Hii ndio sababu Magenius hawawezi kuwa matapeli

Humble African

JF-Expert Member
Jul 28, 2013
4,779
14,303
Duniani tumo binadamu wa aina tatu kiakili na wote tunaishi pamoja in harmony na tumegawanyika katika makundi makuu matatu kiutendaji na utekelezaji wa akili zetu.

Kundi la kwanza ni wale Magenius.. Hawa mabwana wana IQ kubwa kuliko binadamu wa kawaida wana score around (160 - 300) wana uwezo mkubwa sana wa kuchakata taarifa vichwani mwao na kufumbua mafumbo magumu kuliko ila bahati mbaya zaidi hawa asilimia 90% yao ni wagonjwa wa ugonjwa wa usonji( Autism). Ugonjwa wa akili huu, ugonjwa huu wa usonji mara nyingi huwapata wakiwa watoto wa mwaka na nusu na kuendelea. Dalili zao huwa wanapenda kukaa peke yao, hawapendi kelele, wanachelewa kuongea, wana hisia Kali sana za kunusa na kusikia na wako very bright kwenye kitu kimoja pekee. Na pia huwa wanaongea kidogo sana..they only do "small talk" they are not good conversationalist. Sio waongeaji wazuri sana.

Nilifuatilia zaidi na kuyajua mengi juu ya Autism baada ya mpwa wangu kugundulika ana ugonjwa huu wa usonji akiwa na miaka 3..huyu dogo ana miaka 10 tu kwa sasa mnaweza kuwa mmekaa nje akawambia mtoto analia na kweli after a second dogo analia ndani...then mmekaa nje anakwambia maharage yanaungua..na kweli mnasikia harufu ya maharahe kuungua jikoni punde baada ya yeye kusema. Wako very sensitive. Ni wakimya na pia very loner..wanapenda kukaa wenyewe tu na huwa wanaconcetrates na kitu kimoja tu mawazoni mwao huyu dogo shuleni ni mtupu but he is very artistic genius and creative, unaweza ukatembea nae mjini then mkirudi home anadrawing kit yake ya kuchorea tu anachora mji mzima mlimopita kwa usahihi bila kurejea popote pale hadi huwa navurugwa ufahamu ukizingatia Mimi hata kuchora kagari tu siwezi. Nikagundua dogo is genius sababu ya ugonjwa wake wa usonji.

Nikarejea historia ya Michelangelo na Vincent Von Gosh hawa wote walikuwa artistic genius..huyu Van Gosh alikuwa anaweza kuuchora hadi upepo unaovuma..hakyamungu! This is insanely genius..ukingalia kwenye picha zake za starry starry night utaona kazi zake but alikuwa mwehu na michoro hii aliichora akiwa kwenye chumba cha vichaa alipojipiga risasi na kufariki akiwa mpweke sana. Michaelangelo huyu ni balaa yeye hata simzungumzii maana anahitaji Uzi wake kabisa ili tumtendee haki. Tukipata muda tutamjadili.

Albert Einstein Mwanamahesabu na mwanafikizia ambae amebadilisha maisha ya binadamu anaaminika kuwa the most influential scientist of the 20th century, amechangia mengi kwenye aerospace engineering, astrophysics, mathematic, spirituality e.t.c alifanya kazi kubwa ya sisi kuishi hivi Leo kwa theory yake of relativity ya E=MC sqaure ndio theory iliofagia njia ya kutengeneza mabomu ya nyuklia Leo hii. Akiwa na miaka 10 usonji ukiwa umemuandama hakuweza kuongea vizuri wala kuwa na marafiki akiwa na IQ kubwa kabisa aliweza kufaulu somo moja tu la hisabati tu shuleni yaliyobaki alifeli vibaya sana. Alipofikisha miaka 16 alikuwa anaitwa chuoni kusolve complex mathematics equations zilizowashinda maproffesor na akiwa na miaka 25 hakukubaliwa na vyuo vingi maana kwenye mtihani wa kujiunga na chuo alifaulu somo moja pekee mathematics kwa asilimia 100. Watu hawa huwa wanakuwa na ugonjwa wa Usonji unaowafanya kufikiri kitu kimoja tu deeply kutokana na nerve circuit zao zilivyoundwa kwenye brain. Magenius maarufu Waliothibitika kuwa na Autism ni Albert Einstein, Charles Darwin, Sir Issac Newton, Michelangelo, Aristotle, Tesla e.t.c Wengi wao wana muandiko mbaya sana maana mikono yao haiwawezi kuendana na kasi ya ubongo unavyofikiri, hivyo wanajikuta wanaandika fasta na rough ili kukimbizana na kasi ya ubongo wao unachokifikiria.

