Badili mtazamo wako kuhusu BMW

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,783
%24_86.jpg
Ni aina ya gari inayoaangaliwa kwa jicho la tofauti sana... Likionekana ni gari ghali na la kifahari huku watu wakitishana sana kuhusu ughali wa vipuri na upatikanaji wake wa shida.

Lakini nikwambie tu kitu kimoja hakuna gari imara kama BMW na ukiweza kufuata masharti ya kumiliki gari hutakaa ujutie pesa yako
Kama una uwezo wa kununua Brevis, Nissan Fuga au Klugger... Magari ya kijapan yenye engine kubwa na matumizi makubwa ya mafuta... Hakika HUWEZI kushindwa kununua BMW ya kawaida lakini yenye viwango sawa na hizo gari hapo juu.. Huku ukifurahia ulaji mdogo wa mafuta... Mfumo wa BMW uko tofauti sana... Umejengwa kwenye mfumo wa kuokoa ulaji wa mafuta huku nguvu ya mashine ikiwa ni ileile

Gari nyingi za kijapan hazina body ngumu tofauti kabisa na huyu mnyama BMW... Yani hata unapokaa kwenye seat unahisi kabisa umekaa kwenye mashine ya ukweli... Na ni aghalabu kukuta BMW imepinduka kichwa chini mijuu guu

Hizo magari hapo juu nazo spare zake ni ngumu na ghali kupatikana kama BMW tuu... Tena sometimes unaweza kuipata ya mnyama kirahisi zaidi kuliko hizo nyingine.

Kingine ni kwamba BMW wana variety of different styles na kila style ni bakora tofauti na hizi nyingine.... Ukikuta mabrevis yote yanafanana

Badili mtazamo wako BMW ni gari ngumu nzuri na sio ghali kama unavyodhani.. Kuwa tofauti... Miliki mnyama... Pichani hapo juu ni 320td fuel consumption ni km 15 kwa Lita sawasawa na duet tuu... Lakini mkiwa rodini mnyama atatamba
 
Back
Top Bottom