Kuna uhaba mkubwa wa kondomu kwa baadhi ya mikoa

Elli

Platinum Member
Mar 17, 2008
55,498
86,015
Baada ya kupita mikoa kadhaa kwa kipindi cha hivi karibuni, nimegundua kuwa kuna uhaba mkubwa sana wa kondom kwenye baadhi ya Wilaya nchini. Nimefika sehemu husika na kila nilipouliza niliambiwa kuwa zimekwisha.

Nilijaribu kuongea na Wadau wa kondomu hizo kwa maana ya Watumiaji na walikiri kuwa "wanakwenda ngozi kwa ngozi". Si jambo jema wala la kufurahisha, na sio jambo la kufanyia mzaha wala kuweka siasa. Je tatizo liko wapi kwanini kondomu hazisambazwi? Je hii dhana niliyokutana nayo kuwa hazisambazwi ili baadhi ya watu waweze kuuza kondomu zao ni kweli??

Tusipobadilika tutegemee maambukizi makubwa zaidi mwakani.....
 
Hahaha bado wanachukua vipimo, zoezi likikamilika zitatengenezwa kila mtu atapata zake.
Viwanda 100+ kila mkoa ulidhani vya nini?!
 
Nilitaka kuuliza hivi zile kondom walizosema wanagawa ziliishia wapi maana mimi ni mmoja wa wadau lakini sijapata hata pakiti moja
 
Walisema wanagawa Noah sio Kondomu...Kondomu ni tatizo kubwa sana, tuwe wakweli tuwasaidie na wengine
 
Hii ndio sababu ya kuongezeka Maambukizi..... Mwambieni Ummy
 
Baada ya kupita mikoa kadhaa kwa kipindi cha hivi karibuni, nimegundua kuwa kuna uhaba mkubwa sana wa kondom kwenye baadhi ya Wilaya nchini. Nimefika sehemu husika na kila nilipouliza niliambiwa kuwa zimekwisha.

Nilijaribu kuongea na Wadau wa kondomu hizo kwa maana ya Watumiaji na walikiri kuwa "wanakwenda ngozi kwa ngozi". Si jambo jema wala la kufurahisha, na sio jambo la kufanyia mzaha wala kuweka siasa. Je tatizo liko wapi kwanini kondomu hazisambazwi? Je hii dhana niliyokutana nayo kuwa hazisambazwi ili baadhi ya watu waweze kuuza kondomu zao ni kweli??

Tusipobadilika tutegemee maambukizi makubwa zaidi mwakani.....

Asante sana kwa taarifa Mdau. Ni mikoa ipi naipi tuweze kufuatilia kwa urahisi zaidi?
 
Back
Top Bottom