Ume deal vipi na ndugu baada ya kupata kazi ?

haszu

JF-Expert Member
Oct 10, 2017
837
1,550
Kwakweli nimeona wengi wakisema ukiwaendekeza ndugu hutafika popote, siwezi sema sitafika popote ila kwa suala la ndugu mimi ni mmoja wapo wa waathirika, kiwango cha pesa nnachotumia binafsi ni kidogo sana mana sina starehe yoyote maarufu kama pombe, burudani au pamba kali nk. Niko simple, ila asilimia 30- 40 ya kipato nadhan ni ndugu. Ugumu ni kua kwa mazingira tuliokua hata ndugu anaweza asikuombe ila unaona kabisa ni jukumu lako kufanya hivyo.
Sasa unakuta siku zinaenda mambo yako pale pale. Nawezaje kubalance hivi vitu ? With minimal effects ?
 
Kuwasaidia unapoweza ni muhimu... Ila sio wakulazimishe huku wakutolee na maneno ya kashfa...
 
Kuwa na roho mbaya tu mkuu

kipindi nakua nilikuwa nasikia kwa majirani fulani "mjomba wao au baba yao mdogo ana hela yuko mjini hata hawasaidii ndugu zake ana roho mbaya"
 
Kwakweli nimeona wengi wakisema ukiwaendekeza ndugu hutafika popote, siwezi sema sitafika popote ila kwa suala pa ndugu mimi ni mmoja wapo, kiwango cha pesa nnachotumia binafsi ni kidogo sana mana sina starehe yoyote maarufu kama pombe, burudani au pamba kali nk. Niko simple, ila asilimia 30- 40 ya kipato nadhana ni ndugu. Ugumu ni kua kwa mazingira tuliokua hata ndugu anaweza asikuombe ila unaona kabisa ni jukumu lako kufanya hivyo.

Sasa unakuta siku zinaenda mambo yako pale pale. Nawezaje kubalance hivi vitu ? With minimal effects ?
km unaona ni jukumu lako basi bebaneni hivyohivyo maana si kitu chema kuona ndugu zako wanadhalilika wakati uwezo wa kuwasave unaona.

Ila hakikisha mambo yk hayakwami moja kwa moja..

angalia zaidi namna ya kuwainua kiuchumi nduguzo ili na wao wawe ma vipato vinavyojitosheleza( kwenye hili hakikisha unakuwa makini maana si kila ndugu anaweza Fanya biashara!
 
Kwakweli nimeona wengi wakisema ukiwaendekeza ndugu hutafika popote, siwezi sema sitafika popote ila kwa suala pa ndugu mimi ni mmoja wapo, kiwango cha pesa nnachotumia binafsi ni kidogo sana mana sina starehe yoyote maarufu kama pombe, burudani au pamba kali nk. Niko simple, ila asilimia 30- 40 ya kipato nadhana ni ndugu. Ugumu ni kua kwa mazingira tuliokua hata ndugu anaweza asikuombe ila unaona kabisa ni jukumu lako kufanya hivyo.

Sasa unakuta siku zinaenda mambo yako pale pale. Nawezaje kubalance hivi vitu ? With minimal effects ?
Weka akiba mkuu.
Mfano mshahara laki 6 wewe sema laki mbili sisikii la nani wala nani naweka akiba.

Ikiingia tu weka akiba laki mbili na uisahau kabisa kana kwamba huna pesa,kisha baada ya hapo uji yune kwamba una laki nne mfukoni hivyo matatizo ya ndugu yatatoka hapo hapo kwenye laki nne.

Binafsi suala la kumkomalia ndugu usimpe naona sio sawa kabisa kabisa eti kwa sababu ya kuwa hautoendelea sio sawa,bali ni mipango tu.

Hutakiwi kuwatenga ndugu,lazima uwasaidie kwa namna ya uwezavyo.

Mfano.

Kwenye laki 6 umeweka akiba laki 2.imebaki laki 4.
Una balancee balance hapo lazima katabaki kasenti,sasa labda ndugu anapiga simu anakopa alfu 30 unaweza kumuambia sina 30 hapa nna 15 tu,ukimwambia hvyo ataona kweli ulikuwa na lengo la kumsaidiaaa.

