Kuwa mzalendo ni kuipenda nchi, sio lazima Serikali. Wakati mwingine Serikali hushikwa na kundi la waasi,wahuni au matapeli

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,583
11,659
Siku zote nitaendelea kuwaheshimu vijana wa kitanzania wanaoendelea kuikosoa serikali hadharani, pale inapotenda ndivyo sivyo.

Pamoja na matukio ya kutisha yanayowakuta vijana/watu wanaoonesha upinzani, kama kutekwa, kupotezwa na kuuawa, lakini bado idadi ya wanaopinga maovu ya serikali inaongezeka. Viongozi wa kidola wanatumia mbinu za kutisha watu, lakini mbinu hizo hizo zinachochea kupingwa zaidi.

"Taifa linapokuwa katika hali ya vita, walevi na machangudoa huendelea kunywa na kufanya ngono kwenye mabaa na makasino"

Katika mantiki ya kifalsafa msemo huu hauwahusu walevi wa pombe na wafanya biashara ya ngono, hapana; bali wananchi wasiojua wanachokifanya kwa ajili ya nchi yao (walevi) na wananchi wanaofanya mambo yasio na maana wala faida kwa taifa bila kujali yanayoendelea.

Hali ya vita iliyotajwa hapo sio lazima iwe vita ya kuvamiwa kwa silaha maadui wa nje. No, inaweza kuwa jambo lolote linalohitaji kupigiwa kelele na kufanyiwa maamuzi ya haraka kwa faida ya Taifa zima; ingawa msemo wenyewe ukitumika wakati wa vita ya China na Japan (Sino-Japanese war) ya mwaka1937.

Walevi na Machangudoa, ndio watu wasio na msaada wakati wa vita kama wakiendelea na matendo yao hayo. Hao ndio wanaopiga kelele kutetea vitendo vya kuteka watu, na majaribio ya mauaji. Ndio hao wanaotukana maaskofu na wanaharakati wanaopinga uovu wa serikali. Hao ndio watu wa kwanza kukimbia nchi itakapongia katika machafuko.
Vijana wanaopinga maovu ya serikali wakati ambao maisha ya wapinzani hayana thamani, ndio hasa wanajeshi halisi. Kwa kuwa uzalendo ni kuipenda nchi, sio lazima serikali. Wakati mwengine serikali hushikwa na kundi la waasi, au wahuni au matapeli. Lakini nchi ipo tu. Kupinga uovu wa serikali ni ishara ya uzalendo, kiashiria cha tamaa ya mabadiliko chanya kwa nchi. Wanaochukia uzalendo huu ni Walevi na Machangudoa.

Jumapili ya Tarehe 25 machi 2018 ilikuwa jumapili ya Matawi kwa imani za kikatoliki. Huko Vatican, Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis aliwataka vijana kupaza sauti dhidi ya wazee wanaofanya ndivyo sivyo. Aliwataka vijana wasilale badala yake waongoze mapambano, kuwakosoa na kuwapinga 'wazee' wanaotenda kinyume na taratibu. Vijana waliokuwepo katika misa ile waliitika kwa sauti kubwa kukubaliana na Papa Francis.
Sio wakati wa kulala. Bahati nzuri wapo wazee ambao wanafikiri kama vijana. Tumeona hatua za maaskofu wa KKKT na TEC. Nyaraka zao ni sehemu ndogo ya harakati zinazotakiwa kwa sasa. Lakini kwa bahati mbaya kuna vijana wanafikiri kama wazee, ambao hawataki kujadili yaliyomo kwenye nyaraka hizo badala yake wanazusha propaganda na uongo ilimradi kutetea ugali wao. Hao ndio walevi na machangudoa wetu katika harakati.

Ni wakati sasa wa kuungana
na Maaskofu wetu kwa kauli moja. Muunganiko huu ukaondoe ile dhana ya upinzani kwa mslahi ya kisiasa. Maaskofu hawana maslahi yoyote ya kisiasa lakini wamesikia na kuona mateso wanayopata kondoo wao, wamepaza sauti.

Na sasa, harakati hizi sio za chama fulani dhidi ya chama kingine. Sio upande huu na ule. Bali ni upinzani wa wenye akili dhidi ya wajinga. Wema dhidi ya uovu. Uzalendo dhidi ya ulevi na uchangudoa wa kisiasa.
Tusome na kurudia rudia na kutafakari nyaraka za maaskofu. Tusikae kimya.

mr mkiki.
 
Hili gazeti bila mzinga wa Konyagi siwezi kulimaliza.
wUiqvl9.gif
 
Well said, kama mimi ninavyoisubiri hii serikali iondoke hata leo bali nitabaki kuwa mzalendo kwa nchi yangu lkn siyo kwa serikali ya mauaji.
 
We jamaa una jitahidi kujibu kila Uzi unaoanzishwa Ongera kwa hio

Ana utoto mwingi, lakini ndio demokrasia hiyo anaruhusiwa kufanya apendacho. Ila angeitumia fursa hii vizuri kutoa majibu yenye tija na sio hizo clip zisizo na maana yoyote.
 
Nakubaliana nawe 100% kuwa uzalendo wa kweli ni kuipenda nchi yako na sio lazima uipende serikali.
Kwani serikali Fulani itapita lakini nchi itaendelea kuwepo.
Siwezi kuipenda serikali ya kibabe hats Sikh moja.
Sipendi nasema sipendi serikali isiyojenga mifumo/taasisi imara yaani katiba, bunge,mahakama,pia Sera za kudumu za nchi
 
Vijana wanachanganya mawazo haya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom