Kafa kaoza kwangu lakini muathirika wa UKIMWI

Status
Not open for further replies.

Bacyclerbacy

JF-Expert Member
Sep 6, 2016
1,743
3,017
Habari za leo, natumaini mu wazima wa afya kwa uweza wa M/Mungu.

Twende kwenye mada;
Kijana mzuri, mtanashati ametokea kunipenda kulingana na maelezo yake na matendo pia, kulingana na uchache wa wanaume nikaona sio case ngoja nimsikilize tuliongea mengi tukaelewana lakini kabla hatujafanya chochote nilimuomba tukapime kwanza.

Sikuamini macho yangu majibu yalikuja yule mkaka ameathirika, nililia sana kwasababu nimeshaanza kumpenda ila kwa bahati nzuri nilikuwa na subira hivyo hatukuwa kufanya chochote kile zaido ya kuongea kwa miezo m3 sasa najisikia vibaya sijui hata nimsaidiaje.

Najitahidi nisiwe mbali nae ili asijisikie vibaya ila naona kama anakuwa na hasira sana anasema namchora eti kwanini mambo ya kutambulishana kwa wazazi yamesimama, nikiamua kukaa kimya analalamika. Akaamua kukaa kimya nayeye kwa muda mrefu miezi mi2 lakini sasa ananitafuta na kuniomba iwe hivyo.

Nashindwa jinsi ya kumsaidia hapo ila lengo lake lilikuwa anioe 90% niliamini alikuwa na nia hiyo kwani ametumia gharama nyingi wakati tukitaka kuonana hadi huruma, lakini mimi naogopa sana kuwa nae japo siijui kesho yangu nitakufa na nini.

Sasa inawezekan kuolewa na mtu mwenye UKIMWI na nisipate maambukizi?

NAOMBENI USHAURI
 
Habari za leo,natumain mu wazima wa afya kwa uweza wa M/Mungu.

Twende kweny nada
Kijana mzur,mtanashati ametokea kunipenda kulingana na maelezo yake na matendo pia,
Kulingana na uchache wa wanaume nikaona sio case ngoja nimsikilize
Tuliongea mengi tukaelewana lkn kabla hatujafanya chochote nilimuomba tukapime kwanza

Sikuamin macho yangu majibu yalikuja Yule mkaka ameathirika,
Nililia saaaaaana kwasababu nimeshaanza kumpenda ila kwa bahat nzuri nilikuwa na subra hvy hatukuwa kufanya chochote kile zaid ya kuongea kwa miez m3 sasa najisikia vibaya Sijui hata nimsaidiaje

Najitahid nisiwe mbali nae ili asijickie vibaya Ila naona kama anakuwa na hasira sana anasema namchora eti kwann mambo ya kutambulishana kwa wazazi yamesimama
Nikiamua kukaa kimya analalamika .Akaamua kukaa kimya nayye kwa muda mref miez mi2 lkn sasa ananitafuta na kuniomba iwe hivy...wooooiiiii

Nashindwa jinsi ya kumsaidia hapo Ila lengo lake lilikuwa anioe 90% niliamini alikuwa na nia hiyo kwan ametumia gharama nyingi wakat tukitaka kuonana hadi huruma,lkn me naogopa sana kuwa nae japo Sijui kesho yangu nitakufa na nn.

Sasa Inawezekan kuolewa na Mtu kweny UKIMWI na nisipate maambukiz

NAOMBENI USHAURI
labda nikuulize..je yeye majibu ya vipimo vyako aliyaona? kwa sababu nadhani angeyaona asingaliendelea kukusumbua maana lazma ayaonee maisha yako huruma pia.
 
Huna cha kupoteza,muweke wazi kuwa ngoma imebuma. Ni kweli unaweza kuishi naye na uwezekano wako kupata au kutopata VVU upo sana. Lakini uwezekano wa kupata vvu kwako ni mkubwa zaidi kuliko kutopatam na hii ni kwa sababu mazingira ya mwanamke kingono yanampa chance kubwa sana ya kupata maambukizi. Pia wanaume wengi ni wazembe kumeza dawa na hivo CD4+ kuwa chini sana na hivo chance ya kukuambukiza vvu inakuwa kubwa sana kwako. Achana naye regardless ya mapenzi yako kwake. Ila kama unataka kujirisiki jitupie.
 
Ahsante sanaaaaaa
 
wema usizidi uwezo maana huwa ni dhambi,
Usifanye jambo kwa kutaka kumridhisha mtu huwa wanadamu hawaridhiki ,
lawama huwa haziepukili jiulize angekukuta ww ndo unao je angendeleza harakati za kukuowa?

kubwa piga moyo acha m'baki kuwa marafiki wa kawaida ila kujig jig na huyo mtu ni sawa kwenda kulibusu Transfoma pale ubungo..
Na ukifa ukienda kwa mungu atakuchoma moto kwa ujinga wako ,maana amekupa akili umeshindwa kuitumia
 
Angalia mapenzi yako shogaangu, km unampenda nenda mkaoane unaweza ukapata asiye na UKIMWI akakuua kwa sukar na pressure kutokana na stress zisizoisha. UKIMWI sio mwisho wa maisha waweza kufa ukamuacha yy anadunda japo infected. Maisha mema.
 
Huna cha kupoteza,muweke wazi kuwa ngoma imebuma. Ni kweli unaweza kuishi naye na uwezekano wako kupata au kutopata VVU upo sana. Lakini uwezekano wa kupata vvu kwako ni mkubwa zaidi kuliko kutopatam na hii ni kwa sababu mazingira ya mwanamke kingono yanampa chance kubwa sana ya kupata maambukizi. Pia wanaume wengi ni wazembe kumeza dawa na hivo CD4+ kuwa chini sana na hivo chance ya kukuambukiza vvu inakuwa kubwa sana kwako. Achana naye regardless ya mapenzi yako kwake. Ila kama unataka kujirisiki jitupie.
Ushauri mzuri sana. Mleta thread zingatia huu ushauri.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom