Athlete Crown sio gari la kubishana nalo ukiwa barabarani acha liende

PureView zeiss

JF-Expert Member
Sep 5, 2016
8,915
29,284
1579086663469.png

Moja ya gari ambalo ni noma barabarani basi ni hili ndinga,nakumbuka jana nikiwa natokea maeneo ya RUFIJI kuja DAR ilinipa hii gari kama nimesimama

Nikiwa kwenye mwendo wa speed 100 sehemu yenye mwinuko kidogo huku nikijiona mimi ni bingwa barabarani niliiona gari likija kwa nyuma yangu kwa kasi sana ilikuwa kama mita 130 nyuma yangu basi nikasema haiwezekani nikapitwa kijinga kiasi hicho nikachochea moto nikafikisha speed 125 hivi sasa nilichokuja kunishangaza ni namna yule jamaa wa crown alivyokuwa anaomba site apite yaani ilikuwa ni kitendo cha dk 6 ile gari ilinipita na sikuiona tena.

Nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kuendesha CARINA Ti lakini niliambulia patupu
Hizi crown ni gari za safari ingawa inameza mafuta kama jini ila ni chombo cha maana nami namuomba mungu huku nikijichanga nichukue hii ndinga

Hongereni wote mnaoendesha Athletes Crown au mnaomiliki hii ndinga hakika hamjakosea
 
52 Reactions
Reply
Back
Top Bottom