Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,633
- 697,754
Kuna vitu special hutufanya tuwe kileleni....wasanii wetu ni kutokana na kazi zao...lakini zinapokosa mvuto kwasababu ya ubunifu matatizo na mahitaji ya nyakati na kuanza kuporomoka, hutafuta njia nyingine ya kubaki kileleni.
Njia hiyo si ile iliyowapandisha! Hii ni shortcut iliyojaa kuchanganyikiwa, unaweza kuona wasanii wetu wengi wamebaki na umaarufu wa tuhuma za mambo ya ajabu kuchambana mitandaoni na kufanya mambo mengi ya kutia kinyaa alimradi tu wawe midomoni mwa watu na kwenye kurasa za media.
Wanasiasa nao ni waathirika wa umaarufu na mmojawapo ni mkuu wa mkoa wa Dsm...Ukiangalia matamko aliyokwishatoa (ambayo mengi kimsingi na kiuhalisia hayatekelezeki)utagundua kuwa ana mradi maalum wa kutafuta kiki na kubaki kwenye kurasa za vyombo vya habari na midomo ya watu.
Amegundua udhaifu wa media zetu hazina tafakuri ya kina, huandika chochote na kikapokewa kwa mlipuko na kuzua mijadala isiyoisha.....kwa njia hii anajihakikishia kubaki kileleni japo kwa kupayuka! Lakini je yuko peke yake?