Ukishindwa kusamehe lipa kisasi

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,789
ea22182088793d94f7d1d66b1dddcb77.jpg


Hii ya leo ni tofauti kidogo na mada zetu zile, hii inahusika na kulipa kisasi.

Katika maisha bila kujali unaamini nini hakuna jambo jema kama kusamehe! Msamaha hukusaidia mengi mpaka kifo na maisha yanayofuata baada ya kifo iwe reincarnation au rebirth nk !msamaha hukufanya uwe mwema mwenye furaha ya kweli usiye na makunyanzi rohoni na usoni.

Mwenye msamaha ana nuru usoni , msamaha ni tiba, msamaha ni mafanikio msamaha ni amani na ni upendo.

Lakini je kama huamini katika msamaha? Kama unayemsamehe hasameheki? Na je kama ni mbabe mjuaji na dhulumati mkubwa? Je kama anakuletea dharau kwa hali yoyote ile hata uwe msamehevu kiasi gani? Usiishi na maumivu! lipa au lipiza..!

Msamaha wako usikushushe, msamaha wako usikufanye kiumbe dhaifu na mnyonge, utu wako ni muhimu heshima na dhima yako ni vitu vya kulinda na kuzingatia mno. Ukishindwa kabisa kusamehe ukizidiwa na viwango vya uvumilivu wa kibinadamu usiumize roho yako andaa kisasi.

Kama ilivyo kwa msamaha ile nafuu unayoipata kwenye kusamehe basi ndivyo ilivyo hata kwenye kisasi! Kisasi humpa mtu faraja na amani ya moyo huridhika kuona amefanya jambo baya kwa mtu mbaya.

Tunaishi na wajuaji wengi kwenye jamii tunaishi na watu wanaojiona wao ni bora kuliko wengine wao ni zaidi kuliko wewe. Wao ndio wanaijua pesa kuliko wewe. . . .

Usimpe nafasi mtu wa namna hii atambe, ni lazima umfundishe ajue kuwa maisha yana pande nyingi kisha mfundishe kwa maumivu makubwa, maumivu atakayodumu nayo mpaka kifo.

LAKINI maisha ni kupanga na kupanga ni kuchagua. Fanya kile kitakachokupa nafuu ya rohoni na afya ya akilini kwakuwa uamuzi ni wako na mwisho utabaki wewe kama wewe.

Visasi, misamaha na malipizi vitabaki kuwa uamuzi binafsi kutokana na imani yako hofu yako na huruma yako.
 
Ukishindwa kusamehe lipa kisasi
Mkuu mshana jr, kuna mahali umejadiliwa humu kwamba makala zako zina chembe chembe za mafundisho ya kishetani. Je, huu si muendelezo wa hayo mafundisho unayoshutumiwa?
Mshana Jr, agent wa Shetani JF!?
Akitumia elimu yake aliyoipata nchini Afrika kusini ya Budhisim...na mchanganyo wa vitabu mbalimbali vya kishetani...ujuzi wake katika meditation na ulozi...
 
Mshana Jr Umeeleza Vyema Sana. Kwa Kuongezea, Ili Mtu Atoe Mzigo Uliomkaba Shingoni Basi Kina Mambo Mawili Hapa
1. Kusamehe,
2. Kisasi.

Lakn Lazma Tujue Kwmb Kusamehe Ni Jambo Gumu Sana Ambalo Wengi Wengi Tunalifanya Lakn Tunabaki Na Makandokando Na Hatuishi Kuelezea Tulilotendewa Huku Chuki Ikichukuwa Nafasi Kubwa Nyoyoni Mwetu.

Kusamehe Na Kusahau Si Jambo Rahis Kama Humtegemei Mungu.

Mshana Jr Watu Wangekuwa Wanakuelewa, Wangekuelewa Vizuri Sana Lakn Mlengo Wa Tafsiri Zao Kwao Ni Hasi.
 
Back
Top Bottom