Tunahitimisha kwa kukubaliana na mwanafalsa maarufu wa ugiriki ya kale kwamba any genius is accompanied with some sense of madness.. Magenius wengi ni vichaa na hii inapigiliwa msumari na kauli hii "too much of anything is harmful " akili ikizidi kipimo muhusika anakuwa hayuko normal na hivyo anakuwa psychiatric Case hivyo ni ngumu sana kichaa kukutapeli maana ni mgonjwa wa akili maana ana complex things kichwani ambazo hata yeye hawezi na hana lugha ya kuzielezea kwa watu wakamwelewa kirahisi atawezaje kukushawishi uingie mkenge!? Jibu ni hawezi kukutapeli maana hata hawana good socializing ability kama wengine. lakini hapa sasa ndipo linapoibuka kundi la watu wengine wanaitwa "intelligent people" watu hatari sana hawa.

Hawa intelligent people bongo zao ziko katikakati kiakili wana uwezo wa kupata maneno sahihi ya kuelezea zile complex ides za genius..hawa uandika hata zile manual zinavoelezea namna ya kutumia vitu mbalimbali vilivyoundwa na magenius kwa lugha rahisi na nyepesi maana wanayo maneno sahihi na ya kueleweka kirahisi, hawa wanaandika kimkakati hoja zao na kuweza kushawishi watu kirahisi sana kama alivyosema Fid Q msanii wa hip hop kwamba "neno zuri huwa halina ukweli na neno baya ndio lenye ukweli " hawa intelligents siku zote Daima dumu wana maneno sahihi na matamu ya kukufanya uuone ukweli au usiuone.. Aina ya watu hawa ni Adolph Hitler, Barack Obama, Hemingway, e.t.c na Kwenye hili kundi wanakaa matapeli pia Kariba ya brother wa Forex n.k sijawahi kuona katika maisha yangu tapeli asie jua kupachika maneno sahihi na matamu kwenye maandishi au maneno yake. Sijawahi kumuona! Mtaji wao ni maneno yake matamu.

Then group la mwisho ni "normal people" au tunafahamika zaidi kama watapeliwa Ahahaha. Sisi tunafit Kwenye social world maana tunaenda clockwise na jamii yetu na bongo zetu hazijisumbui kuchakata taarifa zaidi wala kuconcertrates na kitu kimoja we are carefree hatuna tofauti na simu za Motorola za zamani mwanga ukizima zinazima moja kwa moja hadi ndani tofauti na intelligents ambao wao ni simu janja(smartphone) zenyewe screen ikizima na kuwa nyeusi ujue imezima kinafiki internal background inaprocess more informations kifupi hazilali bongo zao tofauti na normal people sisi ambao ni kundi kubwa akili zetu ni za kawaida sana na ndio akili za binadamu wenye afya na wazima kiakili maana hatuoverload brain zetu na sisi sio wagonjwa wa akili kama hao wawili hapo juu wanaosumbukiwa na Autism na Bipolar disorder.

Tujitahidi tujue mechanism za matapeli na tuwaepuke mapema before its too late.

Na je unadhani wewe unafit group gani hapo juu? Kwanini unahisi group ulilochagua linakufaa? Tupe sababu?
 

Attachments

  • images.jpeg
    images.jpeg
    22.8 KB · Views: 382
Nakuona humble African aka spiritual
Salute Mzee unajua sana kuandika utafikiri una vinasaba vya Shabani Robert
But heck....Ontario ni tapeli la kiwango cha uzamivu,
Na mbali na Maneno matamu fake pia anajua kucheza na mass psychology hasa kale ka formula ka divide and rule
Ahahaha! Mkuu tunaonana hadi Kwenye Giza? Eti aka spiritual. Ahahaha. Umeninadi mkuu Kama Shaban Robert tena?

Sisi wajanja tumekimbia.. Mshike mshike ndege tunduni.

That guy is intelligent I'm glad at least umesense kitu pia.
 
Back
Top Bottom