Githeri Man awaunganisha Wakenya wakati wa taharuki kwenye mtandao

COLLOH-MZII RELOADED

JF-Expert Member
Apr 6, 2017
7,544
3,130
The guy who queued to vote with githeri on his hands has his Photoshop photos gone viral ... Trending #1 in Twitter.

Here are a sample few.
-------------

b8f06ee17465b6fed9718f353ead67cd.jpg
e590dd1e8790ef25065561e883f20fc6.jpg
26ad7c734e88f107e2e735482f491fa0.jpg


Licha ya kuwepo miongoni mwa wananchi kuhusu matokeo ya kura ya urais, Wakenya kwenye mitandao ya kijamii Jumatano na Alhamisi waliunganishwa na picha ya mwanamume mmoja aliyekuwa akifurahia mlo wa Githeri kwenye foleni ya kupiga kura hapo Jumanne.

Mwanamume huyo ambaye amebandikwa jina 'Githeri Man' alinaswa na kamera ya mmoja wa wapiga kura akila mchanganyiko wake wa mahindi na maharage alioutia ndani ya karatasi ya plastiki katika kijibaridi cha asubuhi ya Jumanne.

Hadi wakati wa kuchapishwa kwa habari hii, jina lake halikuwa limetambulika wala anapoishi, kituo ambapo alipiga kura yake na aliyeipiga.

Kwenye Twitter Githeriman picha ya mwanamume huyo ilihaririwa na kuwekwa katika hali ambazo ziliibua msisimko mkubwa na utani usio na kifani.

Mojawapo ya picha hizo ilionyesha mwanamume huyo akiwa katikati ya Rais Kenyatta, Naibu Rais William Ruto na vinara wa NASA Raila Odinga na Kalonzo Musyoka.

Katika picha nyingine, alionyeshwa akifika Canaan. Msisimko wa safari ya Canaan ulianzishwa na Bw. Raila Odinga aliyasema atakuwa 'Yoshua' na kuwaongoza wakenya kutoka 'Misri'.

Alionekana pia akiwa kondakta, huku pia akitokea katika studio za Runinga za NTV na Citizen. Kwenye Spoti haikuachwa nyuma kwenye uchangamfu huo, mwanamume huyo alionekana kwenye picha mbalimbali.

Daniel Ndambuki wa Churchill Show anamsaka amhoji katika kipindi chake. Mimi niko tayari kumchangia pesa. Kubeba kwake githeri kunaonyesha alikuwa amejitolea kupiga kura. Amewaunganisha wakenya wote katika wakati wa taharuki. Tusherehekee maisha yake.

Ni kuhaririwa kwa picha hiyo ambako kulichangia wakenya mtandaoni kupunguza jumbe za chuki baada ya mwaniaji urais wa NASA, Raila Odinga kudai kwamba mfumo wa KIEMS wa IEBC ulidukuliwa usiku wa kuamkia Jumatano na kuweka matokeo ya uwongo.


6ccaebcb0650bb6421754de9e49604cd.jpg
de026d578a40ed06a3433f531d8728f3.jpg
a69aa547ce8b78f8e7cff440bb0d635a.jpg
9dc860f3730ddb366cdddeb1660802ca.jpg
f23f5b35a8bde19e7031f832a8684c82.jpg
d734e0da2fc22b1300031997c9031d83.jpg
8e1acabdcc709afd6ec4d2ef0a3f154b.jpg
cc7b1a16202d37dfcc6b5cf5f99dcd5a.jpg
1ef71f5c2e29be12c460d0e8735b97c2.jpg
b6b7e207fcd0c6a96b8cb59f36f1de05.jpg
 
Hehe,naona unapenda mokimoo.
Ndio mkuu, napenda sana Mokimoo...

kuna kipindi nilikw Nairobi nikazifahamu na nilikuwa nakula daily ila nilikuwa nanunua then naenda kuandaa maharage au mchuzi wa nyama mwenyewe thn nachanganya.

Mokimoo ni traditional food ya wakikuyu.
 
Ndio mkuu, napenda sana Mokimoo...

kuna kipindi nilikw Nairobi nikazifahamu na nilikuwa nakula daily ila nilikuwa nanunua then naenda kuandaa maharage au mchuzi wa nyama mwenyewe thn nachanganya.

Mokimoo ni tradition food ya wakikuyu.
Dah, utafanya nidondokwe na ute usubuhi usubuhi aisee! Hapo kwa mchuzi wa nyama! Acha tu! Ukipata mokimoo, kitimoto fry na kachumbari afu na kikombe cha supu hapo kando, jombaa hata vidole vyako utatafuna tu!
 
Back
Top Bottom