Sio kila akipoga simu wewe unatoa tu,lazima uangalie na uzito wa ndugu,mtu ana shida ya alfu 10 tu sio mbaya ukampa udugu uendelee.

Kuna wakati inatakiwa kuwa mbahili,weka akiba alafu hakikisha akiba yako huigusi labda mzee wako aumwee kweli kwelii
 
Kutosaidia wenzako ni roho ya kimaskini tu! Kwa mshahara mdogo huo unadhani ukidunduliza ndo utakuwa tajiri!
Wewe pambana uone namna ya kuongeza mapato yako na wala usisingizie na kutegemea ajira tu!
Ondokana na utumwa wa kifikra kuwa ukiwa na ajira na kamshahara basi maisha yako yatakuwa safi!
 
Kwaio hao ndugu matatizo yao yote ni kepewa hela? Au maana ukisema umpe hela mtu mwenye shida ya chakula i.e. 20,000 leo kesho kutwa inarudi tena shida ile ile..mimi watu hawajui hata ninapofanya kazi maana hua sisemagi nafanya kazi wapi nazuga zuga tu kwamba nahangaika mjini hapa hii inapungyza watu kukulilia shida..
 
kubana matumizi sio solution ya kupata hela nyingi...kusaidia ndugu hasa wale wa karibu sio mbaya ila usizidishe,,usiwape samaki wape ndoano moja na uwafundishe kuvua samaki....
 
Kwakweli nimeona wengi wakisema ukiwaendekeza ndugu hutafika popote, siwezi sema sitafika popote ila kwa suala la ndugu mimi ni mmoja wapo wa waathirika, kiwango cha pesa nnachotumia binafsi ni kidogo sana mana sina starehe yoyote maarufu kama pombe, burudani au pamba kali nk. Niko simple, ila asilimia 30- 40 ya kipato nadhan ni ndugu. Ugumu ni kua kwa mazingira tuliokua hata ndugu anaweza asikuombe ila unaona kabisa ni jukumu lako kufanya hivyo.
Sasa unakuta siku zinaenda mambo yako pale pale. Nawezaje kubalance hivi vitu ? With minimal effects ?

Huyu yeye anataka kuacha kazi kwasababu ya kusaidia ndugu na pesa anayo ipata kama mshahara haimtoshi/hapigi hatua
 
Mimi nitakapofanikiwa nadhani ndugu ndio watakaofaidi matunda yangu zaidi pengine kuliko hata Mimi
 
Huyu yeye anataka kuacha kazi kwasababu ya kusaidia ndugu na pesa anayo ipata kama mshahara haimtoshi/hapigi hatua
kumbe tuko wengi ? Mi siwez kusema niache coz bado sijawa na ramani za kueleweka
 
Kwaio hao ndugu matatizo yao yote ni kepewa hela? Au maana ukisema umpe hela mtu mwenye shida ya chakula i.e. 20,000 leo kesho kutwa inarudi tena shida ile ile..mimi watu hawajui hata ninapofanya kazi maana hua sisemagi nafanya kazi wapi nazuga zuga tu kwamba nahangaika mjini hapa hii inapungyza watu kukulilia shida..
inategemea na mzingira ,kwengine unakuta hata iyo kazi wao ndo wamehusika kukuunganishia
 
Kutosaidia wenzako ni roho ya kimaskini tu! Kwa mshahara mdogo huo unadhani ukidunduliza ndo utakuwa tajiri!
Wewe pambana uone namna ya kuongeza mapato yako na wala usisingizie na kutegemea ajira tu!
Ondokana na utumwa wa kifikra kuwa ukiwa na ajira na kamshahara basi maisha yako yatakuwa safi!
thanks mkuu, kama sijakosea unaniambia kua tatizo sio kusaidia tatioz ni kile ninachoingiza nipambane kiongezeke.

Whoever you are in your belief. May God/ Jehovah or Allah bless you,

Nadhan sina serving problem but nina income generating problem.
 
Back
Top Bottom