaka Serikali yetu ione umuhimu wa malipo ya ziada kwa walimu wa sayansi. Katika hili aidha walipwe mshahara mkubwa zaidi ya walimu wa masomo ya sanaa, au mshahara uwe sawa sawa lakini walimu wa masomo ya sayansi wawe wanapewa posho kama wakuu wa shule wanavyopewa kwa sasa.
FAIDA ZA KUFANYA HIVYO.
Kama serikali haina pesa za kuwalipa mishahara mikubwa zaidi walimu wa masomo ya Sayansi au kuwalipa posho za ziada, basi iajili Lab technicians ili kuwasaidia majukumu walimu hao.
=================================
MAONI MUHIMU YA WADAU WENGINE.

- Kufundisha "theory" za masomo husika (chemistry, physics, biology). Na shule nyingi za serikali-kama vile za kata, walimu wa masomo ya Sayansi wana vipindi Vingi kwa wiki (si chini ya 25) tofauti na walimu wamasomo ya sanaa.
- Kutafuta na kuandaa specimens au kuandaa solutions/ vifaa kwa ajili ya practicals.
- Kuelekeza na kusimamia namna ya ufanyaji wa practicals husika.
- Kazi za kusahihisha ni theory na practicals.
- Kazi zingine walimu hao wanazozifanya ni kama vile, kuandaa notes, mipango kazi ya mwaka mzima, maandalio ya masomo sawa sawa na walimu wa masomo ya sanaa.
MAPENDEKEZO.
Ni wakati muafaka Serikali yetu ione umuhimu wa malipo ya ziada kwa walimu wa sayansi. Katika hili aidha walipwe mshahara mkubwa zaidi ya walimu wa masomo ya sanaa, au mshahara uwe sawa sawa lakini walimu wa masomo ya sayansi wawe wanapewa posho kama wakuu wa shule wanavyopewa kwa sasa.
FAIDA ZA KUFANYA HIVYO.
- kutaongeza hali na hamasa zaidi kwa walimu wa masomo ya sayansi kujituma zaidi katika kazi.
- Wanafunzi wengi zaidi kufaulu masomo ya Sayansi.
- Kupatikana kwa walimu wengi zaidi wa masomo ya Sayansi na kuifanya kauli mbiu ya mkuu wa nchi "Tanzania ya viwanda" ieleweke zaidi.
Kama serikali haina pesa za kuwalipa mishahara mikubwa zaidi walimu wa masomo ya Sayansi au kuwalipa posho za ziada, basi iajili Lab technicians ili kuwasaidia majukumu walimu hao.
=================================
MAONI MUHIMU YA WADAU WENGINE.
Si hayo tu kinacho shangaza hata vyuoni hao watu wanasoma kwa ada tofauti, ukienda arts 800,000/= Science 1,200,000/= wakianza kazi scale ni moja na kulipa mkopo wasayansi atadaiwa nyingi zaidi, ukiacha huo wingi wa majukumu ya kazi